KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Sikukusoma baadhi ya sehemu, kwa sababu unayopendekeza toka huko juu hayana nguvu tena.Mzee Ulikosea kutofunga mipaka hapo awali kwa kuhofia uchumi(Kama alivyosema Polepole), Sasa Uliacha kuuanika, leo tunautwanga mbichi.
Wahenga hawakuwa Wajinga kusema heri kinga kuliko tiba!
Kinachoweza kufanyika sasa nchi nzima ni kuhimiza yanayofanyika kama njia za kinga yafanyike nchi nzima kwa msisitizo na ukamilifu zaidi.
1. Himiza kuvaa barakoa kwa kila mtu, hata kama ni kukunja kanga au nguo yoyote ile na kujifunika nayo puani na mdomoni kila anapotoka nje ya nyumba. Hii isisitizwe kabisa, bila kukosa.
2. Usafi, kunawa mikono na kusafisha sehemu zote zinazotumika, kama meza, n.k. na kutumia 'sanitizers'. Wananchi wasaidiwe kuwa na vifaa hivi kila wakati na kuvitumia.
3. Kuachana kabisa na mikusanyiko ya watu ya aina yoyote ile, hata hiyo ya kuabudu. Mungu ni mwema sana kwa binaadam, sijui kwa nini watu hupenda kumfanya aonekane kama hana uwezo wa kusikia sala sehemu yoyote ile, hata toka chooni.
Watu waendelee na shughuli zao za kipato, mradi "Social Distance" izingatiwe kila sehemu. Na sehemu hizo usafi uzingatiwe, 'sanitizer' kila sehemu za maeneo hayo.
Hakuna sababu tena ya kufanya 'lockdown' mahali popote, kwa sababu manufaa ya hiyo ishapitwa na wakati. Ugonjwa ushasambazwa kila sehemu nchi nzima.
La mhimu sasa ni kutumia kila linalowezekana huko huko, kuzuia kusambaa maambukizi ya ziada.