Ndugu zangu, Ugonjwa ulivyoripotiwa huko Kenya tulisema mengi mno.Nilikuwa Arusha siku hiyo.Nilishuhudia mbwembwe nyingi kwa wakazi wa Arusha.Mask ,sanitiser na groves.
Baadaye akatangazwa mgonjwa wa kwanza katika nchi yetu. Mtu mmoja aliandika katika social network kuwa " kipele kimempata mwenye kucha".
Leo waziri Mkuu katangaza maambukizi kufikia 480. Idadi inakimbia mno, nadhani tuko juu katika East Africa. Sio vizuri kwetu, na kwa majirani zetu pia.Baadae ninahisi tutatengwa sisi.Itakuwa mbaya mno kwetu.
Kuna viongozi wana muono tofauti .Mfano niliona video ikimuonyesha Dc wa Iringa akisema kuwa watengeni watu wa Dar es salaam. Nilimpenda mno.kusema kweli sasa hivi ukienda mikoani, umetoka Dar unatisha.
Sasa tuangalie Dar es salaam, jiji letu lililosheheni watu wa kila namna Wanaojua sana na wajanja mno.Toka Rc wa Dar es salaam atuhimize kuvaa barakoa, kuna vichekesho vingi mno kila mahali.Katika daladala waweza kukuta zaidi wa watu 10 hawajavaa barakoa.Nenda mtaa wa Kongo na masokoni, kwenye masoko/magulio ya wiki, hakuna anayejali. Sio mnunuzi wala muuzaji.Nenda Mbagala kaangalie ule msongamano wa wafanyabiashara na wanunuzi. Ninachokiona mbele kabisa kinatisha.
Raisi , kwa kujua hali zetu, hapendi lock down wala kufunga mikoa. Lakini kwa dharau zetu, kwa kuwa hatuwezi na hatutaki kufikiri tutakwisha.
Tufanyeje?- Askari watumike kukamata watu wanaozagaa mitaani bila barakoa.Wakenya na Wahindi wamepigwa mpaka wameelewa. Magari ya abiria yasimamishwe katika maeneo yoyote , askari waangalie wale wanaopuuza kuvaa barakoa, wawashushe wawatandike, pamoja na kondakta aliyewapakia.
Viongozi wetu hawaendi Kongo Street wala Mbagala. Hivyo basi watume watu kuangalia hali halisi.Hizo sehemu hatarishi zifungwe.Nina mengi ya kushauri , lakini nimshauri nani?
Stay home, stay safe
Sent using
Jamii Forums mobile app