#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
''Lock down'' kwa Tanzania ni ngumu watu tunaishi kwakipato cha chakula cha kesho ama leo wengi hawana uwezo wa chakula cha mwezi mzima. Kuwa mzee haina maana unakaribia kufa kwanza vijana ndiyo rate yao ya kufa ni kubwa hapa tujifunze kwamba hii ni laana ya dhambi zetu nifunzo la jumla kwamba maisha yetu ni machafu yaani mwenendo wa maisha yetu hayampendezi Mungu tutafakari upya naman ya kuenenda pia kutojichangayachanganya na mataifa mengine bila mpangilio maalum
We jamaa vip, hujasoma takwimu kuwa wanaokufa wengi ni wazee wa 60+
Acha ramli potofu sijui za dhambi blah blah, milipuko inatokea na inadhibitiwa kimkakati sio kuendekeza imani zisizo na uthibitisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunaona kwa wenzetu Ulaya na Asia kwa namna ugonjwa huu unawadhuru. Tunaona kwa namna ambavyo Italy waziri mkuu analia hadharani kwa jinsi ambavyo ugonjwa huu umeshindikana kudhibitiwa hadi mrusi anasema ataenda kutoa msaada. Kwa wenzetu hili jambo tayari limeshaweka historia mpya kwao hata kama litaisha.

Kwetu sasa. Si tunasema kuwa sisi ni immune? Yaweza kuwa kweli kabisa na tukishapuuzia maisha yanaendelea huku corona akiendelea kuishi baina yetu. Tunaugua mafua na homa tunapona huku corona akiwa ndani hawezi kudhuru ila anaambukizwa kwa mtu mwingine.

Ulaya, Marekani na Asia wakishafanikiwa kuudhibiti huko kwao kitakachofuata ni kuiweka Afrika kwenye total isolation. Hatutaruhusiwa kwenda nje ya Afrika. Wanatuona tunavyoubeza huu ugonjwa. Wakati ukifika tutasaga meno hivyo ndugu zangu, nimeandika kwa uchache ile unumbe umefika. Itakuwa ni zaidi ya Apartheid. Zaidi ya Xenophobia. Tuwe makini nasi kama wananchi tushirikiane na serikali zetu ili Ulaya na Asia wakitokomeza na huku uwe umeisha


Huo ujumbe niliuweka ila Mods wakaunganisha na zingine. sasa tunachoona ni kuwa China wametoa tangazo kuwa wamezuia wageni kuingia China hadi hapo watakapoamua vingine. Hili zoezi kwa kweli litachukua muda mrefu sana hadi pale chanjo itakapopatikana kwani China haitaweza tena kuruhusu nchi yao kuingia kwenye janga kama hili. Italia na Uhispania wanalia. Kesho utasikia wamepiga marufuku ya hali ya juu kwa wazamiaji wote kwa kigezo cha corona.

Niliona katuni moja waafrika wanazuia wazungu kuingia Afrika na ikawa kama mzaha vile. sasa katazo la kutoka nje ya Afrika likianza tutapata taabu sana. Ni kwamba Afrika chini ya Sahara ndiyo itakayoathirika na hii aftermath. Waafrika wataonekana ni career wa virusi hivi na watakuwa na uwezo wa kuvisambaza tena nje ya Afrika na janga lingine linaweza kuibuka, hivyo hawatakuwa tayari hawa watu

Mwanzo walikuwa wanahoji kwa nini Afrika haijaathirika, na hakuna vifo. Walijisikia vibaya na bado wanajisikia vibaya. Pamoja na malaria, kipundupindu, ukimwi, ebola, njaa; bado hawaoni kuwa kwetu yanatosha. Walipenda tushirikiane nao kuugua hii corona. Sasa kwa kuwa inaonekana kushindikana kuugua, itawezekana kushuhudia kipindi kigumu na cha mpito kwa Afrika kuelekea kuitokomeza corona. India kuchapa viboko raia wake wanaokaidi amri ya isolation sio kama hawajui. Rwanda na Uganda hadi kutumia risasi za moto si kama hawajui. Tujifunze na tuamke sasa ili kwa pamoja tuutokomeze huu ugonjwa
Victim mentality inakusumbua sana mkuu. Usipende kuishi maisha ya kuonewa huruma
 
unajua ndugu zangu lazima tukubliane kuwa si lazima Tanzania iige marekani au italy katika kuchukua hatua kisa kuofia kutengwa!

hatua zinazochukuliwa Tanzania ni nzuri ndio maana impact ya haya maradhi hatuioni lakini pia tuzingatie ushauri tunao pewa.

kufunga makanisa,miskiti na masoko sio suluhu ni kumpa shetani nafasi wachungaji wanatwambia hivyo.

haitakiwi kushukuru maradhi kumpata mwanadamu yyte ila ndugu zangu maradhi hya yangeanzia Afirca nakwambia sasahiv vyimbo vya magahribi vingeibua ushenzi sanaaa

wazungu walifika pahala wakijiona ni miungu wa dunia wacha wapokee kichapo kidgo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah...ndiyo mnatutimua town..dah

Sent using Beretta ARX 160
 
Ndio hivyo tena, suala la corona haliepukiki kusambaa huku mjini, tunajifariji na kujaribu kunawa mkono ila ni suala la muda tu,

Nachotaka kuwashauri wazee wangu wa kuanzia miaka 60 na kuendelea warudi tu kijijini kwanza, kwa kuwa ugonjwa huu unaua wazee na watu wenye matatizo mengine kiafya, zaidi ya 95% ya vifo vyote vinaangukia kundi hili

Kijijini kule hakuna msongamano na pia unaweza kujifungia hata mwezi bila kutoka kiurahisi

Maana kikija kunuka hapa (ndani ya mwezi au miwili) hapa mjini hapatatosha na suala la lockdown kwa nchi zetu haliwezekani, so chonde chonde wazee, mjini hapawafai


Sent using Jamii Forums mobile app
Unaposema suala la lock down haliwezekani unamaanisha nini?
 
Mzee mkuu alisepa kitambo baada ya kungundua hii hali siyo kazuka pale kati kaona bado hayupo salama kaona akajisokomezi kijiji kabisa 😂😂
 
Mimi mzee (dingi) 60+ jana nilipata mafua nikapiga piga chafya na kutoa kamasi nikaanza kutafuta kusikilizia dalili, nikawa nasikiliza kama homa itapanda na haikutokea. Nimeamka vizuri tu.

Naona watu wengine wanajimwambafai eti walipata corona wakapona kama mafua vile. Mi naona ilikuwa ni mafua ya kawaida.

Kichonishangaza ni kupanda basi toka posta mpya mpaka G/la mboto alikohoa jamaa mmoja tu mara moja kwa muda wa zaidi ya saa 1na 30, foleni ilikuwa ndefu sana watu kibao wamesimama.

Watu wanaogopa kukohoa au kipiga chafya ndani ya daladala, hii imenionyesha wa TZ tunafuata masharti vizuri sana.
 
Back
Top Bottom