Naunga mkono hoja, tena tusiishie huko bali mahabusu wote waachiwe, Wafungwa pia waachiwe kama Iran.

P
 
Naunga mkono hoja, tena tusiishie huko bali mahabusu wote waachiwe, Wafungwa pia waachiwe kama Iran.

P
Nimesoma ukichoandika kuhusu mahabusu na wafungwa nimeshtuka...
Kuna jamaa alitufanyia uhuni yuko ndani mwaka wa 3 huu, sasa unaposema aachiwe sikuelew wakati hajamaliza 2 yrs bado ili iwe mi 5, wakae hukohuko.

Vp wakina Ruge na wenzake waachiwe?
Wenye kesi za uhujumu uchumi nao vpi?

Kuna utata bado katika kuamua hilo.
 
Naunga mkono hoja, tena tusiishie huko bali mahabusu wote waachiwe, Wafungwa pia waachiwe kama Iran.

P
Huo ushauri siyo mzuri kwani maambukizi yako huku URAIANI na siyo MAGEREZA. Cha kufanya ni kusitisha mahabusi au wafunge wengine toka URAIANI kupelekwa MAGEREZA kwani wanaweza peleka maambukizi huko.

Waliopo wabaki huko hdi vifungo vyao na wasiongezwe wengine labda kama wamepimwa na kuhakikisha hawana maambukizi
 
Mapendekezo ambayo Mr President anatakiwa kufanya .

1. Kwa kuwa ugonjwa umeshafika kwenye community stage transimission , Ningeshauri ile mikoa ambayo case chache zimepatikana.. kungeagizwa test kits za kutosha ili kubaini ukubwa wa Tatizo, Pili kila anayepatikana positive apelekwe kwenye vituo vya karantini.

2. Kwa kuwa ventilator zime prove low rates healing 50% compare to Hydroxychlotoquine + Zinc , pia ni very expensive .. ningeshauri Tanzania itowe order kwa ndugu zetu wa India Watutengenezee hydroxy Ch.. Zinc mseto mara moja na tutume ndege kwenda kuchukua ili zitumike kwa waliotest positive ..

3. Kiwanda cheti cha pharmaceutical kama kinaweza tengeneza mseto huo basi ni wakati mwafaka wa kufanya hivyo.

4. Kwa wagonjwa wenye mild symptoms na wenye ku prove self karantini waruhusiwe kijitibu Nyumbani.

5. Mabaa na Shughuli zote zamikusanyiko isiyo ya lazima zipigwe marufuku.

6 . Wauza masoko wapunguzwe au wauze kwa zamu.. Kuwepo Na mita 2 toka muuza soko mmmoja mpaka mwingine .

7. Serikali ingize barakoa za kutosha Na kutumia wanajeshi kugawa kwenye maeneo mbalimbali na baada ya week mbili iwe ni marufuku kutembea bila barakoa.

6. Mabasi ya mikoani.. yaagizwe kubeba mtu mmoja kwa siti ya watu wawili.. kupunguza kukaribiana kwa Abiria .

7 . Dalaldala kubeba abiria nusu ya idadi ili abiria wakae kwa nafasi Na zoezi hili lisimamiwe Na jeshi.

8 . Kusiwe Na total Lockdown , watu warujusiwe kufanya kazi , pale maeneo ya kazi yatakapokuwa ni hatarishi, basi eneo hilo tu ndio lifungwe.

9: Stendi za mabasi zisimamiwe Na Jeshi Na wale wapiga debe waondolewe wote kupunguza msongamano usio Na lazima .

10. Hospital maalaum za Korona zisifanye kazi y huduma zingine za kawaida ili kupunguza maambukizi.

11. Ibada ziendelee lakini waumini waingie kwa zamu na kuwepo kwa umbali wa mita 2 toka muhimini mmoja Na mwingine Na Usafi wa kutosha ufanyike kila baada ya Ibada moja kuisha kabla ya kuingia Nyingine.

12. Wanajeshi wapelekwe mtaani ili kuangalia maeneo ya kazi ambayo yataonekana kuwa hatarishi basi yafungwe .

13. Shughuli za kilimo na mifuko ziendelee kama kawaida Na wakulima waelimishwe namna ya kujikinga Na kuweka mita 2 toka mkulima mmoja mpaka mwingine.

14 . Wenye viwanda pia wao observe mita 2 toka mtu mpaka mtu Na uvaaji wa mask.

....
 
Embu toa mapendekezo matatu tuu katika hiyo orodha yako. By the way hivi Katibu mkuu wa Wizara ya Afya ni Daktari wa binadamu kwa taaluma yake? nikipata jibu nitauliza swali gumu
 
Mkuu naunga mkono hoja lakini umesahau Dar inabidi iwekwe kizuizini ili kuzuia ugonjwa kuenea mikoani binafsi hili jambo naona serikali inabidi walishughulikie ndio itakuwa njia rahisi ya kupambana na Corona sababu ugonjwa bado haujafika mikoani.

Hata China wameweza kupunguza kasi ya ueneaji wa ugonjwa kwa sababu mji wa Wuhan ambao ulikuwa ndio kiini cha ugonjwa ndani ya China uliwekwa kizuizini.
 

Kuweka Dar yote kwenye Karantini ni zoezi Gumu Na expensive ingawa linawezekana.. kupanga ni kuchagua .. lakini bado tunaweza kuweka Karantini maeneo kwa maeneo badala ya Dar yote .. pia kufanya mapendekezo niliyatoa ili kupunguza maambukizi
 
Embu toa mapendekezo matatu tuu katika hiyo orodha yako. By the way hivi Katibu mkuu wa Wizara ya Afya ni Daktari wa binadamu kwa taaluma yake? nikipata jibu nitauliza swali gumu

Sijui kuhusu Katibu mkuu lakini kuhusu mapendekezo unaweza kupunguza au kuongeza Lengo ni kupata solution yenye kupunguza maambukizi
 
Mawazo yako mengi mazuri, ila hili LA kutumia jeshi siungi mkono.

Jeshi letu Limefanya kazi nyingi nzuri Na kwa weredi , naamini hata hili watafanya kwa weredi bila kutumia mhemuko , nachelea kusema Jeshi letu la Polisi bado linahitaji msasa kabla ya kukabidhia kazi kama hii , mihemko na Rushwa bado ni Tatizo kwa Jeshi hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…