#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Tangazo la dawa ya rungu hujawaikulisikia mikwara yake?

"Tumeamua kutangaza vita dhidi ya wadudu warukao na watambaao, pulizia kidogo tu uone jinsi itakavyo waangamiza kuanzia mende, kunguni, sismizi siafu nk"

Lakini hiyo hiyo rungu kwa kunguni inasanda
 
Hao waliokufundisha Natural Selection ya Charles Darwin ndio haohao wanakuambia uchukue tahadhari. Wewe na wao nani anajua zaidi?
+1
Asichofahamu ni kuwa hata hizo principles anazozijua nyingi zinakuwa challenged na kisayansi ya sasa .na baadhi zinaonekana kupwaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunapambana na Corona, kalipoanza ndio kalikuwa ka Corona sasa ni Corona, tuwasikilize viongozi wetu kwa kutekeleza kila maelekezo tunayopewa.
Tufuate maelekezo ya kitaalamu ya jinsi ya kujikinga lakini pia tuongezee na tiba asili na tiba mbadala.
P
Nani mkweli sasa, wanaotuambia tuchape kazi tusiogope, au wanaotuambia tusiende kwenye mikusanyiko?! Wanaotuambia tushone Barakoa za khanga au wanaotuambia hazitusaidii chochote kutukinga kwa virus vya Corona? Nimeona Tweet ya Dr.Ndugulile akisema Mapua hayastahimili joto lakini Rais kasema tujifukizie dawa za asili?
Nimeona Dr.Mabula kateuliwa kuwa katibu mkuu, nilidhani Dr.Ndugulile kastaafu au kastaafishwa kumbe bado.
 
COVID-19 ipo ndio maana tunaambiwa tuchukue thadhari.

Anatuambia tusipeane hofu kwa kuwa watu wanaukuza sana huu ugonjwa.
Watu gani wanaukuza zaidi yao, wao ndio hutupa taarifa zote nasisi tunazifuata. Kuna hofu zaidi ya KUFUNGA vyuo vyote na shule zote?

Wao ndio wanaeneza hofu, Niliuliza humu kunafaida gani kuambiwa idadi ya watu waliokufa?

Nilidhani ni kutia HOFU umma ili waelewe kwamba ugonjwa upo na unaua kweli, ili wafuate maelekezo ya wataalamu wa Afya?

Kama hiyo haikuwa sababu then nini maana ya kutpa takwimu za wagonjwa waliopo na waliokufa kwa haka ka Corona.
 
Dunia nzima, kupitia WHO, inasisitiza kuzingatia ushauri wa kitaalamu wa kujikinga dhidi ya maambukizi. Je, pale ambapo mtu anapojihisi amekwisha ambukizwa achukue hatua gani kabla ya kusombwa kupelekwa karantini?

Kuna waliopona, je, wametumia tiba gani kUpona? Je, ni siri?

Tunaomba hao hao wataalamu watushauri jinsi ya kukabiliana ba COVID-19 ukihisi umeambukizwa au una dalili za awali, ili kupunguza msongamano kwenye vituo vilivyotengwa kwa ajili ya wagonjqa wa COVID-19.
Covid19 sio Hiv Mkuu.
 
Miujiza baada ya maombi.. Wengine wamejivukiza mvuke wa mitishamba.. Hata mimi pia nimefanya hivyo

Jr[emoji769]
 
Rais kasema tuko vitani, na katuambia tuwe makini kupokea misaada, mingine ina Ma Corona humo humo, sisi tunapokea tu.

Jana niliona habari humu ikisema , Ghala vilimohifadhiwa vifaa vya kujikinga na Corona limeungua, leo tunaambiwa tusi pokee misaada hovyo, hasa hizi mask za kujikinga na maambukizi ya Corona virus.

Hii kauli na ule moto ni coincident tu au tulipanga kuunguza ghala?!

Ile misaada ilitoka China na ilitolewa na Bilionea Jack Ma, na ilipokelewa na waziri mkuu ,akiambatana na waziri wa Afya, na Balozi wang alituhakikishia misaada mingine inakuja. Je, hiyo inayokuja tutaipokea ua tumesha mwambia balozi Wang hatupokei misaada hovyo hovyo tena?

Au sasa misaada itapitia kule TFDA au kwa mkemia mkuu ikapimwe kwanza kabla haijapokelewa rasmi? Maana nasikia wanaweza kutuwekea Ka Corona humo, halafu sisi tuna vaa hayo ma mask hata hatuja yapima tukajiambukiza zaidi.

Kapokea taarifa ya vyombo vya ulinzi na usalama, na kuvishukuru. Kasisitiza tuko vitani, na kuwashauri wanasiasa wngine waache kutafuta cheap popularity kwa matamshi yao hasa wakati huu tukiwa vitani.

Tuondoe hofu, Corona itashindwa. Wamefunga shule na vyuo vyote kwa muda usiojulikana, je ni wao wanawasiwasi au ni sisi wananchi tunawasiwasi?!

Adui wetu nani hasa?! ni haka haka ka Corona au kuna mwingine?! Au ni ile ile vita ya kiuchumi inaendelea?!

Ka uzi Tayari.
Mingine ni ile ya Roast ham imepigwa vijembe vibaya mno.. Msaada unaopokelewa ni mmoja tuu.. SHEKELI

Jr[emoji769]
 
Locking down people causes stress,

naturally the body is effectively adapted to controll/mediate stress by producing cortiso hormon from the adrenal glands.

It's unfortunate that the hormon lowers immunity.
Kwahio ni hatari Kwa mtu aliekua under lock down ikitokea Ka contract Covid19.
 
Dunia nzima ma Rais wanakutana na wataalam wa Uchumi na Wahudumu wa Afya kujadili vita ya Corona

Tanzania sie tunakusanya Majeshi ya Ulinzi na Usalama kujadili Corona bila ya Wachumi wala Madaktar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna Daktar Mtanzania anaeishi Ubeberuni Uingereza alihojiwa na Salim Kikeke alipona corona, yeye alipiga Mixer, dawa na Mzungu na za kina kinjekitilengwale
Dunia nzima, kupitia WHO, inasisitiza kuzingatia ushauri wa kitaalamu wa kujikinga dhidi ya maambukizi. Je, pale ambapo mtu anapojihisi amekwisha ambukizwa achukue hatua gani kabla ya kusombwa kupelekwa karantini?

Kuna waliopona, je, wametumia tiba gani kUpona? Je, ni siri?

Tunaomba hao hao wataalamu watushauri jinsi ya kukabiliana ba COVID-19 ukihisi umeambukizwa au una dalili za awali, ili kupunguza msongamano kwenye vituo vilivyotengwa kwa ajili ya wagonjqa wa COVID-19.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilisema toka zamani kuwa kinachofanyika sasa hivi ni principals of natural selection by Darwinism kwamba the environment will create features which will tend to naturally select unfit organisms from the environment.

Carrying capacity ya nature imeelemewa kinachofanyika ss hivi ni kufagia uchafu wa mazingira na kubakia kilicho fit ndicho kinachoendeleza uhai

Wanasayansi hasa madaktari wamekosea sn kuwashauri wanasiasa Duniani kimsingi kufanya Lockdown ni kosa kubwa ambalo madaktari wa kipindi hiki watalaukia kizazi hadi kizazi

How could they suggest to lockdown 4.5billion people, ukifanya lockdown unaimmunocompromise watu yaani it is a highest level of stigmatization ever existed in the world

Watu wangetengenezewa utaratibu endelevu kwamba maisha yaende huku tukipambana pia na Corona
A form 4 evolution lesson!
 
Nimeangalia sura za wale viongozi wa ulinzi na usalama na kuona hali ya kukata tamaa na hizi confusion zinazo endelea.
Hivi na wao hawana jibu, ushauri au mapendekezo bali huwa wanaitwa tuu kusikiliza kama wanasikiliza Radio?

Sent using Jamii Forums mobile app
Chakaza
Hao wakuu wa ulinzi na usalama wanasikiliza hotuba ya Jiwe, kama vile wanasikiliza taarifa ya habari kwenye Radio?

Hapo umeua Mkuu
 
Nilisema toka zamani kuwa kinachofanyika sasa hivi ni principals of natural selection by Darwinism kwamba the environment will create features which will tend to naturally select unfit organisms from the environment.

Carrying capacity ya nature imeelemewa kinachofanyika ss hivi ni kufagia uchafu wa mazingira na kubakia kilicho fit ndicho kinachoendeleza uhai

Wanasayansi hasa madaktari wamekosea sn kuwashauri wanasiasa Duniani kimsingi kufanya Lockdown ni kosa kubwa ambalo madaktari wa kipindi hiki watalaukia kizazi hadi kizazi

How could they suggest to lockdown 4.5billion people, ukifanya lockdown unaimmunocompromise watu yaani it is a highest level of stigmatization ever existed in the world

Watu wangetengenezewa utaratibu endelevu kwamba maisha yaende huku tukipambana pia na Corona
Illusion plus Hallucination.

Seek for a psychologist.
 
Back
Top Bottom