https://www.facebook.com/video.php?v=1307593556118005
Utaratibu na maandalizi ya kudhibiti ugonjwa huu yamefanywa kwa kiwango kidogo sana, huu ni mtazamo wangu, na kwa jinsi tunavyo li handle hili swala. Hili ni swala hatari, ni swala ambalo lilipaswa kuileta nchi pamoja. Tulipaswa kukaa na wataalamu watushauri na sisi wanasiasa tujadili. Tuwe na mpango wa dharura bungeni, tutafute budget ya dharura ya kushughulikia hili swala.

Kwa mfano mwezi wa pili, wakati hili swala limeanza China. Mchungaji Peter Msigwa Mbunge wa Iringa, aliiomba serikali tulijadili kama swala la dharura. Seirkali ijlere mpango bungeni wa kutuonyesha implications za hili swala kwenye maisha.
 
Watu wengine sijui kwanini hawakufaga kwenye Vita ya majimaji
 
Hakuna msaada ambao serikali ya ccm inaweza kuutoa kwa wananchi kama hauna faida kwao. Ingekuwa ni uchaguzi wangegawa t-shirts, kanga kofia kwa almost watu wote nchi nzima lakini hawawezi kutoa barakoa kwa wananchi wake.

Juzi nilisoma kuwa ventilator ni shs 56 m. Unashangaa serikali inashindwaje kuweka hata kumi kwa kila hospital iliyotengwa kushughulika na wagonjwa wa corona ili watu waweze kupata huduma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunanunua Wabunge na Madiwani
 
Tuliyoshangaa tupo wengi bhasi!
Millioni 56 ni pesa ndogo sana kwa serikali ajabu tuna upungufu mkubwa sana wa ventilator.

Hatupo serious! Hili janga limetonyesha na limetufunza mengi kwa wenye kuona na kutafakari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…