#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
watu kama nyie corona iwaondoe tu, kama kujenga hoja tu huwezi
Kwa uhuni unaoufanya hapa jamii forum ntampigia simu Ummy Mwalimu au Waziri mkuu na kukuripot kuwa una Korona virus na unataka kuja kuisambaza hapa jamii forum..

Seek respect, not attention. It lasts longer
 
Ndugu zangu wapendwa,

Kwanza tupeane pole kwa janga hili linalotukabili kwa sasa.

Nimekuja kwenu naomba msaada wa ushauri. Mimi ni mtumishi wa umma. Tangu mwaka 2018 nilipanga nipambane kutafuta vijisenti ili mwaka huu mwezi wa tano nianze kujenga kabanda kangu kakuishi. Nimezichanga weee nina kama milioni 9, kiwanja ninacho na tofali ninazo sasa najiuliza weee majibu sipati.

Janga la corona linanichanganya, niko mkoa wa Njombe. Najiuliza kama corona ikaendelea kwa muda mrefu serikali ikayumba kiuchumi watumishi tukapata lidandasi (kuachishwa kazi) na hela hiyo nikawa nimeshapeleka kwenye ujenzi yote hii familia nitaiendesha vipi?

Nianze ujenzi au nisubiri corona ipite? Nimechanganyikiwa.

Ushauri wenu great thinkers.
 
Nimezichanga weee nina kama m 9,kiwanja ninacho na tofali ninazo sasa najiuliza weee majibu sipati. Janga la corona linanichanganya,niko mkoa wa Njombe.
Hongera kwa kufikia hapo ulipofikia

Kiasi hicho ni kikubwa sana

Angalia hii thread na mchanganua wa milioni 7, Utakutia moyo.

Ingia hapa: Nmejenga ujenzi rahisi kwa Milioni 7 tu - JamiiForums
Najiuliza kama corona ikaendelea kwa muda mrefu serikali ikayumba kiuchumi watumishi tukapata lidandasi (kuachishwa kazi)
Usiyape nafasi mawazo hasi,
hela hiyo nikawa nimeshapeleka kwenye ujenzi yote hii familia nitaiendesha vipi?
Nianze ujenzi au nisubiri corona ipite?
Anza sasa kujenga.
Kumbuka fedha huwa haikai, chukua hatua sasa.
 
Hongera kwa hatua uliyofikia, hata kama ni kuendelea na jengo wewe ukiwa mfanyakazi wa sekta ya afya huoni kuwa utaweka mkusanyiko usio wa muhimu kwenye jengo lakini (nikimaanisha mafundi)

Harakati za kununua vifaa na kusimamia jengo kwa sasa ni shughuli zinazoweza kusubiri.
 
long live my love,

Anza ujenzi achana na corona wala risks zozote zilizoko mbele yako. Kuna vitu lazima uvifanye no matter Maisha yatakuwaje mfano elimu, ndoa na kuanzisha familia na ujenzi wa nyumba. Hayo mambo hayana excuse huwezi kusema sisomi kwa kuwa kuna UKIMWI au COVID -19 au huwezi kuhairisha kuoa sababu ya COVID 19.

Kwanza umekosea sana kanuni ya ujenzi maana hiyo hela uliyonayo umeifuga bure wakati sasa hivi ungekuwa na boma linasubiri kupauliwa usiku watoto wanapigana miti.

Usisubiri hela iwe nyingi ndio ujenge. Unaweza kuanza hata na laki moja au pungufu na ukapiga hatua

Hongera baba mwenye mjengo mtarajiwa
 
Asante sana mwamba. Nimejifunza kitu kikubwa kutoka kwako.
 
Hongera kwa hatua uliyofikia, hata kama ni kuendelea na jengo wewe ukiwa mfanyakazi wa sekta ya afya huoni kuwa utaweka mkusanyiko usio wa muhimu kwenye jengo lakini (nikimaanisha mafundi)

Harakati za kununua vifaa na kusimamia jengo kwa sasa ni shughuli zinazoweza kusubiri.
Sidhani kama watazidi wanne. Nikifuatilia social distance kutakua na ubaya?
 
Ni hivi ndugu unajua kuna kasumba hadi uwe na mamilioni ndo uweze jenga, hapana ndugu anza sasa maana hili jambo la corona sio la kuisha leo wala kesho imagine ukimwi ulivyoingia watu wangesema wasubiri iishe...kikubwa jitahidi kufanya reserch upate gharama angalau ya kila hatua...kuanzia msingi,boma,mbao bati etc..wewe ushakua na familia unahitaji kuwaweka wanao kwao....nikuaminishe inawezekena nami nipo kwangu na maamuzi magumu nilifanya mwezi wa 10 baada ya miezi mi3 mwezi wa 1 niliweza hamia...ujenzi wa Mtanzania sio wa kuchukua siku moja.
 
Ni hivi ndugu unajua kuna kasumba hadi uwe na mamilioni ndo uweze jenga...hapana ndugu anza sasa maana hili jambo la corona sio la kuisha leo wala kesho imagine ukimwi ulivyoingia watu wangesema wasubiri iishe...kikubwa jitahidi kufanya reserch upate gharama angalau ya kila hatua...kuanzia msingi,boma,mbao bati etc..wewe ushakua na familia unahitaji kuwaweka wanao kwao....nikuaminishe inawezekena nami nipo kwangu na maamuzi magumu nilifanya mwezi wa 10 baada ya miezi mi3 mwezi wa 1 niliweza hamia...ujenzi wa Mtanzania sio wa kuchukua siku moja.
Asante mkuu
 
Nawashukuru sana. Kwa replies hizi chache nimeshatambua nilikuwa nawaza tofauti. Ngoja nianze mapambano,nitareta mrejesho.
Ila uchore Ramani za kisasa madirisha makubwa hewa ya kutosha na pia nyumba iwe ndefu sio mgeni amesimama anajinyoosha anagusa gypsum. Pia kila chumba kiwe self contained ndio tunavyojenga mjini. Sebule na jiko view na nafasi ya kutosha

Ukimaliza uje mjini nikupeleke maduka ya flat screen ya inch 72 unafunga na sound bar ya watts 1000. Unafurahia Maisha katika mwanga bora kabisa
 
Back
Top Bottom