Kasema kuna uwezekano wa hizo barakoa kuwa zinapandikizwa corona mbona baada ya matumizi idadi imepanda?
Ana mashaka hata na upulizaji wa madawa (fumigations) kunaweza kuwa kumetumika kupandikiza virusi na ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama vichunguze, kuna haja tena ya kupuliza madawa?
Huyo ndio Rais wetu maarufu kama Jiwe! hajaribiwi hata kidogo.
Sasa lile agizo la kutaka kuvaliwa barakoa katika ofisi za umma, mabenki na daladala halina maana kwani barakoa haziaminiki tena na kwa nini watu wavae vitu wasivyo na uhakika kama ni salama?
Hayo ya kujipulizia madawa ya kuua mende, Rostam naye akachukue mamashine yake aliyofunga. Kwanza nani kamruhusu kufunga (hata kama ni Majaliwa) mbona yeye hana taarifa huko Chato mapumzikoni?
Haya sasa kwa wale mlio sema kakaa kimya sana! Kasema sasa!
Sent using
Jamii Forums mobile app