sabuwanka
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 691
- 757
Ndungu zangu waislamu asalaam aleykum, ndugu zangu wakristo wa CCT Bwana Yesu asifiwe, ndugu zangu wakatoliki tumsifu Yesu kristu! ndugu zangu wasabato Maranatha!
Awali ya yote napenda kumshukuru mola wetu kwa kunikirimia uzima na kuendelea kunitunza na familia yangu, mtakumbuka mwanzoni wa janga la Corona tulisikia limeshika Kasi huko China likaua maelfu, ikaja italy wakafariki maelfu, hispania wamefariki maelfu, kadhalika huko marekani mpaka May 24 walikuwa wamefariki zaidi ya watu 100036!
Cha ajabu sie watanzania mpaka leo kuna vifo 10 tu vya Corona na wagonjwa wakipungua kutoka 506 hadi 0
Kwa kweli ni jambo la kumshukuru Mungu aliyesikia maombi yetu yakiongozwa na jemedari wa imani Rais John pombe magufuli, ambaye kwa nyakati tofauti amehimiza watanzania bila kujali dini zetu tumuombe Mwenyezi Mungu atukinge na janga la Corona, na hata baadae akaomba tuwe na ibada ya shukrani ya kumshukuru Mungu kwa kutulinda dhidhi ya Corona.
Kwa kweli nawapongeza pia wote waliotikia wito wa kuomba na kwa maombi yao Tanzania imeishinda Corona, shukrani ziwafikie ndugu zetu waislamu ambao katika mfungo wa ramadhani walishiriki kuombea nchi ya Tanzania.
Kwa imani hii, ni wakati muafaka wa kuishinda kansa, ukimwi, T.b, na magonjwa mengine yote
Asante Mungu kwa kusikia maombi yetu
Mungu ibariki Tanzania