Kwanza nitoe pongezi kwa serikali ya JMT kwa juhudi na hatua wanazochukua kwenye kukabiliana na ugonjwa huu wa Covid-19.
Mchango wangu kwa leo utaangazia sekta ya elimu.
Kutokana na kuwa wanafunzi walirudishwa nyumbani ikiwa ni hatua ya kuzuia au kupunguza maambukiki ya ugonjwa huu. Na inavyoonesha kuwa kasi ya maambukizi inazidi kukua.
Sasa je tutahairisha masomo mpaka lini? Na je ugonjwa huu usipopata ufumbuzi mwaka huu ina maana utaratibu wa elimu utasimama mwaka mzima?
Kwa kuangalia inaweza ikawa ngumu kwa wanafunzi kurudi shule kwa sababu alipopatikana mgonjwa wa kwanza shule na vyuo vyote vilifungwa, lakini sasa tunawagonjwa zaidi ya 80 hivyo itakuwa ni ngumu sana kuanza masomo
Lakini serikali ikizingatia mambo flani flani katika uendeshaji wa mfumo wa elimu na mambo yanaweza kuwa 'under control' na wanafunzi wakarudi kuendelea na elimu bila kuleta taharuki zaidi.
Mambo ya kuzingatia ni:-
ELIMU, hapa kwenye elimu serikali na sekta binafsi pamoja na vyombo vya habari wamejitahidi sana,lakini naona bado haitoshi kwa kuwa watu bado hawajajua vyema matumizi ya vifaa tiba na kujikinga zaidi.
Lakini kwa kuwa ninaangazia kwenye suala la elimu basi walimu wakuu wote na wasaidizi wao wapewe semina ya kukabiliana na ugonjwa huo na matumizi sahihi ya vifaa tiba ili na wao wakawape wanafunzi elimu hiyo ili waweze kujihadhari.
Hiyo itasaidia kupunguza maambukizi mfano darasani wanafunzi inabidi wakae wangapi?, kwenye dawati wakae wanafunzi wangapi? Muda wa mapumziko wanafuzi waweze kuangaliwa kwa ukaribu ili 'kumantain distance iliyoamriwa' muda wa kufanya kazi za shule uangalizi uwe mkubwa Nk
VIFAA, pia katika kukabiliana na ugonjwa huu serikali,sekta binafsi na wadau mbalimbali waweze kutoa msaada wa vifaa kwa mashule ili kuweza kusaidia na ugonjwa huo.
Vifaa hivyo ni kama barakoa, sabuni, ndoo za kunawia na maji safi.
WATAALAMU, Pia ingependeza kwenye kila shule wangekuwepo wataalamu wa afya angalau hata wawili, wakiume na wa kike ili kuweza kutoa huduma za afya na elimu kipindi shule au vipindi vinaendelea.
USAFIRI, hii ni mahsusi hasa hapa Dar es alaam ambapo usafiri ni wa shida hivyo utekelezaji wake utakuwa mgumu.
Kutokana na kuwa sasa daladala wanataka 'level seats' hivyo wanafunzi waliozoea kusimama kulingana na kiwango cha hela yao 200/= itawawia ugumu kupata usafiri.
Hivyo wazazi wanaweza wakawaongezea hela ya nauli ili wawe wanakaa kwenye siti kwa kulipa 400/=
Au serikali itoe magari kwenye kila wilaya jijini Dar ambayo yatatoa huduma za usafiri kwa kila wilaya na wanafunzi wachangie kiasi kilichozoeleka cha 200/= ili kutoleta usumbufu na uhaba wa usafiri.
Naamini kwa kufanya hivi tutaweza kuendelea na masomo hata kwa ngazi ya chuo na itapunguza athari kwenye elimu na uchumi wetu kwa ujumla.