#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Niliacha kazi nikaenda shule lakini mwanaume niliyenae ndiye aliyenifanya niende shule! Jana mwanamke wake kanitafuta kaniambia niachane nae kwani ye ndo yupo nae saiz jamani nina maumivu makali nilishaenda shule corona imenirudisha naiona likizo ya corona chungu kwangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliacha kazi nikaenda shule lakini mwanaume niliyenae ndiye aliyenifanya niende shule! Jana mwanamke wake kanitafuta kaniambia niachane nae kwani ye ndo yupo nae saiz jamani nina maumivu makali nilishaenda shule corona imenirudisha naiona likizo ya corona chungu kwangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Njoo PM mkuu nikufariji katika kipindi hiki kigumu chenye unapitia.

Dah nimesikitika sana.
 
Sasa ndio tumeanza kuona kitumbua si andazi. Kuna Mtanzania ameenda India kutibiwa Corona?

Tungekuwa na Mlonganzila tatu Dar es salaam na moja kila mkoa hii Corona isingetubabaisha.

Tujifunze somo hili kubwa, Huko Italy na Hispania pamoja na hospitali zao nzuri kuna wagonjwa wanalala kwenye corridor za mawodi kama tunavyoona Muhimbili.

Tujifunze na somo zuri la Corona kuweka afya mbele.
 
Siasa, maradhi na uzalendo! haviingiliani kamwe.

Niendelee kutoa pole kwa wananchi wenzangu wa Duniani kote dhidi ya ili janga la corona hakika Mwezi Mungu atufanyie wepesi waja wake Tanzania tupone gonjwa ili.

Niseme wazi ninaungana na Dunia nzima kupiga goti na kuomba maradhi haya yatupitie mbali wana wa Mungu.

Niende kwenye mada yangu au kiini cha mie kuishika kalamu na kuandika haya.

Siku chache baada ya kuibuka kwa maradhi haya ya corona mataifa mengi yanetangaza kuchukua hatua mbali mbali sina sababu ya kuzirejea kamwe.

Tanzania pia tumechukua hatua mujarabu kabisa ingawa ndani ya mujarabu yawezekana mwijarubi ikawemo naamanisha uovyo ovyo waweza kuwemo mfano wake mzuri ili mnielewe ni kukatazwa kukusanyika ila inajitokeza lijua limoja linakusanya watu na kuanza kuimba ttarabu ilihali Dunia inalia.

Bhana hehehheee ukiendelea kuandik kwa kununa haitofaa, shiriika la ndege la Tanzania wengi tunajua kuwa Mh Rais wetu amelifufua kwa kupitia kodi zetu watanzania wote.

Ndege nyingi zilizonunuliwa bei zake hazikulenga kupandwa na watanzania wote na badara yake ziliekezwa ziende nje ili wapande wao kana kwamba zilinunuliwa na wao tu.

Sasa nimeskia juzi zimerudi zote zipo Tanzania na bei sasa imeshuka na zinazanfanya kazi ndani ya taifa.

hahahaha mimi nasema nyie si vidume na corona ni likidume zaidi

Sasa tunashukuru videnge vyetu vitatubeba kichwa mkia na miguu mpk vijijini kwetu.

Uzalendo kwanza .

sifileo kesho ikifika ntakuwa tayari kufa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uwepo wa corona tumejifunza yafuatayo:-

1.Imerudisha utu

2.Imerudisha watu kwa muumba wao na
Kuishi kimaadili zaidi

3. Imefanya watu kutii amri za Allah kufungwa kwa Bar. Casino na madanguro kwa kuhofia corona. Biashara za ngono na ulevi na kamari zimefungwa

4.Imefanya wanafamilia mudamwingi kuwa paoja na kuijiepusha na michepuko

5. Imefanya watu waache kula mizoga na wanyama wasioruhusiwa na sheria ya Allah kuliwa

6. Imefanya watu kutunza afya zaidi kama alivyo elekeza Allah.

7. Imefanya Waarabu huko Uarabuni waache kuvuta shishi na kula mirungi kwa kuhofia corona.

8. Imefanya watu kila mara kuomba dua na kumkumbuka Allah kinyume wakati ilivyo kua hakuna coron.na hata waliojiweka mbali na Allah sasa wanamkurubia kwa maombi

9. Imekatiza Udikteta wa viongozi na majigambo ya nguvu za kijeshi na za kiuchumi

10. Ibada imeshika nafasi zaidi kwa watu kuliko masuala mengine ya kimaisha.

11. Imefanya watu kufuata mafunzo ya mtume Muhammad( s.a.w) kuziba mdomo na pua unapotoa chafya au miayo au kukohoa.

12.Imefanya mamlaka husika kutazama na kujali zaidi wafungwa wake.

13.CORONA Imetufundisha kimatendo kua binaadam si lolote wala chochote katika mgongo wa Ardhi akipenda Allah anaweza kuwafuta wote kwa wakati mmoja kupitia jeshi lake la kiumbe CORONA VIRUS

HILI NDILO SOMO MUHIMU KATIAK KUENDELEA NA SHORT COURSE YETU HII YA MDUDU CORONA.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa muelewa anaishi kwa kutafakari. Uliyoyaona ni sahihi ingawa watakuja wapingaji watakupinga kwa hoja za kusimama kwa shughuli za kiuchumi kutokana na mlipuko wa korona.
 
Nyie mnaosema sijui kwenye movie Flani au kitabu Flani Corona ilikuwa predicted sasa mbona awakupredict dawa , yakutibu huu ugonjwa.

Waafrica nawaomba , tufate Yale yanayosemwa na wataalamu wa Afya , na sio awa wazee wa ramli+ politician Ambao / wao Wanaangali Tumbo kwanza.

Tusipokuwa makini Africa corona itakuja / kuwa mtaji wa wazee wa Fursa zakuhamasisha.
 
Nyie mnaosema sijui kwenye movie Flani au kitabu Flani Corona ilikuwa predicted sasa mbona awakupredict dawa , yakutibu huu ugonjwa.

Waafrica nawaomba , tufate Yale yanayosemwa na wataalamu wa Afya , na sio awa wazee wa ramli+ politician Ambao / wao Wanaangali Tumbo kwanza.

Tusipokuwa makini Africa corona itakuja / kuwa mtaji wa wazee wa Fursa zakuhamasisha.
Mkuu unadhani ni Africa tu hizo za movie na vitabu hata wazungu wanatambaa nazo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti ni kwa nini mtu anaweza kuugua kisukari,ukimwi,Tb,pressure,maralia na wakati huo huo akapata maambukizi ya Corona lakini Akifa Anatangazwa kufa kwa Corona ?

Kwa nini asitangazwe kufa kwa ugonjwa mwingine hapo juu,Either pressure,maralia,Tb au Ukimwi,? ni sababu zipi zinazomfanya daktari aandike Report ya kifo chake zidi ya corona.

Naomba kufahamu


Cc Zero IQ


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom