Wana bodi saalam!
Wanajukwaa, mtukufu wetu amekuwa akisema kuwa corona ni vita kama vita zingine.
Kila vita ina siraha zake, na vita hutokea kwa sababu nyingi.
Hatujui vita ya corona imekuja kwasababu gani!
Lakini uasi pia ni vita, kununuliwa nako ni vita.
Kama vile walivyowanunua wabunge wa chadema na vyama vingine vya upinzani.
Ilikuwa vita ya kuua upinzani nchini.
Kama dr silaa alivyonunuliwa ilikuwa ni uasi na ni vita.
Leo hii mtukufu anahisi wanaopima corana katika maabara wamenunuliwa na mabeberu.,
Je hii vita anapigwa nani?
Kununua vipimio fake ni vita,
Hii vita anapigwa nani?
Hii ni kwakuwa watumishi wanajambo wanaolidai kwa awamu hii kwa matendo?
Wanajiona hawana thamani kuliko vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo mh, amevipa kipaumbele kuliko taaluma?
My taje,
Ukizoea kununua wengine, ili waasi walipokuwepo jua nawe kuna siku watakuasi
CHUMA HUNOA CHUMA.
TAFAKARI CHUKUA HATUA
Sent using
Jamii Forums mobile app