#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Kwa vile tumeamua hatuwezi kuweka nchi yetu kwenye "lockdown" kutokana na watu wengi kutegemea kuendesha maisha yao kwa kufanya kazi zinazo walazimisha watoke majumbani, ni vizuri serikali ikaweka sheria ambazo zinaweza kusaidia kupunguza maambukizi ya corona.

Sheria moja ambayo napendekeza na nchi ambazo zimeshambuliwa vikali na janga hili wanaanza kutumia, ni watu wote wakitoka nje ya nyumba zao wavae masks/barakoa. Mtu ambae hatovaa mask/barakoa alipishwe faini.

Masks/barakoa sio lazima hiwe ya kutupa kila siku kwani inaweza kuleta gharama kubwa kwa wananchi; mtu anaweza kushonesha na akafua jioni. Ikiwezekana serikali igawe masks/barakoa za vitambaa bure kwa wananchi hili watu waendelee na miangaiko ya kila siku kama kawaida.

Wale ambao watapata dalili za corona yani homa kali, kukooa, na kushindwa kupumua watabaki majumbani au kwenda hospitali kama watazidiwa zaidi.

Mwenyezi Mungu aendelee kutulinda na janga hili, lakini ni muhimu nasisi tuchukue hatua za kujikinga.
Kama ulinunua barakoa ukitegemea utatuuzia,imekula kwako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WHO wamesema kwa nchi masikini 'lockdown is not practical' inabidi tutumie njia nyingine ikiwemo hii ya kuvaa barakoa muda wote.
Barakoa itahitajika kubadilishwa kila siku la sivyo itabeba virusi. je watu wataweza?
 
Unaweza kutengeneza yako ya kitambaa ukawa unafua. Au jifunge kitambaa cha kichwani kama barakoa then unafua kila siku.
 
Hilo linawezekana, nimewaza tu kama wengi watazingatia usafi kufua ama kubadilisha kila siku
 
Watu wanaogopa kufa, si unaona wanavyoosha mikono sasa hivi. Kabla ya hapo watu walikuwa wanapenga kamasi wanapangusa kwenye mti au ukuta alafu anaenda kumsalimia mwenzake.
 
USHAURI KWA SERIKALI KUU NA HALMASHAURI ZOTE NCHINI:

Naomba S/kuu na halmashauri zipitishe sheria ndogo ya dharura kwa watu wanaokaidi kunawa au wafanyabiashara ambao hawajaweka vitakasa mikono.

1.changamoto nilizoziona w/biashara wengi wameweka Ndoo lakini hawawasisitizi wateja wao kunawa mikono.

2.baadhi ya wananchi wanadharau (coz hakuna sheria ya kuwabana)

3.Ndoo nyingi na sabuni maeneo mengi vikiisha haviongezwe wanaacha hivyo hivyo.

4.wauzaji na watoa huduma mbalimbali hawana Barakoa za kujikinga na maambukizi.

5.kuna mikusanyiko ya vijana vijiweni isio na lazima.( angalau kuwe na watu wasiozidi watatu eneo moja)

6.sheria izingatie kuwabana wakaidi na kutoa onyo na elimu kwa pamoja.

7.Mwisho: utambuzi wa wageni wanaongia kwenye kitongojini kijiji,kata, wareport kwa viongozi wa vijiji na bwana afya wa kata husika( hii itasaidia hata kupata taarifa sahihi za ufuatiliaji kwa wale watakaokutwa na maambukizi .

Corona inazuilika Tuchukue tahadhari.

BY .ADUI WA CORONA TZ.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
USHAURI KWA SERIKALI KUU NA HALMASHAURI ZOTE NCHINI:

naombaS/kuu na halmashauri zipitishe sheria ndogo ya dharura kwa watu wanaokaidi kunawa au wafanyabiashara ambao hawajaweka vitakasa mikono.

1.changamoto nilizoziona w/biashara wengi wameweka Ndoo lakini hawawasisitizi wateja wao kunawa mikono.

2.baadhi ya wananchi wanadharau (coz hakuna sheria ya kuwabana)

3.Ndoo nyingi na sabuni maeneo mengi vikiisha haviongezwe wanaacha hivyo hivyo.

4.wauzaji na watoa huduma mbalimbali hawana Barakoa za kujikinga na maambukizi.

5.kuna mikusanyiko ya vijana vijiweni isio na lazima.( angalau kuwe na watu wasiozidi watatu eneo moja)

6.sheria izingatie kuwabana wakaidi na kutoa onyo na elimu kwa pamoja.

7.Mwisho: utambuzi wa wageni wanaongia kwenye kitongojini kijiji,kata, wareport kwa viongozi wa vijiji na bwana afya wa kata husika( hii itasaidia hata kupata taarifa sahihi za ufuatiliaji kwa wale watakaokutwa na maambukizi .

Corona inazuilika Tuchukue tahadhari.

BY .ADUI WA CORONA TZ.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salamu kwenu wanaJF

Hili janga la corona naona Serikali halichukulii kwa uzito unaostahili kwa sababu zifuatazo

Kushindwa kutoa vifaa muhimu Kama Mask, gloves, vipima joto n.k katika taasisi zake mbalimbali.

Hospitali nyingi na vituo vya afya vingi Sana havina hivi vifaa kwa Wafanyakazi wake achilia

Kushindwa kusimamia swala la mikusanyiko isiyokuwa ya lazima. Ukitembea sehemu nyingi Sana utaona bado vijiwe vingi vya kahawa, mabanda ya video bado watu wanajaa bila tahadhali yoyote na Serikali IPO tu, Serikali ya mtaa/ Kijiji au wilaya!!

Mfano wilaya ya Mkuranga Hali Ni mbaya Sana watu wanajaa kwenye vijiwe vya kahawa huku wakiangalia TV na mabanda ya video bado yanajaza watu tu, hii inaonyesha Serikali haiko makini ktk kukabiliana la corona

Misaada imetolewa na makampuni/ watu binafsi kuhusu kusaidia vifaa mbalimbali vya kujikinga na corona lakini mpaka Leo Hakuna tofauti yoyote mtaani kuonyesha misaada hiyo imesaidia jamii mfano mask bado Bei kubwa 2000/= , sabuni Bei juu, sanitizer bado gharama kubwa hii inatoa picha mbaya kwa Serikali pesa za Rostam Aziz 1bilion, pesa za Mwenge n.k hazijaleta msaada kbs kwa watu,

Ushauri wangu kwa Serikali naomba waonyeshe Nia na juhudi ktk kupambana na corona mfano Jiji la Dsm ndo kitovu Cha maambukizi nchi , hapo ndo itasabsbisha mikoa mingine wapate huu ugonjwa, hivyo Serikali ningethibiti mwingiliano wa watu wa Dar na mikoa mingine, wazuie usafiri wa mikoani walau kwa wiki mbili tu,

Marufuku za mikusanyiko ifanyike kwa nguvu ikibidi patrol za polisi au mgambo ili watu waepukane na maambukizi yasiyo ya lazima!!

Mwisho naomba Watanzania wenzangu tujipende sisi na wenzetu pia tuchukue tahadhari Kabla ya hatari!!

House girl(dada wa kazi) Ni binadamu aheshimiwe, apumzike, apewe Uhuru wa kuabudu pia
 
SUASO,
sawa msuaso ila watu ndio wakuchukua jitihada za makusudi kujiepusha na mikusanyiko, si mpaka nguvu itumike ya polisi. naona lockdown inapaswa endana na support toka serikalini kama vyakula,

labda tutafute lockdown ya namna yetu ila kama zile za nchi zilizoendelea, ni ngumu hasa kutokana na uwezo wa serikali yetu. umeona hapo kwa babu kaguta anapambana lisha wananchi wake ili wasijekufa kwa njaa wakiwa ndani.
 
displayname, Ni sahihi kabisa mkuu, Mimi pia sijapendekeza lockdown isipokuwa naona tunafeli Sana ktk kupambana na hili janga hasa hasa mikusanyiko isiyokuwa na muhimu, watu wafanye kila kitu kwa utaratibu na maelekezo husika!!

Watu wanapiga kawaha kijiweni na unawawekea TV hii si sawa, Watu wanaingia kucheki video bila utaratibu wowote.

Mkuu nguvu muhimu ili Mambo yaende sawa

House girl(dada wa kazi) Ni binadamu aheshimiwe, apumzike, apewe Uhuru wa kuabudu pia
 
SUASO,
ndio hapo sasa inabakia kuwa ni utashi wa mtu, mfano nilienda benki kuchukia kadi yangu lakini ndani watu ni wengi mno nikajiwazia hata kama pana victim si ni balaa.
 
ndio hapo sasa inabakia kuwa ni utashi wa mtu, mfano nilienda benki kuchukia kadi yangu lakini ndani watu ni wengi mmno nikajiwazia hata kama pana victim si ni balaa.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] Daah utashi wetu bado Sana mkuu, tukitegemea tujiendeshe kwa utashi tukakufa kuliko US, maana hata wasomi bado wanachukulia POA hili janga,

House girl(dada wa kazi) Ni binadamu aheshimiwe, apumzike, apewe Uhuru wa kuabudu pia
 
Serikali ni nani utapata jibu.
Mkuu jikinge ww utakiwa umekinga na wengine hiyo ndo serikali.
Anzia nymbani kwako utaokoa faimila ysko jirani kijiji hadi mkoa
 
Salamu kwenu wanaJF

Hili janga la corona naona Serikali halichukulii kwa uzito unaostahili kwa sababu zifuatazo

Kushindwa kutoa vifaa muhimu Kama Mask, gloves, vipima joto n.k katika taasisi zake mbalimbali.

Hospitali nyingi na vituo vya afya vingi Sana havina hivi vifaa kwa Wafanyakazi wake achilia

Kushindwa kusimamia swala la mikusanyiko isiyokuwa ya lazima. Ukitembea sehemu nyingi Sana utaona bado vijiwe vingi vya kahawa, mabanda ya video bado watu wanajaa bila tahadhali yoyote na Serikali IPO tu, Serikali ya mtaa/ Kijiji au wilaya!!

Mfano wilaya ya Mkuranga Hali Ni mbaya Sana watu wanajaa kwenye vijiwe vya kahawa huku wakiangalia TV na mabanda ya video bado yanajaza watu tu, hii inaonyesha Serikali haiko makini ktk kukabiliana la corona

Misaada imetolewa na makampuni/ watu binafsi kuhusu kusaidia vifaa mbalimbali vya kujikinga na corona lakini mpaka Leo Hakuna tofauti yoyote mtaani kuonyesha misaada hiyo imesaidia jamii mfano mask bado Bei kubwa 2000/= , sabuni Bei juu, sanitizer bado gharama kubwa hii inatoa picha mbaya kwa Serikali pesa za Rostam Aziz 1bilion, pesa za Mwenge n.k hazijaleta msaada kbs kwa watu,

Ushauri wangu kwa Serikali naomba waonyeshe Nia na juhudi ktk kupambana na corona mfano Jiji la Dsm ndo kitovu Cha maambukizi nchi , hapo ndo itasabsbisha mikoa mingine wapate huu ugonjwa, hivyo Serikali ningethibiti mwingiliano wa watu wa Dar na mikoa mingine, wazuie usafiri wa mikoani walau kwa wiki mbili tu,

Marufuku za mikusanyiko ifanyike kwa nguvu ikibidi patrol za polisi au mgambo ili watu waepukane na maambukizi yasiyo ya lazima!!

Mwisho naomba Watanzania wenzangu tujipende sisi na wenzetu pia tuchukue tahadhari Kabla ya hatari!!

House girl(dada wa kazi) Ni binadamu aheshimiwe, apumzike, apewe Uhuru wa kuabudu pia
Africa serikali hazijali sana vifo vya watu na wananchi wenyewe hawajui kuwawajibisha viongozi wao utaona October bado watu wanamshobokea jiwe.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] Daah utashi wetu bado Sana mkuu, tukitegemea tujiendeshe kwa utashi tukakufa kuliko US, maana hata wasomi bado wanachukulia POA hili janga,

House girl(dada wa kazi) Ni binadamu aheshimiwe, apumzike, apewe Uhuru wa kuabudu pia

Mkuu unachosema ni kweli kabisa. Ukijaribu kuzunguka sehemu za starehe mida ya jioni, utadhani hakuna janga lolote! Nenda supermarkets, malls, bars, benki nk watu wanajaa kama kawa na misongamano kama yote. Jana nimeenda dispensary kumpeleka mgonjwa nimeshangaa kuanzia wadada wa mapokezi, madaktari, maabara nk hakuna hata mmoja alievaa walau mask tu na watu humo ndani wanakohoa balaa.
 
1586949037788.png

1586949055061.png

1586949081883.png

Wananchi wa kawaida wana huduma ya maji safi na salama yanayotoka kwenye mabomba?

Misaada miningi ya kupamabana na corona ni madumu ya kunawia mikono. Kama tungekuwa na uhakika wa maji misaada ingekuwa sabuni za kunawia mikono.
 
Ngoja tununue ndege na kujenga SGR Kwanza. Maji ya bomba baadae sana.
 
Back
Top Bottom