#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Ndungu zangu waislamu asalaam aleykum, ndugu zangu wakristo wa CCT Bwana Yesu asifiwe, ndugu zangu wakatoliki tumsifu Yesu kristu! ndugu zangu wasabato Maranatha!

Awali ya yote napenda kumshukuru mola wetu kwa kunikirimia uzima na kuendelea kunitunza na familia yangu, mtakumbuka mwanzoni wa janga la Corona tulisikia limeshika Kasi huko China likaua maelfu, ikaja italy wakafariki maelfu, hispania wamefariki maelfu, kadhalika huko marekani mpaka May 24 walikuwa wamefariki zaidi ya watu 100036!

Cha ajabu sie watanzania mpaka leo kuna vifo 10 tu vya Corona na wagonjwa wakipungua kutoka 506 hadi 0
Kwa kweli ni jambo la kumshukuru Mungu aliyesikia maombi yetu yakiongozwa na jemedari wa imani Rais John pombe magufuli, ambaye kwa nyakati tofauti amehimiza watanzania bila kujali dini zetu tumuombe Mwenyezi Mungu atukinge na janga la Corona, na hata baadae akaomba tuwe na ibada ya shukrani ya kumshukuru Mungu kwa kutulinda dhidhi ya Corona.

Kwa kweli nawapongeza pia wote waliotikia wito wa kuomba na kwa maombi yao Tanzania imeishinda Corona, shukrani ziwafikie ndugu zetu waislamu ambao katika mfungo wa ramadhani walishiriki kuombea nchi ya Tanzania.

Kwa imani hii, ni wakati muafaka wa kuishinda kansa, ukimwi, T.b, na magonjwa mengine yote

Asante Mungu kwa kusikia maombi yetu
Mungu ibariki Tanzania
 
VYOMBO VYA habari duniani vinamuita rais wetu bolsonaro of Africa kwasababu ya namna wanavyofanya katika kushughulikia janga la corona.

Wakati kwetu hakuna Ushahidi wa kisayansi kwamba KORONA imeisha kwa maombi tunaendelea kuambiwa kwamba imeisha .

Brazili wamekataa upuuzwaji wa bolsonaro nasasa wako mabarabarani wakimtaka ang'oke.

Sisi wakwetu tunamuita mbarikiwa na mpakwa mafuta Musa alietuvusha.

Naomba washauri wake wamshauri pia tuombe kwa Mungu ukimwi utoweke kama corona ilivyotoweka kimaajabu.
 
Vifo ndo sababu ya wabrazil kupata nguvu ya kufanya hivyo...tizama hapa kwetu serikali imekaa kimy na raia tupo kimy hakuna visa vipya wala vifo vinavyotajwa kutoka pande zote mbili.
 
Wa Brazil wanajitambua sana
Wanajituambuaje wkt ndio wapili kwa.maambukiz duniani?
Anyway kukurudisha nyuma tu ni kuwa rais wao alionywa kuwa ugonjwa huu ni hatari kwa hiyo achukue hatua,lakin kwa siasa zake akafanya mizaha..
Akidai ni mafua tu ya kawaida.
Leo hii mdharua mwiba umemchoma, anatafuta pa kutupia lawama. Too late
Upinzan alionao umeongezeka sababu ya uzembe wake mwenyewe.
 
Kuna wakati mtu unajiuliza hivi tatizo nini? Mkuu anasema Corona imekwisha na wananchi wawe huru , mpaka mzee wa watu SPIKA kaambiwa kwenye kiti yupo peke lakini anakazana kuvaa Barakoa , baada ya kuambiwa hivyo kaacha kuvaa , ikiwa ishara ya kusema kuwa corona imekwisha nchini Tanzania tu , lakini nchi za jirani maambukizi yanaongezeka kila kukicha , hofu ipo kwa wananchi lakini kutokana na kauli ya mkulu watu wote wanashindwa kuamua yaani ni kwa pamoja na wananchi , viongozi wa dini , viongozi wa serikali wote wamevurugwa na sasa hawajui wasimamie wapi , lakini ukifuatilia vyombo vya habari ya hapa nchini hususani katika taarifa za habari , utaona habari nyingi tu zinasema taasisi fulani imetoa wa vitakasa mikono pamoja na ndoo za vitakasa mikono kadhaa kwa ajili kujikinga na virusi vya Corona , LAKINI UKIRUDI KATIKA NYUMBA ZA IBADA MKUU ANAKUAMBIA MUNGU AMETUSIKIA NA CORONA IMEEISHA KABISA , huku si kuvurugana jamani .... KWANINI WATAALAM WA AFYA MNALIACHA HILI JAMBO KWA NAMNA HII ?..... kama Corona ipo watu waambiwe ipo lakini taadhari ichukuliwe lakini sio kauli hizi za kupotoshana....
 
Wadau sio siri mi hadi sasa sielewi,hivi hii corona imekuwaje hapa bongo???!!..kwa jinsi serikali ilivyochukua hatua kupambana na hii corona,halafu nikiangalia masimulizi ya watu wanaishi huko mamtoni,ulaya..nikiangalia worldmeter huko idadi ya vifo toka mwezi wa 9 mwaka jana, hadi leo hii ,nikisikia habari za lockdown, napagawa zaidi nikiangalia idadi ya walioathirika na hiki kirusi hapa Africa..!! tangu kesi ya kwanza ule mwezi wa 3, yule mama wa moshi hadi leo hii wabongo tunaishi ishi tu hatuna hata habari, huku uswahilini mtaani kwangu watu wanapiga tu mishe zao hakuna cha barakoa wala nini, watu tunakusanyika tu hatuwazi yan!!..sasa hii corona vipi!!?

Yaani jinsi inavyosemwa kuhusu hii corona basi hapa mtaani kwangu tungekuwa tunazika tu watu kila aiku kutokana na jinsi ambavyo waswahili tumechukua hatua,lakini cha kushangaza toka mwezi wa tatu tumezika mzee mmoja tu (alale pema),Naye alikuwa na maradhi ya kisukari miaka mingi..

Sasa mi najiuliza zile taarifa tulizokuwa tunapewa na WHO ,zilikuwa za uongo au??!!..je kuna sehemu tulidanganywa??!lakini mbona mchi jirani wenzetu kenya,uganda,rwanda maambukizi ndo yanashika kasi???..sisi tulipatia wapi?..au kwa sababu tunafichwa taarifa??..lakini kama tunafichwa kesi za corona,kwa jinsi hii corona inavyotajwa ni wazi tungeokota maiti huku buguruni, tandale, kariakoo, vingunguti, gongo la mboto!?? Au muda haujafika!!..lakini ni miezi 3 sasa!!!

Kifupi nina maswali mengi sana juu ya hii corona na Tanzania, sielewi hadi sasa...nini kimetokea Tanzania na corona
 
Thanks to prayer by citizens???? Medical professionals must be appreciated if country is free of virus not just prayer
 
Wadau sio siri mi hadi sasa sielewi,hivi hii corona imekuwaje hapa bongo???!!..kwa jinsi serikali ilivyochukua hatua kupambana na hii corona,halafu nikiangalia masimulizi ya watu wanaishi huko mamtoni,ulaya.
Kwa tunaoamini uwepo wa Mungu. Tunaamini amesikia maombi yetu na ametuokoa. Mimi binafsi nimeiombea na ninaiombea nchi yangu dhidi ya gonjwa hili hatari. Mwenyezi Mungu atukinge na haya maradhi.
 
Kwa tunaoamini uwepo wa Mungu. Tunaamini amesikia maombi yetu na ametuokoa. Mimi binafsi nimeiombea na ninaiombea nchi yangu dhidi ya gonjwa hili hatari. Mwenyezi Mungu atukinge na haya maradhi.
Basi tunawashukuru sana
 
Mungu ibarki Tanzania , bariki watoa huduma za afya kwa binadam kwa kazi waliyo ifanya mpaka sasa kuhusu janga la covid-19..kwani watumishi wa afya wamepita kwenye mpito wa kuhatarisha maisha yao lakini hawajaopopa, magufuli juuuuuu....wapinzani tukutane2050
 
Kuna wakati mtu unajiuliza hivi tatizo nini? Mkuu anasema Corona imekwisha na wananchi wawe huru , mpaka mzee wa watu SPIKA kaambiwa kwenye kiti yupo peke lakini anakazana kuvaa Barakoa , baada ya kuambiwa hivyo kaacha kuvaa , ikiwa ishara ya kusema kuwa corona imekwisha nchini Tanzania tu , lakini nchi za jirani maambukizi yanaongezeka kila kukicha...
Mkuu pengine imeonekana kwamba hofu ya corona ndio lilikuwa tatizo kubwa kuliko hiyo corona yenyewe, kwa sababu kinyume na hivyo sioni ni vp Magufuli aseme corona imepungua sana au imeisha kabisa na hadi kutotaka watu kuvaa barakoa huku akijua kuwa kwa kufanya hivyo kutafanya maambukizi yazidi na vifo vitamuumbua tu maana anaficha maradhi.

Hata Marekani tunaona watu wanaruhusiwa kuandama wakati hiyo nchi ndio hadi sasa inaongoza kwa maambukizi na ndiyo yenye vifo vingi vya corona.
 
Wadau sio siri mi hadi sasa sielewi,hivi hii corona imekuwaje hapa bongo???!!..kwa jinsi serikali ilivyochukua hatua kupambana na hii corona,halafu nikiangalia masimulizi ya watu wanaishi huko mamtoni,ulaya..nikiangalia worldmeter huko idadi ya vifo toka mwezi wa 9 mwaka jana, hadi leo hii ,nikisikia habari za lockdown, napagawa zaidi nikiangalia idadi ya walioathirika na hiki kirusi hapa Africa..
Ni kweli mkuu, kwa sababu kama Huko Marekani ambako vifo ni vingi ila tunaambiwa kama si lockdown pengine hali ingekuwa mbaya zaidi. Sasa kwa akili ya kawaida nchi kama Tanzania hadi sasa ingetakiwa tuone hali kuwa mbaya zaidi kwa jinsi serikali inavyolichukulia hili suala.
 
Ni kaswali tu, viongozi wote hasa wateuliwa na wabunge hawavai kabisa barakoa. Iwe kwenye mazishi, mikusanyiko mbalimbali nk hutawaona wamevaa barakoa.

Au watakuwa washapigwa chanjo kisirisiri wanatupoteza maboya wenzao?

Leaders lead by examples. Wananchi wengi wenye low reasoning capacity wanasubiri leaders wavae magwanda ndo nao watimbe! Please leaders tunaangamizana!

NB: Mie navaa barakoa, wewe je?
 
Back
Top Bottom