#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Nashauri mwaka mzima wa masomo usitishwe tutaendelea mwaka ujao ili tupigane kwanza hii vita. Mishahara tulipe tu ilimradi lengo kummaliza adui yetu mkubwa kirusi corona.
 
It
Nashauri shule na vyuo viendelee kufungwa lakini kwa upande wa vyuo vikuu, wakufunzi waanze kufundisha kwa njia ya mtandao.

Hii inawezekana hasa kwa masuala ya theory, na practical zinaweza kufanyika siku wakirejea vyuoni. Tutumie mitandao kuwafundisha kwa vile wapo majumbani.

Kwa kuanzia, kuna wawakilishi wa wanafunzi (CRs) na viongozi wa wanafunzi vyuoni, hawa wanaweza kutumiwa notes na wakufunzi kwa mtindo wa SLIDES na VIDEOS na kusambaza kwa wenzao na hivyo muhula wa masomo kuendelea kama kawaida.

Kwa wale wenye mikopo (BOOM) wanaweza kupewa nusu kwa mfano sh.250,000/= ili zingine wapewe wakirudi vyuo baada ya kusaini.

Nimeshuhudia vyuoni baadhi ya wanafunzi hawahudhurii darasani ila wanachukua slides na kujisomea na wamekuwa wakifaulu hata kuzidi wale wanaohudhuria.

Vyuo vitakapofunguliwa, wakufunzi wanaweza ku-HIGHLIGHT kile walichofundisha na baadae kutoa TEST ONE.

Ili kiepusha msongamano, usumbufu katika vituo vya mabasi, na kukosa usafiri, siku shule zikifunguliwa, wapishane kwa wiki moja. Kwa mfano, wanaweza kutangulia wa shule za msingi na sekondari na baada ya wiki moja wafuatie wa vyuo vya kati na vyuo vikuu.

Wanafunzi wa vyuo vikuu wana viherehere hasa wakati wa uchaguzi, hivyo si vyema uchaguzi ukawakuta wakiwa vyuoni.
[/QUOTE
Ushauri mzuri shule zifunguliwe baadae hali itakapotengamaa
 
Wakuu kufuatia hatua zilizochukuliwa na serikali yetu kupambana na covid 19 hakika kama ingekuwa ni janga basi Watanzania tungekwisha tupukutike!

Shughuli zingine zote zinaendelea, shule na vyuo tu ndio vimesimama, sioni ulazima wa vyuo na shule kufungwa kwa kuepuka corona kama janga kwa nchi yetu.

Corona ipo kwaajili ya wazungu huko ulaya, ni zamu yao sasa wacha iwanyooshe.
Huku Africa tunapambana na majanga yetu ya maralia, njaa, ebola na mengine mengi.
Wazungu wanataka kulazimisha janga lao liwe la dunia nzima...haiwezekani.

PM Majaliwa tunaomba usiongeze muda wa kufunga shule na vyuo, watoto warudi kusoma kuanzia tarehe 17 April
HUWATAKII MEMA WATANZANIA UNATAKA TUANGAMIE
 
Nisamehe mkuu kama nimekukwaza,bat hebu jiulize mtoto ulomzaa wewe unashindwa kumdhibiti vipi kwa mwalimu ataweza kweli kufuata maagizo yake?

Pili kumbuka kuwa wakati serikali inaamuru shule zifungwe tulikuwa na kesi moja,hivi inaingia akili kweli kufungua shule ilikhali visa vya ugonjwa vibazidi kuongeza ka?

Tatu ujue baada ya shule kufungwa kuna watoto walisafiri toka mjini kwenda vijijini na kinyume chake ,sasa huoni kuwa kurudusha watoto shuleni itapelekea kuongezeka kwa visa vya ugonjwa?

Mwisho nyumbani ndo salama zaidi kwa mtoto katika hali tuliyonayo,hivyo acheni watoto watulie majumbani hadi hapo serikali itakapotangaza vingine lakini pia acheni ujuaji serikali inawashauli wake wanaoishauli mambo yakiwa sawa hamtaona tena kama ilivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante Mkuu digba sowey. Ukweli nilifikiri hili ni jukwaa la kuelimishana. Kama kuna jambo unahisi hatujalisema kwa jicho la tafakari ya kina, njia nzuri ni kuelimishana.

Kwa sababu tusi kamwe haliwezi kuoniondelea dhana ninayoisimamia, lakini ukinipa elimu kiungwana na kwa upekee namna hii, unanipa nafasi na fursa ya kujifunza kupitia wewe kaka.

Hakika tunapaswa kuunga jitahada za serikali kwa kutoruhusu Mazoea ya likizo za nyuma yatawale katika kipindi hiki.

Ulinzi wa watoto uanzie kwetu. Corona ni hatari lakini inazuilika. Kama wazazi tuwe msitari wa mbele kuhakikisha watoto wetu nyumbani wanakuwa salama.

Zaidi pia nikutake radhi, kwa neno lolote lililokosa ustaarabu, uungwana na staha kwako.

Ahsante [emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wewe upo dar ambapo mtandao unasoma usifikirie kila mtanzania anaishi mjini, sio kila mwanafunzi wa chuo ana smart phone au laptop!!! Haraka ya Nini kwani hata wakimaliza wataongeza idadi ya wasio na ajira tu mtaani.
 
Wewe ni mpumbavu kweli
Watu kama ninyi ndio hamna uzalendo kwa kuwa hamtaki wananchi wa Tz kuwa salama
 
Tatizo La Mtandao Kutoshika Ni Kubwa Sana Sehemu Nyingi Hapa Tz Tena Hasa Kwa Smartphone Ndio Kabisa. Pia Pamoja Na Kuwa Na Jina Kubwa La Mwana Chuo Kikuu Si Wote Ni Wajuzi Katika Matumizi Ya Mtandao. Hivyo Hoja Yako Kukubalika Na Kukataliwa Yaweza Kuwa 50/50
 
Knowledge ya kusoma online Tanzania ni saw lkn haitowezekan kutokn na technology yetu
f716aa5823c54c0184d2ca37209ef3ee.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawasiwasi ugaidi ulikuwa unachochewa na nchi nyingine zenye malengo ya kuiba rasilimali za nchi ugaidi unapofanyika. Sasa mataifa makubwa yanapambana na Corona na ugaidi umesimama. Swali la kujiuliza magaidi washapata walichokitaka?

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha ujinga. Umekariri habari zije kwa kiingereza na kiswahili. Nakujulisha kuwa Msumbiji Ugaidi umetamba kwa masaa 14 .wamevamia kambi ya Jeshi,vituo vya polisi, benki na wametembea na boti za jeshi na kuua Raia wengi sana. Ndani ya huu mwezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom