#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Naunga mkono hoja. Tusipochukua tahadhari ya kutosha, hii Corona itatuyumbisha sana. Natambua fika walevi wa dini na wale wa vinywaji moto, hawataelewa kabisa somo!
 
Serekal yetu inatakiwa ikubal ushaur wa wadau juu ya ugonjwa huu hatari wa Corona kwa Lock down Ila itafute washaur na kila ushaur upimwe upi unafaa na upi hufai.

Tanzania tunaweza kukaa lock down ya mwezu mmoja tu na tukawa tayar tumesha maliza walio ambukizwa wote SABABU bado mapema na ugonjwa hauja sambaa kiivyo

Tanzania tunaweza kuweka Lock down kwa ntindo wa kutenga nwez mmoja wa Vita dhid ya Corona mfano serekal ikitenga mwezi mmoja ambao kila mfanyakazi wa serekal na taasisi kubwa kubwa zinazo julikana zisitie mshaara wa kiwango Cha awal pia hii iwe kwa wabunge na rais pia hata mawazir wote wasilipwe mshaara wao wa awal na badala yake serekal itoe kwa kila raia shiling laki 2 naiman itatosha na kwa raia wetu wa Tanzania hata katika kununua bidhaa kwa raia sidhan Kama Kuna familia itashindwa ku balance shiling laki mbil kwa matumizi ya mwezi mmoja

Pia SEREKAL itabidi ihakikishe umeme ndani ya mwezi huo ni bure pia maji yapatikane kwa wanao tumia dawasko vingamuzi ndani ya mwez huo viwe Free vyote pia SEREKAL iweke usirias katka mipaka YETU naiman kwa njia hii watu wataweza kukaa ndani bila lawama yoyote na pia madocter watakao kua wanaudumia wagonjwa hospital wasiruhusiwe kurudi ma kwao watafutiwe eneo naiman bado hatuja chelewa watu walio ajiriwa wasipewe mishahara Yao yote Kama wanapokea laki 4 na kuendelea mpaka kwa rais asitoke mishahara na mafisad apa itabidi wawe wawe na HURUMA waache kupiga hela Mana inaweza ikawa Kama fulsa kwao

Nimetoa mawazo ya Lock down sababu bado mapema na ndani ya mwezi mmoja unatosha kabisa kujua Nan na Nan wanaumwa na kuwatenga

Pil kila mwenye mawazo inabid atoe na ajitaid asiingize siasa sababu siasa zitafanya mawazo yake ambayo yanaweza kutusaidia yakaonekana ni upuuzi

Serekal tufikirie ni jins Gan mtu ambae ameathirika hawezi kukutana na mzima na Kama mtafanya ivi askar wawe Makin Sana katika kuakikisha watu hawatok nje
Kabisa Yani Lock down ambayo hata jiran haruusiw kuongea na jiran yake pili wiki moja kabla ya Lock down lazima TV na redio zitumike kuelimisha jamii kwamba tunaenda kupambana Vita ya mwezi mmoja dhid ya korona na hata wasanii ikibid watumike kufikisha ujumbe vijijn na mijin pia zitumike hata propaganda ili kuziwia watu wasitoke nje

Mnaweza hata kutangaza askar wanaua watu wanao kaid kukaa ndani au kudanganya kua Corona kila siku inaua mamia ya watu ili watu waingiwe na woga pia ikibid hata mabom na risas viwe vinapigwa usiku na mchana ili kutisha watu wasitoke nje naiman tukitanya iv na watu wakatii kukaa ndani Nina uhakika ndani ya mwezi mmoja majibu mazuri tutakua nayo

Asanteni pia na wewe unaweza kuchangia unacho fikiria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni serikali ianzishe vituo vya kupima corona kila mtu akapime Afya yake kuangalia kaukwaa ama vipi. Kwa sababu hii staili ya kusubiri mtu aumwe ndo aende hospitali ndo wampime ndo wakute ana corona itatumaliza.

zile nchi ambazo tunaona maambukizi yapo juu ni kwamba wanawapima wananchi wao hususani kwenye miji ambayo imeonekana kuathirika zaidi.

Kwa sababu tulishafanya uzembe tukaruhusu wageni wenye corona waingie nchini wakati ugonjwa umepamba moto na baada ya wageni kupungua ndo mkafunga anga wekeni vituo maalum watu wakapime.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa vile tumeamua hatuwezi kuweka nchi yetu kwenye "lockdown" kutokana na watu wengi kutegemea kuendesha maisha yao kwa kufanya kazi zinazo walazimisha watoke majumbani, ni vizuri serikali ikaweka sheria ambazo zinaweza kusaidia kupunguza maambukizi ya corona.

Sheria moja ambayo napendekeza na nchi ambazo zimeshambuliwa vikali na janga hili wanaanza kutumia, ni watu wote wakitoka nje ya nyumba zao wavae masks/barakoa. Mtu ambae hatovaa mask/barakoa alipishwe faini.

Masks/barakoa sio lazima hiwe ya kutupa kila siku kwani inaweza kuleta gharama kubwa kwa wananchi; mtu anaweza kushonesha na akafua jioni. Ikiwezekana serikali igawe masks/barakoa za vitambaa bure kwa wananchi hili watu waendelee na miangaiko ya kila siku kama kawaida.

Wale ambao watapata dalili za corona yani homa kali, kukohoa, na kushindwa kupumua watabaki majumbani au kwenda hospitali kama watazidiwa zaidi.

Mwenyezi Mungu aendelee kutulinda na janga hili, lakini ni muhimu na sisi tuchukue hatua za kujikinga.
 
Je, zipo za kutosha, na bei ni ya kumudu kwa namna zivaliwavyo- kubadilisha kila baada ya masaa manne? Au zitakuwapo za kufuliwa?
 
Je, zipo za kutosha, na bei ni ya kumudu kwa namna zivaliwavyo- kubadilisha kila baada ya masaa manne?
Huitaji kitambaa kikubwa kutengeza mask. Unatengeza mask japo tatu hili ubadilishe mara mbili kwa siku na kama huna uwezo moja inatosha, ni bora kuliko kukosa kabisa. Hizo nchi za nje wanatumia mask moja siku nzima na hapo ni hospitali kwa vile kuna upungufu wa masks.

Kwa mtu wa kawaida ambae anaenda kazini haiwezi kuchafuka kihasi cha kuitaji kubadilisha kila baada ya masaa manne.
 
Tuvae mask na gloves, hapo sawa, mask pekee haisaidii kama bado tukifika dukani tunashika meza ya duka, tunafungua milango ya maofisi nk
 
Ukiambiwa uvae mask muda wote haina maana uavhe kunawa,kutumia sanitizer na njia nyingine zilizoshauriwa.
Sawa mimi nimenawa, je wenzangu wote watakaopanda bodaboda itakayonipeleka kazini nao watakuwa wamenawa? Vp wakiacha korona kwenye kiti cha abiria baada ya kushika bomba wakati wa safari?
 
Tuvae mask na gloves, hapo sawa, mask pekee haisaidii kama bado tukifika dukani tunashika meza ya duka, tunafungua milango ya maofisi nk
Huitaji kuvaa gloves, mikono tutaendelea kuosha au kutumia vitakasa mikono. Maofisi na wafanya biashara waendelee kuweka maji na sabuni pamoja na vitaka mikono.

Mikono unawza kuosha na sabuni au kujizuia usishike pua, mdomo au macho mpaka utakapo pata nafasi kunawa, lakini kuvuta hewa yenye vijidudu ni ngumu kujizuia kama hauna mask. Na hapo ndio umuhimu wa masks unazidi umuhimu wa gloves.
 
Dunia imejaa watu.
Acha tupungue
NA dunia ipumzike NA vurugu za wanaadamu.

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
IMG_20200411_044022.jpg
 
Huitaji kuvaa gloves, mikono tutaendelea kuosha au kutumia vitakasa mikono. Maofisi na wafanya biashara waendelee kuweka maji na sabuni pamoja na vitaka mikono.

Mikono unawza kuosha na sabuni au kujizuia usishike pua, mdomo au macho mpaka utakapo pata nafasi kunawa, lakini kuvuta hewa yenye vijidudu ni ngumu kujizuia kama hauna mask. Na hapo ndio umuhimu wa masks unazidi umuhimu wa gloves.
Kumbuka wewe ni banadamu sio robot, watu wanapuuzia kuvaa kondom, nini kushika pua. Mask tuvae na gloves tuvae
 
Back
Top Bottom