#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Ingependeza zaid na level seat zingatiwa,
Pia Itazidi kujenga tabia ta kistaarabu unapokohoa au kupiga chafya kijikinga kwa ajili ya wenzako.
Ipunguze tabia pia ya wale wanopenda kujichokonoa ma pua hovyo hovyo..
Ipunguze pia tabia ya kusalimiana kwa kushikana viganja, zipo njia nyingi tu, At least nyuma ya kiganja basi.
 
Ingependeza zaid na level seat zingatiwa,
Pia Itazidi kujenga tabia ta kistaarabu unapokohoa au kupiga chafya kijikinga kwa ajili ya wenzako.
Ipunguze tabia pia ya wale wanopenda kujichokonoa ma pua hovyo hovyo..
Ipunguze pia tabia ya kusalimiana kwa kushikana viganja, zipo njia nyingi tu, At least nyuma ya kiganja basi.
Nina mashaka wale wanaoiita sahani tizer kama wanaelewa matumizi yake. Hili la kujifokonoa pua Waziri Ummy alitolee maelekezo vizuri.
 
Kusafiri nchi za watu itakuwa ngumu sana.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli mkuu,tutageuzwa geuzwa kupimwa balaa,karantini za kufa mtu. Kwa mfano kama una semina nchi flani lazima ofisi ipige mahesabu ya siku kumi na nne karantini kabla ya siku yenyewe. Wazungu wameshapata sababu ya kuzuia illegal migrants pia
 
Wakikusikia na kutekeleza mshukukuru Mungu.
Yule raisi wa jiji anaweza kuwakusanya tena RAIA wake stendi mojawapo na kuwaambia wapige Nazi.
Bora ukose mali, upate akili.

Hahahhaha,
 
Moja ya mabadiliko makubwa yatakayo baki hata baada ya corona kupunguza mashambulizi ni tabia ya kunawa mikono. Usishangae kukuta kila seat ya basi la luxury kuwa na chupa ya sanitizer. Hata kwenye ndege sanitizer kutolewa kwa wasafiri.

Kiwango cha malipo ya kadi ya benki bila kuweka nywila kuongezeka. Malipo ya contact less yameonekana kuwa salama zaidi katika maambukizi.
Ukimwi nao ulituletea condom ambayo imepunguza ladha
 
Alivyojulikana yule mmoja haraka sana

Tungefunga mipaka

Tungezuia mikusanyiko

Tungefanya mass checkup kwa wananchi wote na kutenga maeneo maalum ya kutoa huduma

Ila neno ninge/tunge huja mwishoni
Saivi acheni tu tuisome namba kakorona hakakuletwa na serikali ila maafa watachangia
 
Mkae mkijua Corona haito isha tu kwa kusema watu wajikinge na maambukiz Ila ipatikane CHANJO bila ivyo hamna mtu atae weza kuimaliza Ila itatumaliza cc alafu sio lazima twende nje na ikitokea ivyo unavyo sema kwamba watatutenga Basi ndio itakua afadhal ya muafrica kujikwamua ki fikra na kujitegemea yeye Kama yeye na kuona kua bila mzungu maisha yanaenda japo itachukua muda Ila Nina uhakika kizaz kimoja kikiisha au viwil waafrica tutakua tayar tumesha jikwamua katika mfumo tegemez wa mzungu Kwan Sasa ivi wanao ikost Africa na mtu mweus ni wale ambao wanaona maisha bila mzungu haiwezekan au bila kwenda ulaya hujaish

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri kwa serikali yetu. Msikufunga sehemu nyingi kwa sasa kwa muda mfupi 30-45 inawezekana huu ugonjwa ukalamisha mlivyofunga sasa kuendelea kwa miezi sita maana kesi hazitapungua badala yake zitakuwa zinaongezeka kila siku. Kufunga sehemu moja ya uchumi halafu watu waambukizane sehemu ambazo hazileti chochote kwenye uchumi kama makanisani au misikitini ni sawasawa na kubeba maji kwenye gunia.

Kupunguza pigo la uchumi ni bora ufunge sehemu zote kasoro ambazo si muhimu kwa siku 45 halafu mkifungua mnakuwa hamna hali hii ya wagojwa kuongezeka. watu wakikaa ndani kwa siku 14 sio wote lakini wagojwa wengi watapona bila hata kwenda hospitalini maana hivi vidudu vinaondoka baada ya muda. Hivyo wanaoumwa wanakuwa hawawezi kuambukiza hata kama serikali haiwajui. Bila hivyo tutafunga kwa miezi sita au zaidi na tutakuwa na pigo zaidi. Acheni siasa fuatilieni wengine wanavyofanya

Inabidi kwa sasa tuongeze kuchukua vipimo na sio kwa wale wanaoumwa tu.
 
Heri ya pasaka kwa wakristo wote na Watanzania wote kwa ujumla.Nianze kwa kufanya mrejeo wa tamko la wizara ya Afya kupitia waziri wetu Mh.Ummy Mwalimu ya kuwa tujiandae na maambukizi ya ndani kwa ndani,ikiwa kama ndiyo hivyo.Mimi kama mtanzania nashauri yafuatayo ili kuweza kukabiliana na maambukizi hayo
1.Ikiwa kama serikali yetu tayari au tuna vifaa vya kutosha,basi visambazwe kwenye hospital zote,maabara na vituo vyote vya afya serikali na vya binafsi pia kwa idadi maalumu.
2.Mgonjwa yeyote atakayekuwa ameenda sehemu zote hizo kupata huduma za kimatibabu na akiwa na kifua,mafua au kama haelewi anachoumwa basi apimwe Corona tu.
3.Kama wagonjwa hao watapimwa na watakugundulika wana maambukizi au wana Corona basi watengwe kuanzia siku hiyo baada ya kugundulika na kupelekwa kwenye wodi mojawapo katika hospitali katika mkoa husika ambayo itatengwa kwa ajili ya wagonjwa wa Corona.

Nini faida ya hayo yote kwa mtazamo wangu
1.Tutapata kuwajua wagonjwa ambao wana corona na wapo mtaani lakini hawajijui.
2.Tutaweza kudhibiti maambukizi ya ndani kwa ndani kwani wagonjwa waliopatikana watakuwa wameshatengwa sehemu maalumu.
Mimi nimewaza hivyo kama mtanzania mwenzenu.
mazagaone@gmail.com
Mhitimu UDOM,
Job Seeker,
Mwanasayansi.
Umesahau.
Ongeza Waathirika watajwe
wanatokea maeneo gani viz mitaa vijiji nk .
Hii itasaidia watukuchukua tahadhali zaidi hasa kwenye maeneo hayo kwa kuepuka mikusanyiko km misiba nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom