Wanaiongelea tu na mambo mengine yanaendelea kama kawaida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Points nzuri sana.ijapo utekelezaji unahitaji analysis.mfano ukizuia mwingiliano na mikoani tutakufa njaa Dar.sababu chakula kinatoka mikoani.pia uchumi wa Dar uta colupse kwa sababu Dar kuna viwanda wateja wako mikoani.pia Dar kuna bandari.ijapo shughuli za bandari zinaweza hamishiwa Tanga au mtwara.

labda tuongeze point moja

15. wafanyakazi wote wa hospitali zote zinazotibu wagonjwa wa korona watafutiwe hostel maalumu.wasirudi mitaani.maana wanaweza kkuuwa wasambazaji wakuu wa korona

16.Serikali iweke kipaumbrle kuhakikisha watumishi hao wa afya wanapewa vifaa vya kutosha vya kujikinga pia mafunzo ya mara kwa mara yatolewe kwa watumishi wengi.jinsi ya kutumia hat hizo ventilators.ikitokea wakaugua kuwe kuna back up ya kutosha kuendeleza huduma

hii imekuwa changamoto hata kwa nchi zilizoendelea.

17.Watumishi wote wa afya wanaostaafu sasa waongozewe muda wa kustaafu.na wale watalaamu wa public health na mgonjwa ya milipuko walio staafu hivi karibuni wapewe mikataba warudi kazini.
 
Mapendekezo yako ni mazuri ila hapo kwa kutumia jeshi Nadhani umesahau ule usemi usemao "Heri ya shetani unayemjua kuliko malaika usiyemjua"

Ni kweli kwa sasa Polisi, na wateule wengi wa mikoa wameonyesha Double standard wazi wazi kiasi kwamba watu sasa wamewatilia Mashaka.

Mapendekezo yako nayaunga mkono kasoro pendekezo moja la kutumia jeshi.
 
Wazo zuri
 
Nianze kwa kutoa pole kwa Watanzania wenzangu juu ya taharuki hii ya Corona inayo tukabili

Mhe Waziri nimekuita Dada ya Corona kama rafiki yangu mmoja wa Kimasai anavyo shindwa kukuita Waziri wa Afya sasa anakuita Dada ya Corona labda kwa kuwa kaanza kukufatilia wakati huu wa Corona na hizo Updates za wagonjwa zinazo ongezeka bila kushuka toka uanze kutangaza

Naomba niseme wazi Mimi ni miongon mwa watu tunao liombea Taifa hili juu ya maswahibu yanayo tukumba hasa gonjwa hili la Corona

Lakini pia naomba nikubaliane na Serikali yangu juu ya njia inazo chukua kupambana na corona

Ila juhudi hizi hazitoshi kuweza kuleta matokeo kwan ni kama mzaha mzaha hivi ambapo matokeo yake tunaweza kutumbua Usaha

Tupongeze serikali kutuacha kufanya shughur zetu halali ili kujitafutia kipato kuliko tungewekana lockdown ingawa naamin kwa mizaha hii hii Lockdown inaweza kutokea

Katika kipindi hiki mhe, utapokea maoni mengi juu ya njia za kupunguza athari za Corona kwenye jamii yetu

Kila njia ina pande mbili katika kutatua tatizo hilo njia nyingi na ushauri unatolewa baada ya kuangalia wapi tumefeli sasa Dada ya korona naomba niseme na Mimi

Do it now ama tusubir hatma

Kwanza polisi waingie Ku-regulate social distance hasa kwenye mabaa na vyombo vya usafiri na maeneo mengine ya mikusanyiko kama masoko

Pili kuvaa barakoa iwe lazma kwa kila mtanzania ambae anaingia kwenye makusanyiko hii ni muhimu kwa kizingatia sasa hivi ni local transmition hivyo uvaaji wa barakoa kwa lazma inaweza kupunguza uenezwaji wa virusi

Mabasi yote yanayotoka na kuingia Dar na kwenda mikoani lazima yapuliziwe dawa kwani tunapoelekea ugonjwa utatoka majiji makubwa na kuja mikoani na pale getini ubungo kuwe na kibali kuonesha kuwa gari lilipuliziwa dawa na kuruhusiwa

Kujengwe maabara kubwa kanda mbili ambazo ni kanda ya ziwa, nyanda za juu kusin ili kupima sampuli kwa haraka

Kila kampuni wawe na vipima joto ili kuangalia joto la abiria wakiwa wanashuka kabla ya kwenda kujichanganya na familia zao

Mwisho kabisa kama itashindikana ipigwe marufuku ya muda bus za abiria zisiruhusiwe kuingia na kutoka dar kwa wiki mbili MTU akitaka kutoka lazma awe na kibali cha polisi kama kuna ulazima

Lakini pia kuwe na kauli moja ili kutoa maelekezo kuliko hivi sasa tunavyo taka kuanza Mara Mkuu wa mkoa huyu achape watu viboko bar, Mara huyu azuie bar mwisho saa tatu, Mara kuanzia kesho kwenye mkoa wangu wote tuvae barakoa Mara biashara zote ziwe take away

Naomba niombe kuanzia kesho basi kama kuna kamati zimeundwa mtuambie nini ni nini na maelekezo yote yatoke kwa nani

Kwa Dar kila kaya wawe na ndoo za kunawia Maji na vitakasa mikono ili watu wanawe kabla ya kujichanganya na familia

Njia zote za kupambana na corona ziwe za Kitaifa kuliko sasa tunavyo taka kwenda kila Mkuu wa Mkoa atengeneze njia zake ndio maana huyu kapiga bar marufuku Leo katengua

Niongeze tena tunaweza jikuta wenzetu wote Afrika mashariki wameweza kuzuia harafu sisi tukawa kitovu kwa Afrika mashariki

Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika
 
Mimi hata sijui maanake natoka saa 10 alfajiri narudi saa tano usiku.
 
Anza kuchukua hatua wewe mwenyewe na wanaokuzunguka..ukisubiri serikali ifanye kitu mwisho wa siku utajikuta karantini na bado utaendelea kuilaumu serikali kwa yaliyokupata.
Mkuu Ni sahihi kujilinda kwanza lakini zipo sababu zisizo epukika,
Mfano mfumo wa daladala zetu si rafiki kabisa, watu wamebuni seat mpya humo hivyo mlindikano km huo hauepukiki,

House girl(dada wa kazi) Ni binadamu aheshimiwe, apumzike, apewe Uhuru wa kuabudu pia
 
  • Uzi huu ni mrefu.
  • Ukichangia naomba ujikite Zaidi katika kutoa maoni yako lakini kukosoa kunaruhusiwa.
Binafsi nadhani maamuzi haya ynagechukuliwa mwezi mmoja uliopita pale waziri mkuu alipotangaza kuzifunga shule na vyuo, lakini haikua hivyo badala yake shule zilifungwa kisha hakukua na mpango mkakati madhubuti wa kukabiliana na COVID-19, Zaidi ya makatazo ya kuepuka mikusanyiko na kunawa mikono na maombi. Lakini hu sio muda wa kuendelea kulaumiana Zaidi ni wakati wa kupeana mawazo na kushauriana.

Pia bado naamin, athari za kiafya kama watakao fariki kutokana na virusi hivi bado watakua wachache kuliko watakao athirika kutokana na athari za kuepo ugojwa huu, haswa suala la uchumi na elimu. Hivyo ni lazima kuwe na mpango mkakati wa haswa kuhakikisha kua baada ya muda furani tuwe tumefikia jambo Fulani.

Any way, binafsi kama ningekua na mamlaka ningetuimia njia hii kutatua tatizo la hili |Ushauri wangu.

  • Kwanza ni lazima kila mmoja ( serikali na wananchi kwa ujumla) kuwa na fikra ya kutatua tatizo na si kutengeneza faida, waswahili husema hasara roho, pesa makaratasi na zinatafuwa, huu ni wakati wa serikali na wananchi kujua kua nchi iko kwenye vita kubwa sana na inapambana na adui wa ajabu asie onekana menye madhara lukuki ikiwemo kupoteza maisha na hali mbaya ya uchumi, amapo kama serikali ni lazima iwe tayari kutumia rasilimali zilizopo katika kunusuru taifa, rasilimali hizi kama fedha na watu na miundombinu
Nini cha kufanya?

  • Serikali inainishe maeneo ambayo yako hatarishi Zaidi katika maambukizi ya virusi vya Corona, naamini yako wazi. Maeneo mengi ya mjini yanamuingiliano mkuwa wa watu kutokana na shuhuli zao za kiuchumi.

  • Baada ya kuanisha maeneo hayo, viongozi wa mtaa na katika maeneo yalioainishwa wapite wachukue idadi ya watu wote katika mtaa husika wakizingatia mambo yafuatayo:-
    • Idadi ya watu katika nyumba husika (hili nimesikia limefanyika maeneo ya Dar sina uhakika.
    • Hali yao ya kiuchumi
    • Kuchukua mawasiliano wa watu wawili waliopo katika nyumba hiyo na kuacha mawasiliano ya viongozi wawili wa mtaa husika.( namba za simu zenye uhakika).

  • Baada ya hatua ya kuainiasha maeneo na kujua wakazi namba ya wakazi husika na hali zao za kimaisha, serikali ikishirikiana na wadau, waangize bidhaa muhimu kutoka nje( kwenye upungufu) pia kwa wakati huu serikali inunue au iongoze vifaa vya kupimia Virusi vya corona Viwepo kwa wingi Zaidi visambazwe kila wilaya. Kama nilivyosema huu ni wakati wa kutumia rasilimali tulizonazo katika kupamba na janga hili si wakati wa kuanza kuangalia faida.

  • Hatua ya nne ni serikali kugawa chakula kwa familia zilizo na uchumi duni ambao hawana uwezo wa kuishi kwa siku ishirini na moja wakiwa ndani. Hatua hii inahitaji unaminifu na uadilifu kwa viongozi wa serikali wanaokadiria hali za kiuchumi za wananchi na pia kwa wananchi ambao watakua wanaeleza uhalisia wa maisha yao ili wasiibebeshe serikali mzingo ambao wanauweza, wasiwakoseshe wale wenye uhitaji na wala wasionewe. Watu wanosihi kijijini wengi chakula wanacho, shida walionayo ni hela ya kusagia mahindi, hela ya sukari chunvi na mafuta ya taa.

  • Hatua ya tano serikali itangaze lockdown kwa siku ishirini na moja (21) . Hapa wananchi wakiwa tayari wana mahitaji muhimu hasa chakula. Katika kipindi hiki.
    • Serikali itumie vyombo vya usalama katika kuhakikisha watu wanafata utaratibu lakini wawe ni wenye kuelewa kuepuka maafa kama yaliotokea nchi nyingine.
    • Tangazo la kua lockdown liwe mapema na watu kufanya maandalizi ikiwa ni pamoja na wale watakao pewa msaada mapema
    • Katoka kipindi hiki cha wiki tatu, kodi za biashara, umeme na maji viwe free kwa ambao luku zao zitaisha basi wasizime, pia wakadirie matumizi ya maji ya wiki tatu wasihesabu katika bili ya maji.
    • Mawasiliano ya karibu ya viogozi wa serikali katika kujua kinachoondelea latika kila kaya, hasa kwa dharura ya wagonjwa na mama wajawazito kuweza kupatiwa uduma.
    • Wale wanotamulika kama homeless na watoto wa mitaani, watafutiwe sehemu ya kuhifadhiwa( nashauri kwenye walo moja la kambi ya jeshi mana watakua na adabu, au watakapo wekwa wasimamiwe na wanajeshi).
    • Mipaka ifungwe kabisa.

  • Wiki ya pili ya lockdown, yaani siku ya kumi na nne (14), serikali ichukue sampuli ya watu wawili au mmoja kutoka katika kila nyumba, nashauri awe yule anaetoka toka sana( mtafutaji) na yule mtu mzima Zaidi au ambao anaumwa. Lengo na madhumuni ni kua,
    • kwa kipindi cha wiki mbili kama kama mtu alikua na virusi basi atajulikana.
    • Lengo la kuchukua mtu mzima au yule mgojwa ni kua, mwenye virusi anaweza kua yuko na kinga madhubutu hivyo kwa mtu mzima itasaidia hugundulika mapema.
    • Kuchukua watu wawili au hata mmoja kila nyumba kutasaidia kupunguza utumiaji wa rasilimali katika upimaji. Mfano kama idadi ya watu katika kaya yenye nyumba 300 na watu 2000, then tunapima 300 au 600 (kama wakichukua kila nyumba wawili) badala ya watu 2000.
    • Baada ya kuchukua sampuli kutoka katika kila nyumba, kutegemea na siku watakazo tumia. Kasha nyumba zitakazo kutwa na maambukizi watawekwa katika ungalizi( kutotoka au kuwapeleka katika maeneo maalumu yaliotengwa ) na kui disinfect nyumba.
  • Baada ya kuchukua familia zilizokutwa positive, kutegemea na siku zilizotumika kupima na kupata majibu, na kufanya mapendekezo ya namba saba, the tunaweza kufungua shule na shughuli zikaendelea huku tukiendelea na tahadhali, suala la level seat likendelea, kunawa mikono na uvaaji wa barakoa.

  • Katika kipindi chote hicho , serikali isisite kufanya utafiti katika jamii mbalimbali kwa asili yao kwa jinsi walivyoweza kupambana na magonjwa ya mfumo wa hela ili kuangalia uwezekano wa tiba mbadala.
Haya ni mawazo yangu ya jinsi ninavyoona jinsi gani ya kuweza kupambana na suala hili.

Aman ya BWANA iwe nayi wote.
 
Corona itakuwa imekupanda kichwani! Kwa nini usijilock down wewe na familia yako? Nani kakukataza kufanya hivyo?
 
Unajuaje kama hajajilockdown?

Kutojilockdown kunakunyima haki ya kutoa maoni yako?

Kiongozi yupi wa serikali corona haijampanda kichwani??

Kwakweli ili uwe mshabiki wa serikali hii ya meko inakuhitaji kwanza uwe mnafiki mkubwa.
Corona itakuwa imekupanda kichwani! Kwa nini usijilock down wewe na familia yako? Nani kakukataza kufanya hivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi.. Akae kimya aendelee kufaidi joto la mkewe... Marekani wenyewe wenye pesa chungu mzima yamewashinda... Kuanzia J3 watu wanaanza kwenda makazini japo maambukizi yapo juu! Sembuse sie hoe hae ndio tutaweza?
 
Basi.. Akae kimya aendelee kufaidi joto la mkewe... Marekani wenyewe wenye pesa chungu mzima yamewashinda... Kuanzia J3 watu wanaanza kwenda makazini japo maambukizi yapo juu! Sembuse sie hoe hae ndio tutaweza?
Mawazo yaajabu kabisa haya. Yani unadhani sisi hatuwezi kufanikiwa katika jambo ambalo watu wa nje wameshindwa? Acha mawazo ya kitumwa. Huenda haya yalioandikwa hujasoma
 
Reactions: THT
Mawazo yaajabu kabisa haya. Yani unadhani sisi hatuwezi kufanikiwa katika jambo ambalo watu wa nje wameshindwa? Acha mawazo ya kitumwa. Huenda haya yalioandikwa hujasoma
Tangu uzaliwe umewahi kufanikisha lipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…