KWELI Mtanzania Bara huruhusiwi kuendesha gari Zanzibar bila kuwa na kibali maalum

KWELI Mtanzania Bara huruhusiwi kuendesha gari Zanzibar bila kuwa na kibali maalum

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Huu Muungano ni chenga kabisa una kero nyingi mno, naona kwa Zanzibar wao ni raha kwenda mbele.

Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria.

Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar.

Huu Muungano ni wa kishenzi sana.

Bilikundi.jpg

Tunachokijua
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa Aprili 26, 1964 ikiwa ni Muungano wa Mataifa mawili huru ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo yaliingia mkataba wa Muungano mnamo mwaka 1964 na kuanzishwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964 huko Zanzibar.

images

Picha: Mwalimu Julius Nyerere (kushoto) na Sheikh Abeid Amani Karume (kulia) wakibadilishana Hati za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili, 1964.
Sababu ya Muungano
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwepo kutokana na sababu mbalimbali kama vile kuwepo kwa mahusiano ya karibu na ya kihistoria baina ya Tanganyika na Zanzibar katika nyanja mbalimbali kama vile undugu wa damu, biashara, utamaduni, lugha na mahusiano ya karibu kisiasa hususan baina ya vyama vya TANU na ASP.

Pamoja na kuwepo muungano lakini Tanganyika na Zanzibar hazikuungana kwenye kila jambo bali kwa baadhi ya mambo tu, hivyo kuwepo kwa mambo yahusuyo Muungano na ambayo hayahusu Muungano hivyo kila upande huyashughulikia bila kuhusisha Muungano.

Je, Mtu wa Tanzania bara anaruhusiwa kuendesha gari Zanzibar kwa kutumia leseni yake aliyopewa na TRA?

JamiiForums Imezungumza na Kamanda wa Polisi Ramadhani Ng'azi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, ambaye amekiri kuwa:

"Ni kweli mtu hawezi kutumia leseni yake aliyopewa na mamlaka ya Mapato Tanzania( TRA) kwasababu Mamlaka ya utoaji wa leseni sio jambo la kimuungano hivyo Mamlaka za utoaji wa Leseni kati ya Tanzania bara na Zanzibar zipo tofauti.

Tanzania bara Mamlaka inayotoa leseni ni TRA, baada ya kupata uthibitisho kutoka jeshi la Polisi kuwa mtu huyo amesomea udereva na amepitia mitihani ya polisi au utahini wa polisi na kupewa hati maalum ya kufaulu na kwamba mtu huyo anatakiwa kupatiwa daraja fulani la leseni.

Baada ya TRA kupokea taarifa ya uthibitisho kutoka Polisi hutoa leseni kulingana na maelekezo ya jeshi la polisi kikosi cha usalama Barabarani.

Lakini Zanzibar wao wana mamlaka yao ya utoaji leseni ambayo ni tofauti na huku Bara na ndio maana wameweka utaratibu mtu akitoka huku kwenda kule ataomba kibali maalum kwa kuwa mamlaka ya utoaji leseni siyo jambo la kimuungano.

Hivyo
mtu akienda Zanzibar ataomba kibali maalum na vivyo ivyo mtu akitoka Zanzibar kuja bara ataomba kibali maalum ili aweze kuendesha gari".

Pia, JamiiForums imezungumza na Abubakar Nassor Ali Mkuu wa Divisheni ya Upasishaji Madereva, Mamlaka ya usafiri na usalama barabarani Zanzibar, ambaye amesema kuwa:

"Kimsingi tunapozungumzia suala la usafirishaji, Tanzania tuna sheria 2 tofauti, zikiwa na lengo moja la udhibiti wa usalama barabarani. Huko bara mna sheria ile namba 30, ya mwaka 1973 (Road Traffic Act) lakini Zanzibar tuna sheria namba 7 ya mwaka 2003 kwa ivyo ni sheria 2 tofauti ila lengo ni moja la shughuli za usafirishaji.Na hii kutokana na jambo hili kutokuwa la kimuunano.

Kwa maana Zanzibar tuna sheria yetu, sheria hiyo ndio inashughulika na mambo mbalimbali ya leseni, na inamtaka dereva yeyote awe na leseni.

Sheria yetu inatuambia mtu yoyote ambaye atatoka nje ya nchi, inamtaka mwenye leseni ya udereva mbali na ile iliyotolewa na Msimamizi Mkuu wa usafiri barabarani( Mkurugenzi wa mamlaka na usalama Barabarani) kwenda kufanya jaribio au kuangalia afya au kufanya mtihani ili kupima uwezo wake wa uendeshaji chombo cha moto akiwa ndani ya nchi.

Kwa maana hiyo mtu yoyote ambaye atakuwa na leseni ya nje ya nchi( nje ya nchi hapa ni pamoja na Tanzania bara)
anatakiwa kukata permit, kwa hiyo kwetu mtu yoyote ambaye atakuwa anatokea bara maana yake anatokea nje ya nchi, na anatakiwa kukata Permit (kibali maalum) ambapo kwa sasa gharama yake ni 15,000 ambayo hudumu kwa miezi 3.

Na kwa yule ambaye atakuwa anataka kuendelea kukaa Zanzibar kwa muda mrefu zaidi au kuweka makazi ya kudumu basi ana uwezo wa kubadilisha leseni yake, yaani atakata leseni ya huku Zanzibar,( hatubatilishi leseni ila atabaki nayo ya bara na atapewa nyingine ya huku baada ya kufuata taratibu za kuchukua leseni huku)

Mtu atakayekiuka sheria hii na kuendesha bila leseni atakuwa ametenda kosa, Kosa la mtu kuendesha bila leseni hapa ni kwa wageni wote ( nchi nyingine pamoja na wa bara) adhabu yake ni faini ya dola zisizopungua 50 ambapo kwa sasa ni sawa 116,500".

bilikundi-jpg.2703699
JamiiForums baada ya kusoma mambo yahusuyo muungano na kujiridhisha kuwa suala la usafirshaji si la kimuungano na kuzungumza na mamlaka za usafirishaji pande zote 2 za muungano ambao wamekiri mtu anayetoka upande 1 kwenda mwingine anatakiwa kukata kibali maalum ivyo imejiridhisha kuwa ni kweli Mtu wa Tanzania bara haruhusiwi kuendesha gari Zanzibar mpaka akate kibali maalum(permit)
Huu Muungano ni chenga kabisa una kero nyingi mno, naona kwa Zanzibar wao ni raha kwenda mbele.

Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria.

Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar.

Huu Muungano ni wa kishenzi sana.

View attachment 2703699

Sio Mtanganyika. Bali rais yyt asiye mznz.
 
Normalize reading between the lines big man. Ubaguzi na matabaka huanzia kwenye majina watu wanayoitana na ndio maana majina kama gringo, nigga, mzungu na mengineyo yanaweza kuwa yanayotumika kuashiria uhalisia wa ethnicity ya mhusika ila huchukuliwa kama offensive yakitumika in most cases.

Kwetu Tanzania tuna makabila zaidi ya 126 na kwakua nchi yetu ndio home of pan-africanism, wala hatuoni noma kutaniana na kuitana "we mpemba, we msukuma, we muha" na kadhalika kwakua tumefundishwa utani na hivyo hatuchukulii uzito kama maeneo mengine ya dunia. Hata hivyo, name-calling has never been ideal anywhere in the world kwakua inapandikiza chembe chembe za migawanyiko na ubaguzi.

Wewe umeona tu kuitwa "mtu wa bara" hilo la "waDanganyika" hujaliona eti eeh? MUUNGANO HUU HAUNA USAWA NA MTU YOYOTE MWENYE AKILI TIMAMU HAHITAJI MIWANI KUONA HILI.

mbona na nyinyi wapemba munawaita wapemba?
 
Huu Muungano ni chenga kabisa una kero nyingi mno, naona kwa Zanzibar wao ni raha kwenda mbele.

Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria.

Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar.

Huu Muungano ni wa kishenzi sana.

View attachment 2703699
lakini kama ndo ivo kwenye muugano kuna udhaifu kwel basi na mzanzibar akija tanzania bara asipate ardhi au apitie vikwazo kama kule
 
Makubwa. Ivi why even bother? Zenj is 0.1% ya Tanganyika and less than 2% of its pop and we have access to the ocean from Tanga, Pwani, Dar, Lindi na Mtwara; Yaani except ilo jina la Tanzania tunahitaji nn hasa from Zenj?🤐🤐🤐

ABSOLUTELY NOTHING, INFACT ZANZIBAR IS A TICK ON OUR NATION.
 
Ndio Maana ukaitwa Muungano Wazanzibar waan sheria zao sisi Wabara tunatumia sheria za Muungano kwa hiyo ukiwa bara unafanya utakavyo ukiwa unguja unapangiwa sheria zao kwani kule kuna Serikali yake haihusiani na Serikali ya Muungano.Kuna mambo ya Muungano na kuna mambo yasio ya Muungano ndio hivyo.
Halafu ukaona ni sawa tu ?!. Hivi mTanganyika anakoswa nini mpaka alazimike kujidhalilisha kwa zanzibar ?!.

Mambo mengine yanakera tena bila ganzi .
 
Usalama wa kusarenda rasilimali kwa kina wajomba !!.

Si ndo hapo! kwanza tujilinde dhidi ya Zanzibar ama nani? Maana kama ni usalama tu mpaka sasa usalama wetu uko in jeopardy tayari, angalia ata security procedures zilivyo pale ferry kwenye boat zao. Yaani ukiwa unaenda Zenji kitambulisho/passport mkononi kwenye checkpoint zote, ila ukiwa ukitoka kwao kuja huku yaani ukaguzi hauna uwiano hata kidogo. Mamluki kibao wanapita kuingia kwetu.
 
Huu Muungano ni chenga kabisa una kero nyingi mno, naona kwa Zanzibar wao ni raha kwenda mbele.

Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria.

Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar.

Huu Muungano ni wa kishenzi sana.

View attachment 2703699
ila wapemba wanaendesha gari wapendavyo na popote. huu muungano sijui utavunjika lini aisee. Kakobe alisema its just a matter of time, muda ufike hawa wala urojo warudi tu kwao wakamezwe na maji huko.
 
Wanzanzibari wasiotaka muungano ni wale masikini, vijana wa vijiweni

Ila 80% ya wanzanzibari waliopo bara hawataki kurudi kwao, wakafanye nini?? Wanaajiriwa bure, wanamiliki mashamba, biashara etc etc

Wanadanganywa Zanzibar itakua kama Dubai, wajiulize Shelisheli, Madagascar wamekua kama Dubai??

Uislam wa mtu mweusi hautajirishi bali unaongeza umaskini tu
Wewe nawe huna hoja mbona hao wazanzibari wapo hata kenya na wengine wamewapa uraia

Sent from my ATU-L31 using JamiiForums mobile app
 
Anazuiliwa kwa kuwa bado dawa ipo jikoni, ikiipuliwa, ipoe na watu wanywe, hatazuiliwa tena kuendesha gari.
 
Mkuu Anyisille

Wazazibari tumo katika muungano na tanganyika kwa kulazimishwa tu. kila miaka mitano watanganyika wanaleta mapaka vifaru ili kuhakikisha muungano bandia unabaki. Hakuna mzanzibari yoyote anayetaka muungano. Nyie ni watu wengine na sie ni watu wengine kabisa. hakuna uhusiano wowote baina yetu zaidi ya kwamba niye ni binadamu na sie ni binadamu.

kwanza uvunjike tu tuone mtakula nini wavivu nyie
 
First off, Zanzibar haijawahi kuwa empire mkuu ilikua ni sultanate. Na kuhusu kauli yako ya "once an empire, forever an empire", ziko wapi Ottoman, Mongolian, Shongai na empire zinginezo leo hii?

Kingine, Zanzibar haijawahi kuitawala Afrika Mashariki yote bali pwani yake tu na hii haikuwa kwa muda mrefu na wala haikuwa kimabavu bali ni kiuchumi.

Eti "Zanzibar haifaidiki chochote na Tanganyika"😂 hata malaika wanakucheka huko waliko. Umeme mnatoa wapi? Mnakuja huku mnanunua mashamba na viwanja na mnajenga makazi yenu kwa amani tu, hii sio faida? Faida ni nyingi kiasi kwamba muda wa kuainisha yote hapa sina.

Hili suala la waZanzibari kuwa colonialists na kuwa waArabu😂 naomba nijibu kwa kucheka tu.

AY 5225

Tulia nikujibu, tatizo sijui ukubwa wa ufahamu wako wa mambo ya dunia. Lakini hatahivyo nitakujibu upate kucheka. Nitakwenda deep kidogo, ikiwa ni above your capacity utaniwiya radhi kwa hilo.

1 Kwanza Sultanate haikuwa Empire, Zenj Empire, ndio ilokuwa Empire. Sultanate ilikuwa Serikali ya zanzibar. Ingawaje ni ukweli kwamba waliojenga Zenj Empire wahakuwa waafrika. Walipofika wageni zanzibar, wa Iran na waarabu hapakuwa na mtanganyika zanzibar. siku hizo watanganyika wahakuwa na sababu ya kwenda zanzibar, walikuwa na maisha yao na wanyama wao, watanganyika wote waliofika zanzibar waliletwa kwa ajili ya kazi au kuolewa.

2 Zenj Empire ilikuwa ikiendeshwa kutoka zanzibar, iliitawala afrika mashariki yote na kulikuwa na magavana tu huko tanganyika na miji mbali mbali ya afrika mashariki. kwa mara ya kanzwa tanganyika ilipoanza kujiendesha yenyewe japo kibendera tu ni baada ya uhuru 1961. na ndio maana mumeshidwa kujiongoza kwasababu hamuna historia ya kujitawala, hamuna uzoefu wa kujitawala. mulikuwa mukitawalia miaka yote ambayo historia ilipoanza kuandikwa.

3 Ndio narejea tena zanzibar haifaidiki na chochote kutoka tanganyika, umeme kama ulivyoutaja ni mipango ya muda mfupi tu, katika mipango ya muda mrefu hakuna faida yoyote tunayoipata kutoka tanganyika. kumbuka nyie wenye tanganyika muko hahe hoe, taaban kwa shida na dhiki na usumbufu munaopeana wenyewe kwa wenyewe. Leo umeme unaweza kupatika kwa njia za upepo, Hydrogen, juwa, bahari na hata kutoka kenya. In fact, zanzibar ilikuwa nchi ya tatu kutumia umeme duniani.

4 Zanzibar kuwa colonialist na empire forever. labda nikuchukwe nyuma kidogo, zamani kulikuwa na Ottoman Empire, persian empire, zenj empire, japanese empire na empire za kichina. Ukitizima uhusiano baina hizi empire za zamani katika maisha ya leo utanona kwamba empire zote hizi zimebanwa na global political dominance ya watu weupe. hawa watu weupe wanazo taasi zao kama vile UN na matawi yake, makanisha na taasisi za kijasusi ili kuhakikisha empire hizi hazirejei na kukuwa tena.

Hawa hawa watu weupe ndio wanoiwekea vikwazo Iran, Turkey, China na hata japan waliifanyia hivyo hivyo zamani na hadi leo hii japan hawana ruhusa ya kuunda baadhi ya silaha. sabau kubwa ni kwamba nchi hizo zote zilikuwa empire na wakati huu empire wanailzimisha iwe ya watu weupe tu kupitia wamerikani.

Kuhusu zenj empire, wanaizuia kupitia muungano. ukitizama kijuu juu utadhani dodoma inalazimisha muungano, si kweli, watanganyika hawana uwezo hata wa kusafisha ucha mitaani, wanaohakikisha muungano unaendelea ni hao hao wanaoiweke vikwazo Iran, Turkey na china, huku wanatumilia ofosi yao iliyoko nairobi. Leo waondoshe mikono yao, haifiki miaka 50 zenj empire will be back. na nyie watanganyika mutarudi tena katika himaya yetu.
 
Ulipoanza mwanzoni kwa kudhihirisha mashaka yako juu ya ufahamu wangu, sikutumia hata sekunde mbili kujua kwamba wewe ni mropokaji uliebarikiwa uwezo wa kujua namna ya kuishi tu ili siku ziende. Nilipoendelea kusoma zaidi nikajua, hell yeah! my prejudice was right.

Fallacy yako kitaalamu tunaiita AD HOMINEM, kwakua badala ya kujenga hoja ya utetezi wewe ukaanza na kuonyesha wasiwasi wako juu ya ufahamu wangu. Ila usijali ndugu yangu, umekutana na mimi jobless mwenye muda mwingi zaidi ya majukumu, hivyo nitakuelewesha na utaelewa.

1. Kabla ya yote, nakuomba kama itakupendeza unifahamishe zaidi japo kwa ufupi kuhusu Zenj empire maana ni ukweli usiopingika kwamba hakuna ninachojua kuhusu Zenj Empire. Kwa ufahamu wangu wa historia ya Africa, Zanzibar ikiwa ndani yake, hakuna empire iliyowahi kuitwa Zenj empire. Ni mwaka gani hii empire ilikuwepo?

-Kwa kuongezea tu kwenye hili la kwanza, jina Zanzibar limetokana na maneno "Zang" na "bar" ambayo yanatokana na Persian yakimaanisha LAND OF THE BLACKS, key word BLACKS. Kuna mZanzibar mwenzio mwehu alikuja hapa akasema eti nyinyi ni waArab na ni natural born colonialists, hazijapita hata siku tatu umekuja wewe nakutuambia kuhusu Zenj Empire na kwakua umekiri kwamba haikuundwa na waZanzibari wenyewe (that's if the empire even existed at first), naomba nikuulize wewe mwenye ufahamu mkubwa, HOW CAN AN EMPIRE YOU DIDN'T BUILD BE YOURS?

Nimepata ka'deal kamoja hapa, wacha nikapambanie hela yangu ya kula leo kisha nitakuja kumalizia kukuelewesha ndugu mZanzibari.

Ombi langu ni moja tu kabla sijasahau, kindly work on your thinking, typing and language skills. Haiwezekani utuandikie 'munasema badala ya mnasema' na mu mu zingine kibao kwenye chapisho lako.
 
Back
Top Bottom