Tunaona kwa wenzetu Ulaya na Asia kwa namna ugonjwa huu unawadhuru. Tunaona kwa namna ambavyo Italy waziri mkuu analia hadharani kwa jinsi ambavyo ugonjwa huu umeshindikana kudhibitiwa hadi mrusi anasema ataenda kutoa msaada. Kwa wenzetu hili jambo tayari limeshaweka historia mpya kwao hata kama litaisha.
Kwetu sasa. Si tunasema kuwa sisi ni immune? Yaweza kuwa kweli kabisa na tukishapuuzia maisha yanaendelea huku corona akiendelea kuishi baina yetu. Tunaugua mafua na homa tunapona huku corona akiwa ndani hawezi kudhuru ila anaambukizwa kwa mtu mwingine.
Ulaya, Marekani na Asia wakishafanikiwa kuudhibiti huko kwao kitakachofuata ni kuiweka Afrika kwenye total isolation. Hatutaruhusiwa kwenda nje ya Afrika. Wanatuona tunavyoubeza huu ugonjwa. Wakati ukifika tutasaga meno hivyo ndugu zangu, nimeandika kwa uchache ile unumbe umefika. Itakuwa ni zaidi ya Apartheid. Zaidi ya Xenophobia. Tuwe makini nasi kama wananchi tushirikiane na serikali zetu ili Ulaya na Asia wakitokomeza na huku uwe umeisha
Huo ujumbe niliuweka ila Mods wakaunganisha na zingine. sasa tunachoona ni kuwa China wametoa tangazo kuwa wamezuia wageni kuingia China hadi hapo watakapoamua vingine. Hili zoezi kwa kweli litachukua muda mrefu sana hadi pale chanjo itakapopatikana kwani China haitaweza tena kuruhusu nchi yao kuingia kwenye janga kama hili. Italia na Uhispania wanalia. Kesho utasikia wamepiga marufuku ya hali ya juu kwa wazamiaji wote kwa kigezo cha corona.
Niliona katuni moja waafrika wanazuia wazungu kuingia Afrika na ikawa kama mzaha vile. sasa katazo la kutoka nje ya Afrika likianza tutapata taabu sana. Ni kwamba Afrika chini ya Sahara ndiyo itakayoathirika na hii aftermath. Waafrika wataonekana ni career wa virusi hivi na watakuwa na uwezo wa kuvisambaza tena nje ya Afrika na janga lingine linaweza kuibuka, hivyo hawatakuwa tayari hawa watu
Mwanzo walikuwa wanahoji kwa nini Afrika haijaathirika, na hakuna vifo. Walijisikia vibaya na bado wanajisikia vibaya. Pamoja na malaria, kipundupindu, ukimwi, ebola, njaa; bado hawaoni kuwa kwetu yanatosha. Walipenda tushirikiane nao kuugua hii corona. Sasa kwa kuwa inaonekana kushindikana kuugua, itawezekana kushuhudia kipindi kigumu na cha mpito kwa Afrika kuelekea kuitokomeza corona. India kuchapa viboko raia wake wanaokaidi amri ya isolation sio kama hawajui. Rwanda na Uganda hadi kutumia risasi za moto si kama hawajui. Tujifunze na tuamke sasa ili kwa pamoja tuutokomeze huu ugonjwa