Wakuu jana tumemsikia mheshimiwa Rais wakati akizungumza na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kule nyumbani kwake Chato kuwa, wizara ya afya itoe takwimu sahihi za idadi ya watu wanaopona ili kuwatolea watu taharuki. Kwa mjibu wa Mh Rais idadi ya waliopona ni zaidi ya watu 100 ilihali wizara ya afya bado inautangazia umma ya kuwa waliopona ni 11 tu.
Wakuu ikumbukwe kuwa mlipuko huu ulizikumba kwa wakati mmoja nchi za ukanda wa Africa mashariki lakini mpaka Jana idadi ya waliopona Kenya walikuwa watu 85, Uganda 51 na Rwanda zaidi ya 100 huku Tanzania waliopona wakiwa ni wachache zaidi miongoni mwa majirani zetu.
Sasa basi wizara itoe data sahihi kama alivyopendekeza Mh Rais, lakini pia wizara ihakikishe inazuia aina yoyote ya tarifa inayoweza kuzua Taharuki , miongoni mwa taarifa hizo kama ile ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam akisema Kuwa watu wanapukutika hii si Sawa.. .
Wakuu tuchapeni kazi huku tukifaata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wetu .