#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Raisi Magufuli, Wakati hauko upande wako yafuatayo ni mapendekezo ya Kizalendo kabisa natoa, kama nilivyotoa mwanzoni kabisa mwa janga hili lilipoanza, Nilipendekeza Tuzuie watu kutoka nje wasiingie nchini, kwa maana mipaka yote ya nchi ifungwe (isipokuwa kwa situation maalum za. mizigo kuingia na kutoka)

hatuna jinsi sasa ni muda wa maamuzi magumu.

Situation tuliyo nayo ni ngumu kuliko hata wakati wa vita ya Kagera, ni mgumu kuliko hata harakati za kudai uhuru, WAKATI HUU TULIO NAO NI TISHIO LA, UWEPO WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA WATU WAKE

1. Kama unaweza kuilisha dar, Arusha, Mwanza na Miji yetu mikubwa piga lockdown yote nyumba kwa nyumba, Kama huwezi basi Piga Lockdowndown miji hiyo kwa level ya kata, siyo nyumba kwa nyumba, aliyeko Mwenge asiende kinondoni, aliyeko Kinondoni asiende Posta, masoko ya chakula yawe wazi, Hospitali ziwe wazi, watu watoke mmoja mmoja kwa ajili ya essential goods. Hakikisha unaplan vizuri watu hawafi kwa njaa, Mtihani upo kwenye watu kula Hapa umiza kichwa sana

2. Kopa watumishi wa umma kwa muda wa miezi miwili, Kata mishahara Ya watumishi wa Umma wenye kipato cha milioni moja kwenda juu kata 50%, wenye kipato cha laki tano kuja chini kata 10%. Hizi pesa ziwe deni la ndani ambalo serikali itakuja kulipa siku moja. Hizi pesa zitumike kununulia Chakula na Kukigawa bure kwa wananchi.

5. Ndani ya mikoa, kwenye mikoa ambayo haijaathiriwa sana, Funga nchi kwa level ya wilaya, mtu asitoke wilaya moja kwenda wilaya myingine.

6. Funga nchi yote kwa level ya mkoa, Safari zote za mikoa zife

8. Chagua nyumba kadhaa kila kata za miji ya Dar, Arusha, Mwanza na ile ambayo inaonyesha dalili za kuwa hardly hit ziwe supply point (maghala) kwenye kata hizo

7. Rasilimali za Jeshi la wananchi kama vile magari ya kijeshi zitumike kusambaza bidhaa muhimu nchi nzima, kwenye masoko na kwenye supply point katika kila kata, na kila Mwenye usafiri wa gari katika kila kata awe identified ili awe supplier wa essential goods katika kata yake, awezeshwe kwa mafuta

9. Tumia mtandao ulionao, Matawi ya CCM, Viongozi wa nyumba kumikumi, Misikiti ya maeneo, Makanisa, Vituo vya polisi, Hapa pia uwe makini isije ikaonekana misaada inakuja kwa misingi ya udini, uchama n. k

9. Challenge kubwa ni wale watu wasio na makazi maalum, ambao hula magengeni, ambao hawajui kupika, ambao hawana nyenzo za kupika, Hapa inabidi uumize kichwa kwelikweli maana ukikosea hapa watu watavamia nyumba nyingine kupora chakula. Hapa unaweza kutumia shule za msingi na sekondari zilizofungwa kuwaweka hawa na kuwasaidia kwa chakula.

10. Tulipeleka vijana wetu JKT siyo wakapige kwata, bali kwenye wakati kama huu tuwaite on duty watekeleze duty kama za kusimamia order kwenye kipindi kama hiki, kwa hiyo hawa ambao ni reserve army waitwe wasaidie kuimplement lockdown hizo nilizopendekeza

Mzee Ulikosea kutofunga mipaka hapo awali kwa kuhofia uchumi(Kama alivyosema Polepole), Sasa Uliacha kuuanika, leo tunautwanga mbichi.
Wahenga hawakuwa Wajinga kusema heri kinga kuliko tiba!
aanze kukata mishahara ya wanajeshi sio hao wanyonge unaosema! hapo ndio ntamuelewa
akifanikisha hilo NITAGI
 
Ghala la NFRA Lina chakula kiasi gani ?

Maana Magufuli anaona ni BORA kuchota MILIONI 38 kwenda kutafuta sifa ya kumtoa MSIGWA Jela kuliko kuweka Akiba Ya Chakula NFRA.

Waliokuwa Wanaweka Alikuwa Anawaona Wajinga.
 
Suala LA mishahara hapana kwa kuwa katiba inaruhusu matumizi ya dharura toka kwenye mfuko Mkuu WA sserikali ambao unaweza shughulikia hayo. Na baadaye watapeleka marekebisho ya bajet bungeni hivyo pesa na uwezo WA pesa upo.

Lock down kwa hakika tuliyokuwa tunaifikiria vichwani ni ya level ya nyumba isipokuwa watu watendelea kupata huduma za maduka kwa dharura baada ya kupata kibali cha kiongozi WA shina au mlinzi aliyepo barabarani.

Mengine yako safi.

Sijui mh. Rais anawaza nini. Au pengine ni Yale mawazo ya jingalao aliyoyaleta wakati alipokuja na bandiko lake like!

Wanajifariji kuwa n wakati WA curve hivyo soon itashuka.

Wanajidanganya. Wakianza kuzika kule Congo LA mboto ndipo watawafungia ninyi WA dar
 
Binafsi nafikiri ni kila mmoja kuwajibika maana tatizo ni ugonjwa,so kusambaa kwake ndio athari kubwa zaidi ni vyema kujilinda kwa hali ya juu zaidi ili kutoathiri zaidi na zaidi na pia itarahisisha kuleta wepesi kwa wale wachache watakao kuwa wameugua kuweza kuhudumiwa vilivyo na serikali.. tutaipunguzia gharama za kutuhudumia,ugonjwa unaweza kuwahi kuondoka kabla madhira hayajafika pakubwa hivyo watu kuendelea na shughuli za uchumi ndani ya muda mfupi..

Hatuhitaji kujitia ubishi lazima tuwajibike kwa pamoja..
Ni vyema waliopo mijini kutulia kutokimbilia kijijini ambapo wanaweza peleka ugonjwa na ukaathitlri sekta za kilimo na ufugaji ambazo ni uti wa mgongo..
Mengine serikali itajiongeza
 
Lockdown Dar es salaam ingekuwa njia nyingine ya kupambana na covid19 baada ya ile ya kufunga mipaka kuchelewa,lockdown ina adhari zake lakini kwa mataifa yetu ya kimaskini ni njia inyoweza kutoa msaada mkubwa katika kumaliza janga hili

Ni rahisi kupigana na ugonjwa huu ukiwa katika mazingira ya mijini hasa miji mikubwa ambapo miundo mbinu yake imepagika na kuna huduma za maji tiririka sabuni,sanitizer masks na huduma muhimu za afya. Lakini ugonjwa huu utakapofika vijijini sehemu ambazo miundombinu mingi si rafiki basi ugeuka kuwa janga zaidi. Ugonjwa unaposambaa zaidi uwezo wa kuudhibiti unapungua.

Prevention is better than cure.
 
Mkuu
Umetoa ushauri mzuri sana,
Umetumia umakini na umahihiri kutafakari,
Nakupongeza.

Natamani viongozi wenye dhamana wapite hapa, waone ushauri huu
Wachukue hatua haraka
Wasiendelee kuuwa watu

Tatizo kubwa ninaloliona Mimi
Rais alikosea tangu mwanzo, akaendelea kukosea, anajua wazi kwamba anakosea lakini hataki kuonekana ameshindwa kusimamia anachokiamini, hataki kuonekana dhaifu
Ni jambo hilo pekee ndio linagharimu Taifa mpaka sasa.

Ushauri wangu:
Viongozi acheni ubinafsi,kujificha na kuwaambia wananchi wachape kazi ni zaidi ya ubinafsi.
Tumewapa dhamana, Okoeni taifa
Reli, barabara, madaraja makubwa na mabwawa ya umeme hayana maana bila WATU WENYE AFYA.!!
Raisi Magufuli, Wakati hauko upande wako yafuatayo ni mapendekezo ya Kizalendo kabisa natoa, kama nilivyotoa mwanzoni kabisa mwa janga hili lilipoanza, Nilipendekeza Tuzuie watu kutoka nje wasiingie nchini, kwa maana mipaka yote ya nchi ifungwe (isipokuwa kwa situation maalum za. mizigo kuingia na kutoka)

hatuna jinsi sasa ni muda wa maamuzi magumu.

Situation tuliyo nayo ni ngumu kuliko hata wakati wa vita ya Kagera, ni mgumu kuliko hata harakati za kudai uhuru, WAKATI HUU TULIO NAO NI TISHIO LA, UWEPO WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA WATU WAKE

1. Kama unaweza kuilisha dar, Arusha, Mwanza na Miji yetu mikubwa piga lockdown yote nyumba kwa nyumba, Kama huwezi basi Piga Lockdowndown miji hiyo kwa level ya kata, siyo nyumba kwa nyumba, aliyeko Mwenge asiende kinondoni, aliyeko Kinondoni asiende Posta, masoko ya chakula yawe wazi, Hospitali ziwe wazi, watu watoke mmoja mmoja kwa ajili ya essential goods. Hakikisha unaplan vizuri watu hawafi kwa njaa, Mtihani upo kwenye watu kula Hapa umiza kichwa sana

2. Kopa watumishi wa umma kwa muda wa miezi miwili, Kata mishahara Ya watumishi wa Umma wenye kipato cha milioni moja kwenda juu kata 50%, wenye kipato cha laki tano kuja chini kata 10%. Hizi pesa ziwe deni la ndani ambalo serikali itakuja kulipa siku moja. Hizi pesa zitumike kununulia Chakula na Kukigawa bure kwa wananchi.

5. Ndani ya mikoa, kwenye mikoa ambayo haijaathiriwa sana, Funga nchi kwa level ya wilaya, mtu asitoke wilaya moja kwenda wilaya myingine.

6. Funga nchi yote kwa level ya mkoa, Safari zote za mikoa zife

8. Chagua nyumba kadhaa kila kata za miji ya Dar, Arusha, Mwanza na ile ambayo inaonyesha dalili za kuwa hardly hit ziwe supply point (maghala) kwenye kata hizo

7. Rasilimali za Jeshi la wananchi kama vile magari ya kijeshi zitumike kusambaza bidhaa muhimu nchi nzima, kwenye masoko na kwenye supply point katika kila kata, na kila Mwenye usafiri wa gari katika kila kata awe identified ili awe supplier wa essential goods katika kata yake, awezeshwe kwa mafuta

8. Tumia mtandao ulionao, Matawi ya CCM, Viongozi wa nyumba kumikumi, Misikiti ya maeneo, Makanisa, Vituo vya polisi, Hapa pia uwe makini isije ikaonekana misaada inakuja kwa misingi ya udini, uchama n. k

9. Challenge kubwa ni wale watu wasio na makazi maalum, ambao hula magengeni, ambao hawajui kupika, ambao hawana nyenzo za kupika, Hapa inabidi uumize kichwa kwelikweli maana ukikosea hapa watu watavamia nyumba nyingine kupora chakula. Hapa unaweza kutumia shule za msingi na sekondari zilizofungwa kuwaweka hawa na kuwasaidia kwa chakula.

10. Tulipeleka vijana wetu JKT siyo wakapige kwata, bali kwenye wakati kama huu tuwaite on duty watekeleze duty kama za kusimamia order kwenye kipindi kama hiki, kwa hiyo hawa ambao ni reserve army waitwe wasaidie kuimplement lockdown hizo nilizopendekeza

Mzee, lengo la lockdown, ni kulocalize cases zilipo kirahisi na kuziidentify maana baada ya muda fulani wataonyesha dalili, kuzuia maambukizi kusambaa na pia kusaidia mfumo wa afya usicollapse kwa kuzidiwa na new cases za kiwango kikubwa

Mzee Ulikosea kutofunga mipaka hapo awali kwa kuhofia uchumi(Kama alivyosema Polepole), Sasa Uliacha kuuanika, leo tunautwanga mbichi.
Wahenga hawakuwa Wajinga kusema heri kinga kuliko tiba!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni serikali ianzishe vituo vya kupima corona kila mtu akapime Afya yake kuangalia kaukwaa ama vipi. Kwa sababu hii staili ya kusubiri mtu aumwe ndo aende hospitali ndo wampime ndo wakute ana corona itatumaliza.

zile nchi ambazo tunaona maambukizi yapo juu ni kwamba wanawapima wananchi wao hususani kwenye miji ambayo imeonekana kuathirika zaidi.

Kwa sababu tulishafanya uzembe tukaruhusu wageni wenye corona waingie nchini wakati ugonjwa umepamba moto na baada ya wageni kupungua ndo mkafunga anga wekeni vituo maalum watu wakapime.

Sent using Jamii Forums mobile app
wabongo tumekuwa hodari sana sasa hivi kushauri kuhusu Corona. Huko kupima inahitaji hela nyingi na vifaa hata nchi Tajiri imewashinda.

The only cure for this virus is to stick our asses at home and seek divine intervention!
 
Hiyo namba moja imeshashindikana. Sad to say so!
Mambo mengi uliyoshauri yalipaswa kuchukuliwa day one alipogundulika.
Nimenukuu hapa "Situation tuliyo nayo ni ngumu kuliko hata wakati wa vita ya Kagera, ni mgumu kuliko hata harakati za kudai uhuru, WAKATI HUU TULIO NAO NI TISHIO LA, UWEPO WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA WATU WAKE"
 
Mkuu
Umetoa ushauri mzuri sana,
Umetumia umakini na umahihiri kutafakari,
Nakupongeza.

Natamani viongozi wenye dhamana wapite hapa, waone ushauri huu
Wachukue hatua haraka
Wasiendelee kuuwa watu

Tatizo kubwa ninaloliona Mimi
Rais alikosea tangu mwanzo, akaendelea kukosea, anajua wazi kwamba anakosea lakini hataki kuonekana ameshindwa kusimamia anachokiamini, hataki kuonekana dhaifu
Ni jambo hilo pekee ndio linagharimu Taifa mpaka sasa.

Ushauri wangu:
Viongozi acheni ubinafsi,kujificha na kuwaambia wananchi wachape kazi ni zaidi ya ubinafsi.
Tumewapa dhamana, Okoeni taifa
Reli, barabara, madaraja makubwa na mabwawa ya umeme hayana maana bila WATU WENYE AFYA.!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Siamini kama "wazee wa kitengo" hawakushauri haya.
Usalama wa Taifa .......
 
Back
Top Bottom