Rafiki hakuna biashara rahisi kama hii, na uzuri wa biashara hii haiitaji uharaka-haraka, kama wewe unahitaji milioni za chap-chap basi usiwekeze huku.
Rafiki yangu mmoja, juzi kati kipindi mchele umeshuka bei, alipiga mafao yake sehemu kama 6M, na mchele wa kawaida ulikuwa unauzwa mpaka kilo moja 800/=, akanunua kilo za hela yote (ile milioni 6) jumla kilo 6,000, halafu akazificha mahala, akaendelea kunganga njaa kwa vibarua vya hapa na pale.
Juzi kati hapa mchele umepanda mno na ameuza kwa kila kilo 1600/= (mean shilingi ikazaa shilingi). Jamaa kapiga noti milioni karibia kumi. Aisee ukiongea nae anakwambia kumbe kuwa bilionea ukivumilia inawezekana. Na anajipanga kufanya kwa ukubwa zaidi.
Nina ushahidi na hilo ndio maana nashauri huyu bwana autupie mzigo wote.