Mimi sijui kuhusu Tanzania hivyo ningependa niweke maoni kiujumla,
Kuna baadhi ya nchi ni aibu kuwa na wagonjwa wengi wa COVID-19 sababu njia zilizotumika kudhibiti ugonjwa aidha zilichelewa kuchukuliwa, au hajiza chukuliwa kabisa.

Kwa lugha nyingine hizo nchi zilizembea kuchukua hatua madhubuti tena kwa wakati.
 
Hata idadi ya vifo vya corona wanachakachua wanaficha ukweli matokeo yake corona imeonekana siyo Tatizo ni kaugonjwa kadogo ka kuombea kanisani kanaisha
 
Magafuli nchi imemshinda

"Naodha tosa nanga
Abiria sote twateseka"
 
Tatizo walisema ni "kaugonjwa"!!
Watu wamejanaza vijiweni vibarazani watoto wadogo wanacheza pamoja uswahilini zote huko jiji Dsm ndipo penye shida kubwa sana misongamano vituo vya basi bodaboda bajaji daladala mwendo kasi ni mkubwa uvaaji wa masks ni wa hovyo hovyo hawavai vizuri ipasavyo
 
Magafuli nchi imemshinda

"Naodha tosa nanga
Abiria sote twateseka"
waliwapora upinzani wenyeviti wa Serikali za mitaa ikabakia CCM peke yake lakini huko mitaani ndipo kuna vijiweni maambukizi makubwa hakuna Matangazo ya kuzuia watu kukaa vijiweni hakuna msaada kwa wananchi wamekaa tu wakiangalia watu wakizidi kuambukizana zaidi kwenye mikusanyiko isiyo na tija
 
Corona haina aibu yoyote. Kama ingekuwa na aibu basi hiyo aibu ingeanzia USA, UK, Spain, Italy... Ni ushamba tu wa mtu mmoja kama alivyosema Nape. Bahati mbaya huyo mtu yuko kileleni.
 
Kwa mujibu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr J P Magufuli, hofu ni ugonjwa hatari zaidi kuliko hata virusi vya Corona! Ndiyo, unapokuwa na hofu kunakosekana umakini na ujasiri hali inayopelekea watu kukata tamaa. Tunapokata tamaa maana yake ni kuwa umuhimu wa kuchukua tahadhari unakosekana.

Yanasemwa mengi kuhusu COVID-19 lakini ukweli unabaki pale pale kuwa hili ni janga la dunia na maafa yake ni makubwa kiasi kwamba hali inatisha! Kwa sababu hiyo, jamii iendelee kuelimishwa juu ya vipimo vya kujikinga na balaa hili la dunia na kwamba njia nyingine ambayo inaweza kuisaidia jamii kuondoa au kupunguza hofu ni ukweli wa taarifa za wenye matatizo, wenye hali nafuu, wenye hali mbaya sana, vifo na mipango endelevu katika kukabiliana na tatizo hili.

Kama haya hayakufanyika tena kwa wakati, hofu itaendelea kutanda miongoni mwa jamii
 
Hiyo video hapo chini inaonyesha vijana wanavyoenda sawa na kasi ya awamu ya tano, yote ni katika kujitafutia ugali, hata ikibidi kuning’inia kama popo toka ghorofa ya 10. sasa vijana kama hao uwaambie Corona watakuelewa kweli?
Your browser is not able to display this video.
 
Wanatekeleza maagizo kutoka juu.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Wataalamu wa afya mnatuambia gonjwa hili halina tiba harafu mnasema wagonjwa wanapona au kupata ahueni .

Inamaana kuna kupona kama kupo mkisema halina tiba mnamaana gani ?

Je mnatutisha huku mkijua matibabu yapo?

Nimeambiwa kuna watu wanaletwa wakiwa mahututi na baadae wanapona kabisa so kumbe kuna kupona ?


Hivi maana ya ugonjwa kutokuwa na tiba wala kinga inamaana gani hasa?


Kukumweupe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuanzie hapaa.. Mkuu, umeshawahi kuumwa mafua!??
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanapona madhara yatokanayo na kolonya

Jr[emoji769]
 
Kichwa cha habari chajieleza.

Uzi huu ukitumika bila kudharau au utani basi yaweza kusaidia watu wengi katika kupambana na hili dubwasha linalojiita KORONA lilitokea huko China.

Kila mmoja aandike mchanganyiko wa tiba asili au matunda asili ambayo imemsaidia yeye au mtu mwingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…