Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

penyapenya upate kakorido maeneo ya mnazi mmoja karibu na jengo la red cross au huku ushirika ufungue ka - stationery office uweke computer zako 5 unajua tena used zimejaa kariakoo, printer ndogo mbili, copier used mbili, internet connection, then utaniambia. maeneo niliyokutajia kuna demand kubwa za hiyo sevice na hakuna reliable service providers au waliopo ni very few na demand ni kubwa wanawaburuza wateja, watu maeneo hayo wako busy kweli na makaratasi ila hawaonekani
 
mimi nakushauri kuwa invester maana michakato ya biashara huwa ina mikanganyiko mingi sana

na moja ya nyanja ambayo unaweza kuwekeza ni local real estate ya kibongo kwanini

1.soko ni la uhakika sasa hivi asilimia 99 ya wabongo akili yao iko katika kujenga si utawakamata nina uhakika
2. hauwekezaji huo hauna presha yaani uko zako ulaya na unasimamia kwa mbali kama rimote

cha kufanya nunua kiwanja chenye hati kabisa na ndio biashara yenyewe kwani nyumba ya 10m hakuna

pili hakikisha kuwa unaweka fence japo ile ya kuzungushia nyaya

tatu subiri ipite miezi sita tu au mwaka then kiweke sokoni kaka

madalali kibao ukiwapatia ofa yako tu wanachacharika kweli

mwisho usiwekeze 10m yote wewe nunua cha 7 au 8m

utakuwa na uhakika wa kuuza kati ya 12, 13, 14 au 15m

angalizo!

usiwe na haraka wakati wa kukiuza taratibu la sivyo utauza kwa bei ndogo

USHUHUDA
Kuna kakiwanja nilinunua mwaka 2007 kwa 3m na sasa ninaenda kukiuza wakati wowote kwa 40 au 45m

any swali nicheki kwa 0713 32 77 13
ushauli mzuri sana brother.!keep it up.
 
Mimi nilikuwa nataka kuanzisha "business" ya food supplv hapa DAR. Inalipa sana!Tayari nimekwisha ifanyia mchanganuo wa kutosha! Kuweza kuanzishwa muda wowote kuanzia sasa,
ila mtaji ndio issue!. Kama vipi tufanye "partinership" in kama utakuwa tayari!!
0714306015
0759601820
 
Mimi nilikuwa nataka kuanzisha "business" ya food supplv hapa DAR. Inalipa sana!Tayari nimekwisha ifanyia mchanganuo wa kutosha!
ila mtaji ndio issue!. Kama vipi tufanye "partinership" in kama utakuwa tayari!!
0714306015

0759601820
 
Mbu, mtaji wako ni mdogo na biashara za tender zinataka pesa zaidi ya hizo 10m. Ukitegemea tender unaweza kulaza familia kwa njaa na kupata maisha magumu kwani hao serikali kuwasupply si tatizo lakini wakati wa malipo utazungushwa hadi utoe rushwa. Kwa tabia hio mara ya kwanza na ya pili utafanya biashara. Lakini mara ya tatu sija ukawekwa kwa list ya mafisadi maana baada kuzungushwa sana ulipo supply mara ya kwanza na pili basi nawe unakuwa sugu na unaanza kusupply hewa upate pessa za bure nk. Mambo ya tender usiyafikirie nakushauri.

Kama unataka kuwa tajiri basi biashara ya tender Ndio yenyewe. Ingawa Kuna risks. Lakini Unaweza kupunguza risk hizo kwa kiasi kikubwa.

Mimi Nipo katika biashara hii. Kama upo serious nita-inject million 10.
Napatikana 0655308308 au 0767102102.
 
...dah, kaka masuala ya ubunge wala sina fikra hizo, japo ni ukweli usiopingika miaka mitano bungeni, ni 'return' nzuri ya mtaji utaoweka!

hee ubunge si kusaidia tena wananch ishakuwa sehem ya ku invest mungu zidi kuangazia watu wako wanateketea kwa maarifa ya watu wengine
 
Wataalamu wa uchumi na biashara kwa mara ya kwanza toka nijiunge na huu mtandao leo ndio nimekuja na andiko mahususi kuomba ushaur.in short mi bado mgeni humu

nipokeen ndugu..ila nyie mnatumia et WAKUU...hahaha n furaha sana

mimi nipo kwenye hatua za kuomba mkopo ktk moja ya taasis za fedha hapa nchini

mkopo wa shiling takriban million sita (6)

vipaumbele na mchanganuo wangu ulikuwa ni huu

1.2,500,000tsh kununua pikipiki ya biashara.bodaboda

2..2.000.000...kununua shamba/kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba...

3.1,000,000 (milion moja) kununua alizet ambayo nitakamua mafuta na kuuza baadae

4.500,000..zawad ya mama...kmbka wimbo wa Banana zoro 😀mama yangu japo ameshakuwa mwana.ccm..sijaskiliza tena

ushauri wenu wandugu..aaaaaaa WAKUU
naamini ntaondoka na kitu leo
 
tuambie sehemu unayotarajia kuwekeza ili tujue pa kuanzia , pia wazo linaanzia palepale unapotoka....je kuna mapungufu yoyote ambayo yatakupa fursa?......fanya utafiti mkuu!
 
huo mkopo masharti yake yakoje kulipa? mbona ushaandika mchanganuo tayari japo huo mchanganuo hauko makini labda ndio malengo yako.

unaishi wap? na huo mkopo utalipa kwa muda gani na riba?

je una kazi nyingine?
 
Hiyo laki 5 itumie kuweka insurance ya pikipiki yako maana utachanganyikiwa pale ambapo dereva atapigwa na kuibiwa hiyo pikipiki,itakayobaki weka kama backup ya investment yako ya arizeti then faida ya hizo biashara zako ndio umnunulie mama zawadi.

In short inaonekana hujafanya risk analysis ya investments zako japo kwa upande wangu naona ni investments ambazo zitalipa hasa ya bodaboda
 
Kwa mchanganuo wako "mdau" maisha ni rahisi sana
 
Hapo kwenye bodaboda unaweza kupata kwa Tshs. 1.7 mil MPYA. Kisha ingia mkataba na dereva wa kumuachia bodaboda kwa muda fulani ili uepuke risk ya chombo kukufia mkononi, miezi kumi upendekezwa zaidi.

Kuhusu arizeti naona kama umefanya makadilio kimakosa. Huo mtaji sidhani kama utakuwa na tija yoyote kwenye hiyo biashara.

Angalizo: pesa ya mkopo itumike kwa ajili ya biashara yenye faida kwa kuwa mkopo uandamana na riba.
 
Na ule umbwiga wako wa kufunga biashara ili uende kwenye mikutano ya chadema,mafanikio ni ndoto ya mchana.
 
Back
Top Bottom