Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Malila hongera sana, unaonekana ni mjasiriamali mzuri na mwenye kupenda wenzako nao wafanikiwe, MOLA AKUZIDISHIE ZAIDI. Kweli shule inayotoka hapa inaleta mvuto kujaribu. Hongera Mbu kwa kuanzisha hili, na pia hongera kwa wachangiaji wengine pia, Next Level uko juu naona soon utamsaidia Yo Yo manake aliwahi uliza "jinsi ya kuwa tajiri".

Mfumwa;

Nakwambia Malila hapa kwa kweli kawa mzalendo sana! anakata issues acha kabisa.....!

Niliianza hii project nikiwa form two in 1995 but nikastop because msitu wote uliungua, sasa huyu jamaa kanirudishia uhai sana.......going back to that project! Nitakuwa nawaupdate wadau hapa...ofcourse together with the cashflows!
 
Mbu,
Sikuwa nimeona hiyo signature yako. 🙂
Masanilo ni member JF kama sijakosea?

...ndiye yeye huyo! 🙂

Mfumwa;

Nakwambia Malila hapa kwa kweli kawa mzalendo sana! anakata issues acha kabisa.....!

Niliianza hii project nikiwa form two in 1995 but nikastop because msitu wote uliungua, sasa huyu jamaa kanirudishia uhai sana.......going back to that project! Nitakuwa nawaupdate wadau hapa...ofcourse together with the cashflows!

...haki ya nani tena, ujasiriamali wa Malila na stanmokiwa wamenifurahisha sana katika thread hii. Duh, kumbe nawe tangu upo form two ulijaribu ujasiriamali, na sasa umepata mwamko mpya!

unajua yale maneno ya Mkapa; "watanzania ni wavivu wa kufikiria,..." si kwa wote aisee...!

"Kwa wale wasio tayari kujituma na wale wanaoingojea serikali iwafanyie kila kitu, hao wataachwa nyuma jambo ambalo siyo lengo la serikali," -Mkapa 11.1.2005
 
Malila, IR mko eneo gani hasa? Mi nakufahamu sana Njombe....sasa kule now kuna wajanja wengi sana wameshapanda miti na maeneo mengi yanatumika kwa kilimo cha viazi na mahindi!

Sasa hayo maeneo huwa yanaandaliwa muda gani? December? Je, huwa mnatumia workers wepi kuchimba mashimo....wanafunzi, au vipi na mnaotesha miche hukohuko IR?

BWT....Umeona reaction ya members hapa?......ngoja tuendelee kukata issues hapahapa!

kama wewe mjanja wa njombe,nakwambia nenda Moronga ni kijiji cha mwisho barabarani kama unakwenda Makete, kijiji kinachofuata upande wa kushoto kinaitwa Makangarawe kipo Makete,kuna ardhi ya kutosha bei iko chini bado. Ila mimi siko huko. Au nenda imalilo sio kipengere,Igosi au Mang`oto au lupembe,hakuna ardhi.

Mimi niko Kilolo kwa Msolwa ( je nikutajie na vijiji ?).Huko niliko/tuliko mashamba hayaandaliwi kwa sababu ni grassland tupu. kinachoandaliwa ni kitalu cha miche.Miche tunaotesha hukohuko kukwepa gharama na ndio maana tuko timu (nasikitika timu haina watu wa IR kabisa). Nina wanafunzi wanne tu wanaosoma Universities (Tumaini na UDSM). Tunatumia zaidi vijana ambao hawasomi kuliko wanafunzi. Desemba huwa tunatumia kuwapa angalao tusenti. 2009 tumeanza kutumia jumuiya za makanisa pia.
Tayari mwezi huu tunakwenda kuandaa kitalu cha pines,lakini mlingoti ni mwezi august.

Watu wa kule wana kiwango cha juu cha uelewa kuhusu athari za moto kuliko sehemu nilizopita.
 
Mfumwa;

Nakwambia Malila hapa kwa kweli kawa mzalendo sana! anakata issues acha kabisa.....!

Niliianza hii project nikiwa form two in 1995 but nikastop because msitu wote uliungua, sasa huyu jamaa kanirudishia uhai sana.......going back to that project! Nitakuwa nawaupdate wadau hapa...ofcourse together with the cashflows!

Nakwambia rudi ndugu yangu na sisi tuwekeze ktk ardhi. Wewe ulianza form Two,mimi nilianza darasa la sita. Mzee mmoja jirani kijijini aliniomba nikamsaidie kupakia miche ktk gari lake apeleke shambani kwake. Nikafanya vile, jioni alinipa miche 50 (pine/mlingoti) nikapande kwetu,baba akanipa kisehemu nikapanda. Huyo mzee kwa sasa anatisha,ila ameacha alama kubwa sana kwangu na kila mwaka ananikumbusha kupanda miti. Ukifaulu kushinda hofu ya moto,hii ni bonge ya biashara.
 
Nilipokiona kitalu cha Mkenya yule,moyo ulitaka kusimama. Hesabu rahisi ni hii. Kule tuliko,mlingoti wa nguzo unauzwa Tsh 15,000/ kwa bei ya leo. Jamaa amepanda milingoti 4,000,000 mwaka huu. Baada ya miaka kumi jamaa/familia yake wanaanza kuuza. (kwa hiyo 4,000,000 x 15,000/) kwa nini jamaa asiiweke serikali mfukoni. Kumbuka jamaa anapanda miti kila mwaka. Eneo hilo alitenga Marehemu ili Watz waje wawekeze pale.

Siku moja alisema,baada ya miaka kumi,nguzo zote za Umeme kwa nchi za Tz,Uganda na Kenya zitakuwa zimeoza na itabidi zibadilishwe. Serikali haipandi miti tena ya aina hiyo. Umeona hesabu za huyu mbwiga? Na kasema pia atajenga plant kulekule shamba na sasa anajenga ki-airstrip pale shambani kwake.
 
Bro Mbu kwako milioni kumi kama mwanaume ni vigumu kuku-sustain lakini hizo hizo 10m akizipata mmoja wa dada zetu hawa wa siku hizi wenye mwamko na biashara utashangaa baada ya miaka miwili ana maduka 2,gari na kaanza kujenga polepole.
 
wajameni eeh, nimebahatika "kupata" mahala ka-Mtaji. Ni kiasi cha shs. milioni kumi tu, (10,000,000/=) za Kitanzania.

Nipeni mapendekezo nizi invest wapi, kivipi na matarajio ya faida.
(i.e biashara gani inalipa (plus location), kwa muda gani, na SWOT analysis zake)

Nichotee, hali ngumu huku...Boksi zinatereza! LOL
 
Kwa wale wasio tayari kujituma na wale wanaoingojea serikali iwafanyie kila kitu, hao wataachwa nyuma jambo ambalo siyo lengo la serikali,” -Mkapa 11.1.2005

Hiyo kauli iko poa, ila nionapo kauli ya mfano huu hapa chini, sio rahisi nikaiacha bila kuisemea: "watanzania ni wavivu wa kufikiria,..."
Ni uvivu au ni kutoweza kufikiri?

Halafu hiyo kauli inatoa lawama badala ya solution. Kiongozi - tena kiongozi wa nchi akilalama lalama huenda nikamtusi.

Kuwajengea watoto wetu desturi ya kusoma vitabu itaondoa tatizo la "kushindwa kufikiri"
 
Wekeza kwenye kilimo. Lazima watu wale. Lima mpunga, utavuna, utauza, utakaobakia utakula wewe na familia yako. Suala ni: Una shamba? Kodisha, usinunue. Hakikisha kuna maji ya kutosha.... kilimo cha mpunga hakitegemei tena mvua siku hizi!
 
...haki ya nani tena, ujasiriamali wa Malila na stanmokiwa wamenifurahisha sana katika thread hii. Duh, kumbe nawe tangu upo form two ulijaribu ujasiriamali, na sasa umepata mwamko mpya!

unajua yale maneno ya Mkapa; "watanzania ni wavivu wa kufikiria,..." si kwa wote aisee...!

Haahaaaaa.....mkuu Mbu, kule kwetu ujasiriamali huanza tukiwa bado hatujaingia hata darasa la kwanza mkuu! Hiyo ya form two ilikuwa ni big project ya pines kama ekari kumi hivi, ila nikiwa kama darasa la kwanza na pili nilishapanda miti kama hamsini hivi....ambayo hii ilinipa ada ya Secondary!

Ila niliachana na hii kitu baada ya ekari zote 10 kuungua na moto......but Mkuu Malila kanipa ...Rejuvenation energy.........I will be back to my roots!

Cost ya kumag misitu, mi nafikiri ni moto tu.......nyingine ni rahisi sana!

Malila.........Nitarajie huko mkuu, you must see new faces this year!
 
I will be happy to see/meet you there. Ukitaka msaada wo wote kuhusu huko wasiliana nami.
 
Mradi mwingine mzuri wa bei nafuu ni mradi wa kukamua alizeti. Mwaka jana nilipata bahati ya kutembelea Singida kwa ziara ya kitume. Nikapata muda nikaenda mitaa ya sido. Nilitembelea viwanda vidogo vya kukamulia alizeti. Nikatafiti gharama za mradi wote ule. Kwa mujibu wa Sido,mtambo wenyewe unafikia Tsh 6,000,000/ kwa mwaka jana. Ila mitambo ya mitaani inaweza kuwa chini ya hapo. Gharama za jengo zinategemea sehemu.Ukiweza kufunga kimtambo hicho,mikopo ya upanuzi toka Sido ni mingi bila urasimu.

Wale jamaa wanatengeneza hela sio mchezo. Nimegundua pia kuwa watu wanarudi ktk matumizi ya mafuta ya nafaka sana na ukulima wa alizeti/ufuta unaongezeka sana.

Mr MBU think on this also
 
Malila: ninauheshimu sana mchango wako katika kuamzha fikira za wana JF katika suala zima la ujasiriamali ungizingati kuwa na mimi ni mdau katika eneo hilo. Kwa kweli waTZ wengi leo hii wamejikita sana kwenye biashara za uchuuzi yaani kununua bidhaa na kuuza (hasa bidhaa za kutoka nje kama China); lakini iko haja ya kuhamasishana na kurudi katika uzalishaji ambapo mwanzo wake ni kuwa mjasiriamali. Mimi naamini maendeleo hayapatikani kwa njia ya uchuuzi bali kwa kuzalisha. wakati umefika sasa kujikita katika shughuli za kilimo na ufugaji. WaTZ wengi tukipata vijisenti kidogo ni kukimbilia kununua "kiusafiri" na mambo mengine ya kutaka kuonekana na sisi sasa tunazo, badala ya kuangalia investment ambazo zitatufanya kuendelea kuwa nazo especially sisi tunaotumwa na wengine.
 
I will be happy to see/meet you there. Ukitaka msaada wo wote kuhusu huko wasiliana nami.

Mkuu kwa kweli mi takusumbua sana......june taenda huko bush ila nitapitia hapo Kilolo coz ninamaschool mates wengi pale.....later on takuPM unipe contacts details zaidi mkuu!

Stay blessed man!
 
Tanga,Kilimanjaro,Mbeya,Songea,Shinyanga,na Arusha ,shemu ipi kati ya hizi inafaa kwa kulima milongoti?
 
Tanga,Kilimanjaro,Mbeya,Songea,Shinyanga,na Arusha ,shemu ipi kati ya hizi inafaa kwa kulima milongoti?

Milingoti inakubali mikoa yote Tanzania,isipokuwa growth rate zinatofautiana kutoka mkoa mmoja na mwingine. But should be at the highlands plateaus. Mind you usipande milingoti karibu na mashamba ya watu wala vyanzo vya maji. Miti hii kwa ujumla inakunywa maji sana. Lakini kwa ufupi.Mbeya,Iringa,Arusha na Ruvuma, Tanga Lushoto/korogwe hali ya hewa inaruhusu miti hiyo kukua faster. Tatizo, Arusha/Mbeya/Klm ardhi ni tatizo. Shinyanga ukame.
 
Mkuu kwa kweli mi takusumbua sana......june taenda huko bush ila nitapitia hapo Kilolo coz ninamaschool mates wengi pale.....later on takuPM unipe contacts details zaidi mkuu!

Stay blessed man!

Karibu sana,hata mimi kuna watu walisumbuka kwa ajili yangu. Ukiwa tayari nitakupa detail za mawasiliano.
 
Malila,

..je, miti unayozungumzia ni Eucalyptus?

..ningefurahi kama ungetuelimisha kuhusu aina ya miti unayolima na inachukua muda gani mpaka kuvuna.

..wengine sisi tunapendelea mradi wenye mzunguko wa haraka wa fedha. je, ni miti ipi inakua kwa haraka zaidi na matumizi/soko lake ni nini?
 
Ndio ni Eucalyptus,lakini jamii hii ni ukoo mkubwa sana,kuna zaidi ya aina 300 kama sijakosea, sisi tunashughulika na aina mbili tu nazo ni saligna( baka jekundu na ndio maana huitwa mlingoti mwekundu)na grandis(baka jeupe). Soko la miti hii kwa sasa liko juu sana. Saligna hutoa mbao,boriti na nguzo za umeme kadhalika na grandis. Ubao wa mlingoti ndio umekuwa mbadala wa mbao ngumu(hardwood) kwa sasa pale dsm na kwingineko.

Kama shamba liko karibu na mji utaanza kuvuna baada ya miaka nane tu. Wajenzi wengi sasa wanatumia kujengea majengo ya ghorofa na hizi hotel za kitalii kwa sababu ya urefu na durability ya miti hiyo. Haina vibali vya uvunaji toka kwa serikali. Lakini muda mzuri kwa mlingoti ni miaka 10 mpaka 12 hivi. Wajanja wanaanza kufaidi shamba baada ya miaka mitano,hawa wakisha panda miti hiyo wanatafuta Title deed na kisha wanawahi benki. Kwa wenye kutafuta fedha za haraka misitu ya mbao sio mahali pao.

Mimi nakushauri kama una fedha za kupeleka benki,basi peleka ktk shamba la misitu kwa sababu biashara nyingine unafanya bila kuathiri msitu wako.Kama wewe ni mzazi,basi hazina nzuri ni misitu.

siku njema.
 
Tunashukuru saa kwa hili darasa. Hata mimi ningependa kujua miti ya aina gani unafikiri itaweza kustawi maeneo ya mkoa wa pwani eg mkuranga, chalinze. Kuna eneo nilitembezewa siku za nyuma.
 
Back
Top Bottom