Hii ni JF unaruhusiwa kutumia lugha Kali ila sio kutusi wazazi wa MTU
Tu najua ninyi ni wasukuma mliochoka kuchunga kipindi hiki mnataka mrudi chuo mkarelax but sisi wazazi tunaojali wanetu tu najua bado risk mtoto kwenda chuo kwa hali iliyopo saivi
Najua hujui ila mtaka radhi my sweet mam kwa kumuita mpumbavu ilihali alishaacha upumbavu na anamiliki PhD yake
Sanitizer ni pombe sasa wewe unabisha nn?Hahaha eti "pombe sanitizer"...wee jamaa una mzaha
Covid19 ni janga mkuu,nakumbka italy ilianza na visa vi2 tu vya corona lakini kwa sasa ni shida,tuna watu Tz wanakinga dhaifu wakiupata ni shida.Wakuu kufuatia hatua zilizochukuliwa na serikali yetu kupambana na covid 19 hakika kama ingekuwa ni janga basi Watanzania tungekwisha tupukutike!
Shughuli zingine zote zinaendelea, shule na vyuo tu ndio vimesimama, sioni ulazima wa vyuo na shule kufungwa kwa kuepuka corona kama janga kwa nchi yetu.
Corona ipo kwaajili ya wazungu huko Ulaya, ni zamu yao sasa wacha iwanyooshe. Huku Africa tunapambana na majanga yetu ya maralia, njaa, ebola na mengine mengi. Wazungu wanataka kulazimisha janga lao liwe la dunia nzima. Haiwezekani.
PM Majaliwa tunaomba usiongeze muda wa kufunga shule na vyuo, watoto warudi kusoma kuanzia tarehe 17 Aprili.
Akikujibu nitag.Familia yako wako wangapi wanaumwa hiyo corona?
Hakuna na haitotokea na kama ikitokea itakuwa kwako.Naomba huu uzi usiufute, baada ya mwezi kuanzia leo turejee hizi PUMBA zako.
Sent using Jamii Forums mobile app
Utakuwa huijui vizuri nchi yako Mkuu, Tanzania ni kubwa sanaSidhani kama kuna sehemu hakuna network, HALOTEL ndo mpango mzima hadi huko nanjilinji. Kuhusu simu, wananzo kama hana smart, sidhani kama kuna kijiji hakina mtu mwenye smart, watz ni wazalendo tunaazimana
Yaani hata manyeusi wenzao hawawatibu? Kuwa serious mkuu.Nina jamaa yangu pale Minneapolis Minnesota ni daktari na juzi juzi alikuwa ananiambia anataka aende The Empire state kuchukua zile dollsr 10,000 kwa wiki zilizotangazwa na meya wa Empire stateBlack kule wanatelekezwa hawapatiwi tiba sahihi ndiyo maana wanakufa wengi kuliko weupe!
Bado mfumo wa elimu THEORY ORIENTED hausaidii sanaWatanzania tusilizike na matamko ya wanasiasa kwamba serikali inatoa elimu bure,,tujiulize je!elimu bure hii inayohubiliwa na hawa viongozi inamuandaa mtoto kuwa nani?kwa maarifa yepi? Inamfanya awe mshindani duniani au Watchers ya kile kinachoendelea duniani? Watanzania wanasiasa sio rafiki zetu huuata kidogo hawapo kwa ajili ya shida zetu hebu angalia yanayoendelea toka awamu hii ilipoingia madarakani muda wote wanahangaikia uchaguzi ujao,akina polepole wanabema maburungutu ya fedha kwenda kulipa faini ya watuhumiwa wa mauaji yakubumba wakati wanafunzi hawana vitabu,hawana madawati,shule hazina maabara za kutosha,walimu wanadai madeni lukuki na wanajibiwa serikali haina fedha jifikirie mtoto wako masikini atafundishwa ipasavyo na mwalimu mwenye kinyongo? Rudi kwenye miundombinu ya shule kuna baadhi ya shule ni magofu hayatamaniki hata kidogo,madarasa yamechakaa haswa lakini watu wanabeba pesa kwenda kulipia faini za kijinga kabisa huku wakiacha mambo ya msingi yakijiendesha bila kusimamiwa ipasavyo. Tanzania nchi yangu
Watoe taarifa mapema ili wazazi waanze kuandaa na wengine kukopa naulisidhani kuna mzazi atafurahia kurudisha shule wanae sasa, it is too soon!! at least tuone kwanza data zetu for a month more, na hasa hawa wagonjwa wanaotibiwa sasa wakipona itakuwa safi sana. turudi zero with extremely tight entry to Tanzania, mimi bado siamini sana kama tumedhibiti ipasavyo uingiaji wa waleta Coronavirus mipakani na Airport hadi nisikie JWTZ wamechukua kazi hiyo, but wenyewe wakiamua shule zifunguliwe tutawapeleka shingo upande!
Sidhani kama kuna sehemu hakuna network, HALOTEL ndo mpango mzima hadi huko nanjilinji. Kuhusu simu, wananzo kama hana smart, sidhani kama kuna kijiji hakina mtu mwenye smart, watz ni wazalendo tunaazimana
Nashauri shule na vyuo viendelee kufungwa lakini kwa upande wa vyuo vikuu, wakufunzi waanze kufundisha kwa njia ya mtandao.
Hii inawezekana hasa kwa masuala ya theory, na practical zinaweza kufanyika siku wakirejea vyuoni. Tutumie mitandao kuwafundisha kwa vile wapo majumbani.
Kwa kuanzia, kuna wawakilishi wa wanafunzi (CRs) na viongozi wa wanafunzi vyuoni, hawa wanaweza kutumiwa notes na wakufunzi kwa mtindo wa SLIDES na VIDEOS na kusambaza kwa wenzao na hivyo muhula wa masomo kuendelea kama kawaida.
Kwa wale wenye mikopo (BOOM) wanaweza kupewa nusu kwa mfano sh.250,000/= ili zingine wapewe wakirudi vyuo baada ya kusaini.
Nimeshuhudia vyuoni baadhi ya wanafunzi hawahudhurii darasani ila wanachukua slides na kujisomea na wamekuwa wakifaulu hata kuzidi wale wanaohudhuria.
Vyuo vitakapofunguliwa, wakufunzi wanaweza ku-HIGHLIGHT kile walichofundisha na baadae kutoa TEST ONE.
Ili kiepusha msongamano, usumbufu katika vituo vya mabasi, na kukosa usafiri, siku shule zikifunguliwa, wapishane kwa wiki moja. Kwa mfano, wanaweza kutangulia wa shule za msingi na sekondari na baada ya wiki moja wafuatie wa vyuo vya kati na vyuo vikuu.
Wanafunzi wa vyuo vikuu wana viherehere hasa wakati wa uchaguzi, hivyo si vyema uchaguzi ukawakuta wakiwa vyuoni.
Sisi tunaweza siasa za kukomoana tu basi mengine sio kipaumbele chetu kabisa,,kuendesha nchi unahitaji mikakati thabiti sio longolongo za akina Polepole and the likehivi hata mitandao ya kufundishia tunayo?
hizo mb za kuunga unga za makampuni ya simu utaweza kuona lecture ya saa nzima?
Hatuna miundombinu ya kufanya hayo. Sisi mitandao yetu ni ya kutongozana na kuandika siasa na Clips ndogo ndogo za dakika tano.
kufundisha online kunahitaji internet ya nguvu. TTCL wameshindwa kazi ya kujenga mtandao wenye tija kwa wananchi wote.