Tangu Corona iingie Tanzania imeau watu watatu tu na wagonjwa wapo 94 kwa Mujibu wa Bi. Ummy.
Juzi ajali imetokea Mkuranga, ajali ya Coaster wamekufa watu 20 na zaidi., sasa ajali moja inaondoa watu wengi kuliko wa Corona.

Daladala za Dar es salaam ambazo nying ni Eicher, Toyota Coaster na Rosa na Nissan Civilian,huwa na beba watu 28-Coaster na 26 -Civilian,lakini kwakuwa watu wa Dar ewapo vululu na viongozi yaani LART hawajali basi huwa wanatoa viti vyote vya katikati na kubaki ukumbi ambao watu husimama wengi kuliko waliokaa.

Baada ya Corona na watu kuambiwa wakae MSAMBWANDA/ LEVEL SEAT basi daladala wamerudisha hizo seat /viti lakini wameweka vigoda vya mbao ambapo mkaaji yaani abiria hana balance, hana pa kuegamia, na gari ikishika breki huwa wanaanguka, hii ni hatari na sheria hairuhusu lakini Makamanda wa polisis wamelala usingizi wa pono, mpaka ajali itokee, watu wafe ndio utaskia tamko linatoka.

IGP una watendaji vilaza na wasio penda kazi zao, wanasubiri watu wafe, narudia wanasubiri vifo maana gari ikipiga breki mtu anatoka na kioo cha mbele
 
Toka huo utaratibu umeanza, ni wangapi wamepata madhara?

Hivi kwa spidi za daladala hapa mjini ambazo sidhani kama hata 60km/hr wanafika, break inaweza kukutisha kweli?
Huo umepewa ni mfano, hivyo ongeza ya kwako. Sio break tu, bali hata kupewa pande na kuishia mtaroni.
 
Mabasi ya mikoani yanayokuja na kutoka,huoni kama ni hatari kusambaza.........??? Kwakifupi bado hatujachukua hatua yoyote zaidi ya maombi
 
Toka huo utaratibu umeanza, ni wangapi wamepata madhara?

Hivi kwa spidi za daladala hapa mjini ambazo sidhani kama hata 60km/hr wanafika, break inaweza kukutisha kweli?
Umewahi kujikwaa ukaanguka na kuvunjika mguu? ulikuwa spidi ngapi?
Nahisi utapia mlo upo sehemu nyingi za Tanzania.
Kwanini dereva akamatwe hajafunga mkanda kwakuwa ajali ikitokea ataumia ila abiria amekaa kwenye kigoda amabacho hakijashikizwa sehemu yeyote asilindwe?
 
Mabasi ya mikoani yanayokuja na kutoka,huoni kama ni hatari kusambaza.........??? Kwakifupi bado hatujachukua hatua yoyote zaidi ya maombi
Maombi bila hatua ni bure, na wanao tangaza maombi watubu otherwise ni kelele mbele za Mungu# Free Tito , bring back Saa nane
 

Mkuu nakubaliana na observations zako kwamba inaweza kutokea.

Swali langu ni, toka huo utaratibu umeanza, imeshatokea?
 
Unapotoa ushauri,, toa na way forward nini kifanyike..
 
Mkuu, Serikali lazima ilaumiwe maana inanafasi yake ktk haya mapambano, kwa upande wangu napambana vizuri, Sera, mwongozo na mikakati ya serikali Ni muhimu

House girl(dada wa kazi) Ni binadamu aheshimiwe, apumzike, apewe Uhuru wa kuabudu pia
 

Play your part. Sehemu kubwa tushauri Sisi. Serikali imetimiza wajibu Wake kiasi kikubwa. Tujilinde


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anza kuchukua hatua wewe mwenyewe na wanaokuzunguka..ukisubiri serikali ifanye kitu mwisho wa siku utajikuta karantini na bado utaendelea kuilaumu serikali kwa yaliyokupata.
 
Kwa kweli huku mtaani kwangu mimi ni bora mtu ujiweke lockdown mwenyewe,nikitoka nje naona watu km hawajui lolote kuhusu Corona!

Yaani Inatisha,Sijui km wanajua kinachoendelea kila siku wanachojua wao ni kuweka vile vindoo vya maji na sabuni tuuu yaani wameyaweka mpaka kwenye mabanda umiza halafu wanajazana kuangalia muvi sijui mpira,Hatari sana.
 
Mtaani kwangu mm watu wanajitahidi kuchukua tahadhari kiukweli.. wafanya biashara wana vifaa vya kunawia mikono na wameweka nje watu wanawe kabla ya kuingia.. baadhi yao wanavaa mask pia.. lakini pia mtaani kwangu hakuna kitu kinachosababisha mikusanyiko ya watu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mtaani kwangu hawana habari, wengi ukiwauliza kwanini hawachukui tahadhari nyingine muhimu mbali na kunawa tu wanajibu huu ugonjwa ni wa watu waliotoka nje ya nchi ama wenye ndugu waliotoka nje ya nchi 😟
 
Mtaa wangu kwa kweli naona watu wameelewa kiasi kikubwa mabanda ya video na vijiwe kwa sasa havina watu , ndoo na sabuni pia wameweka sijajua he wananawa Mara kwa Mara au ni pambo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…