#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Moja kwa moja kwenye mada.

Kufuatia mwendelezo wa hatua za serikali kuhusiana na ugonjwa wa Corona nchini ikiwamo hotuba ya jana ya mheshimiwa rais, ni wazi sasa mheshimiwa anahitaji mawazo mbadala.

Mawazo mbadala hatayapata tokea kwa hao waliomzunguka wala hao wakuu wanaomzunguka ambao kwa sababu zilizo wazi wana matumbo yao yanayohofia tumbuzi.

Ilikuwa muhimu sana, kwa maslahi ya taifa hili mheshimiwa rais akakutana sasa na watu wengine wanaowasilisha mawazo tofauti, angalau kwa mazungumzo tu:

1. Baba Askofu Niwemugizi
2. Askofu Dr. Bagonza
3. Mheshimiwa Zitto Kabwe

Na wengine wa namna hiyo waliojipambanua kuwa hawana maslahi binafsi.

Mkuu watu hawa watakusaidia kuliokoa taifa hili. Kumbuka umoja ni nguvu.

Kwa nini Uganda waweze?


Na sasa ndio amejifungia kijijini ndio tutegemee mambo ya kienyeji zaidi.
 
Wito ni wizara kutoa takwimu sahihi, kule worldometer Tanzania haina idadi ya watu waliopimwa wakati mataifa mengine hutoa takwimu hizo kwa uwazi!

Kama wameamua kuwa wakweli basi waseme kila kitu kwa uwazi hadi wanaokufa!
 
Raisi yuko sawa sana, hizo barakoa wengi tu tulitilia mashaka toka mwanzo, na huo mvuke hajasema ukiwa wa moto hivo watanzania tuache mambo ya kujua sana, maji yanapata moto na kuua vidudu yakifikia nyuzi joto Mia moja, Sasa hapo yapo tayar kutumika, tumuamini raisi wetu hizo taarifa wa chini yake ndio wanamfikishia wako na ujuzi mwingi kuliko wengi wetu humu ndani ambao tunaendeshwa na mihemko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania kusalimika, labda jamii ya kimataifa iingilie kati. Kwa hatua ambazo zinachukuliwa na mataifa mbalimbali, itafika wakati Dunia nzima kutatulia, wakati janga likitokota nchini mwetu.

Kuna hatua unaweza kuficha, kuna hatua haiwezekani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunapambana na Corona, kalipoanza ndio kalikuwa ka Corona sasa ni Corona, tuwasikilize viongozi wetu kwa kutekeleza kila maelekezo tunayopewa.
Tufuate maelekezo ya kitaalamu ya jinsi ya kujikinga lakini pia tuongezee na tiba asili na tiba mbadala.
P
Paskali,itendee haki nafsi yako.With this, you may end up with split mind!!!Tiba mbadala,tiba mbadala,mmh
 
Nakumbuka msanii MwanaFA ni miongoni mwa watanzania wa mwanzo kabisa kujitangaza kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19. Na baadaye RC Makonda alithibitisha hilo pale stendi kuu ya mabasi ya mikoani Ubungo alipozungumza na wananchi kuhusu athari za Corona.

Kwa kuwa mwanaFA amepona kabisa ni vema wizara ya afya ikamtumia kama balozi wa kuelimisha jamii na kuitoa hofu kwa kuiaminisha kwamba Covid 19 inapona.

Aunganishwe na Mrisho Mpoto kwenye zoezi la kuelimisha Umma linaloendelea.

Ni hayo machache,

Maendeleo hayana vyama!
 
Hii secta utachukuwa hata miaka 5 na zaid kurecover. Unless kuwe na chanjo ya korona na kila raia apatiwe. Hakuna watarii watarusk maisha yao kwenda kwenye nchi iliyokuwa na taarifa au data zilizichezewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuwa mwanaFA amepona kabisa ni vema wizara ya afya ikamtumia kama balozi wa kuelimisha jamii na kuitoa hofu kwa kuiaminisha kwamba Covid 19 inapona.
Kwani haijulikani kwamba wapo wanaopona? Mnabuni vimiradi vya upigaji, mara sijui kupulizia mitaa madawa, mara kupulizia mabasi, mara satnaiza
 
  • Thanks
Reactions: rr4
Akihutubia kutoka mafichoni chato, amesikika akipigia debe tiba ya kujifukiza mvuke kwa waathirika wa corona.

Hii itasababisha watu wengi watakaoambukizwa ugonjwa huu kubaki majumbani wakijifukiza mvuke badala ya kwenda hosptali kwani wameambiwa hakuna tiba. Matokeo yake wagonjwa wa majumbani waambukiza watu wengi zaidi, kuanzia kwenye familia na nje ya familia.

Pale mgonjwa atakapofariki atazikwa mazishi ya kawaida kwani familia itakuwa imeficha siri ya mgonjwa na kuzidi kumbukiza watu wengi zaidi.

Hakika mweshimiwa amekosea sana na tutegemee maangamizi makubwa

Yajayo yanatisha
 
Hata bado sijaamini kama kweli huyo Mwana FA aliugua hiyo Corona, juzi tena mkaja na yule mlevi eti nae anaumwa Corona, nikashangaa mtu gani anaugua Corona halafu anaruhusiwa kutuma salamu?!

Ma- celebrity wanatumiwa kutangaza utalii na mengine kama hayo, hawa wa kwetu tunawatumia kutangaza ugonjwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watalamu wanasema sehemu kubwa ya maambukizi mhusika anajiambukiza mwenyewe kwa kujigusa usoni na mikono yake. Wengi wetu tuna hulka kugusa uso macho, pua,mdomo kila baada ya muda mfupi. Suluhu hapa ni kupaka mikono pilipili, jaribu kwa siku tatu pekee .Utajiounguzia ama kuacha tabia kugusa uso huku tukiendelea na tahadhari zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom