#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Hatima yako haiwezi kuamuliwa na serikali katika kipindi hiki.
Tujifunze kutotoa lawama maana hazitosaidia angali unajua madhaifu ya sereikali yako!
Maisha yako! Familia yako! Uchumi wako! Ww ndo wakuamua au uamuliwe na mwingine abaki kutoa lawama!
Xre! Sijajua ww kama ni mwanasiasa maana ndo zenu kuchafuana!
Mm huko siku mkuu
 
Kirusi cha corona kinasambaa kwa njia ya upumuaji. Wengi tunafahamu msongamano ulioko magerezani. Kama msamaha kwa wafungwa ili kuzuia maambukizi magerezani hauwezekani basi waboreshewe mlo.

Corona haina tiba Bali ni kinga ya mwili. Milo iliyokamilika husaidia kuimarisha kinga ya mwili. Basi wapewe matunda mboga na karanga kusaidia afya zao.
 
Useme , wapate matunda kwa wingi ila karanga zinaleta nyege

Pia serikali ingetoa dhamana kwenye kesi za mauaji hata kwa masharti magumu, maana magerezani watu 60% nikesi za mauaji tena ni mahabusu.
 
Kirusi cha corona kinasambaa kwa njia ya upumuaji. Wengi tunafahamu msongamano ulioko magerezani. Kama msamaha kwa wafungwa ili kuzuia maambukizi magerezani hauwezekani basi waboreshewe mlo.

corona haina tiba Bali ni kinga ya mwili. Milo iliyokamilika husaidia kuimarisha kinga ya mwili. Basi wapewe matunda mboga na karanga kusaidia afya zao.
Na karanga tena?
 
Vyakula vyenye madini ya chuma ni muhimu kwa Wafungwa
 
Kwanza nitoe pongezi kwa serikali ya JMT kwa juhudi na hatua wanazochukua kwenye kukabiliana na ugonjwa huu wa Covid-19.

Mchango wangu kwa leo utaangazia sekta ya elimu.

Kutokana na kuwa wanafunzi walirudishwa nyumbani ikiwa ni hatua ya kuzuia au kupunguza maambukiki ya ugonjwa huu. Na inavyoonesha kuwa kasi ya maambukizi inazidi kukua.

Sasa je tutahairisha masomo mpaka lini? Na je ugonjwa huu usipopata ufumbuzi mwaka huu ina maana utaratibu wa elimu utasimama mwaka mzima?

Kwa kuangalia inaweza ikawa ngumu kwa wanafunzi kurudi shule kwa sababu alipopatikana mgonjwa wa kwanza shule na vyuo vyote vilifungwa, lakini sasa tunawagonjwa zaidi ya 80 hivyo itakuwa ni ngumu sana kuanza masomo

Lakini serikali ikizingatia mambo flani flani katika uendeshaji wa mfumo wa elimu na mambo yanaweza kuwa 'under control' na wanafunzi wakarudi kuendelea na elimu bila kuleta taharuki zaidi.

Mambo ya kuzingatia ni:-

ELIMU, hapa kwenye elimu serikali na sekta binafsi pamoja na vyombo vya habari wamejitahidi sana,lakini naona bado haitoshi kwa kuwa watu bado hawajajua vyema matumizi ya vifaa tiba na kujikinga zaidi.

Lakini kwa kuwa ninaangazia kwenye suala la elimu basi walimu wakuu wote na wasaidizi wao wapewe semina ya kukabiliana na ugonjwa huo na matumizi sahihi ya vifaa tiba ili na wao wakawape wanafunzi elimu hiyo ili waweze kujihadhari.

Hiyo itasaidia kupunguza maambukizi mfano darasani wanafunzi inabidi wakae wangapi?, kwenye dawati wakae wanafunzi wangapi? Muda wa mapumziko wanafuzi waweze kuangaliwa kwa ukaribu ili 'kumantain distance iliyoamriwa' muda wa kufanya kazi za shule uangalizi uwe mkubwa Nk

VIFAA, pia katika kukabiliana na ugonjwa huu serikali,sekta binafsi na wadau mbalimbali waweze kutoa msaada wa vifaa kwa mashule ili kuweza kusaidia na ugonjwa huo.

Vifaa hivyo ni kama barakoa, sabuni, ndoo za kunawia na maji safi.

WATAALAMU, Pia ingependeza kwenye kila shule wangekuwepo wataalamu wa afya angalau hata wawili, wakiume na wa kike ili kuweza kutoa huduma za afya na elimu kipindi shule au vipindi vinaendelea.

USAFIRI, hii ni mahsusi hasa hapa Dar es alaam ambapo usafiri ni wa shida hivyo utekelezaji wake utakuwa mgumu.
Kutokana na kuwa sasa daladala wanataka 'level seats' hivyo wanafunzi waliozoea kusimama kulingana na kiwango cha hela yao 200/= itawawia ugumu kupata usafiri.

Hivyo wazazi wanaweza wakawaongezea hela ya nauli ili wawe wanakaa kwenye siti kwa kulipa 400/=
Au serikali itoe magari kwenye kila wilaya jijini Dar ambayo yatatoa huduma za usafiri kwa kila wilaya na wanafunzi wachangie kiasi kilichozoeleka cha 200/= ili kutoleta usumbufu na uhaba wa usafiri.

Naamini kwa kufanya hivi tutaweza kuendelea na masomo hata kwa ngazi ya chuo na itapunguza athari kwenye elimu na uchumi wetu kwa ujumla.
 
1. Viongozi wetu wa Tanzania wamesita kufunga Ibada makanisani na misikitini hili hofu ya kutoungwa mkono na viongozi wa dini. mfano Mikusanyiko ya ibada za Kakobe, Gwajima, Mwamposa, ni janga kueneza maambukizi corona.

2. Kuchuka maamuzi ya ku-lockdown basi kutoka nje ya Dar es salam

Ukweli ni kwa kama kusingekuwa na uchaguzi mwaka huu, Serikali ingefanya hatua nyingi zaidi katika kupambana na corona. Ikiwepo partial lockdown mji kama Dar es Salaam. Kufunga (ku-ban) mikusanyiko yote bila kujali ni walazima au si lazima. Maana corona haijui mkusanyiko gani ni lazima au si lazima. Corona haijui ibada au maombi.

Kinachotakiwa watu wasali majumbani wao basi.
 
Sasa wakizembea Raia wakaanza kufa hovyo uchaguzi utakuwa na maana gani, siasa zisipofushe macho washindwe kuchukua hatua stahiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Awali ya yote, nina kila sababu ya kumshukuru MUNGU kwa uweza wake mpaka sasa tuwazima kabisa.

Pili, natoa pole kwa wale ndugu zetu wote ambayo wamepata maambukizi ya virusi vya corona.

Tatu, naomba kutoa pendekezo langu dhidi ya kuzuia kuenea kwa virus vya Corona.

Serikali inatakiwa wale watu wote ambao wanakutwa na maambukizi isiwe siri tena. Bali Serikali ichukue taarifa zao na picha then isambaze zote ili watu wakiona na wao weweze kwenda kupima haraka.

Lakini huu utaratibu wa kufuatilia watu pasi na uwazi naona kama sio afya kabisa dhidi ya kutokomeza maambukizi ya Covid-19.

Mficha maradhi kilio humuumbua. Sie kama Taifa tuje na utaratibu huu wa Uwazi kwa wagonjwa wote ili tuweze kushinda vita hii.

Kwahiyo, kuanzia sasa wale wote wenye maambukizi taarifa zao ziwe wazi pamoja na picha zao na zitumwe kwenye magroup, vyombo vya habari, social media ili pindi mtu anapomuona mtu ambaye walikuwa nae na yeye afanye haraka kwenda kupima au kujiweka carantini.

Alex Fredrick
Dar es salaam








Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habarini za muda huu wanyonge wenzangu ambao kila kukicha tunasema afadhali hata ya jana, ya leo na kesho inshalah.

Tumejiandaaje kupambana na corona - kifedha, kitahadhari, na kutoambukiza wengine pindi utakapopata hata kwa bahati mbaya? Hebu tupeane mbinu hasa za kifedha na chakula; wewe umejiandaaje?

Binafsi nina akiba kiduchu ya fedha ambayo siwezi kununulia hata mtungi wa gesi. Ikitoea lockdown i can't survive even for a week.

Tuendelee kuchukua tahadhari kama shirika la afya duniani linavyo sisitiza pamoja na wizara yetu ya afya.

Mungu Ibariki na uiokoe Tanzania.

Naomba kuwasilisha
 
Habari wana Bodi.
Kutokana na maambukizi na kusambaa kwa ugonjwa wa corona (COVID 19) tunamuomba Mhe Jaji Mkuu afunge mahakama zote kwa wiki 6, na tunamuomba Mkurugenzi wa CMA afunge ofisi zote za CMA Tanzania, na tunaomba mamlaka zifunge mabaraza yote (kodi, ardhi na nyumba na nk)

Aidha mashauri yote yaahirishwe.
 
Mkuu, pole sana. Same hapa tuna vipato vya kuunga unga sana.
 
Back
Top Bottom