#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Hili jambo la kujifukizia linaweza likatutoa kwenye hili janga ambalo halina kinga.

Nimejaribu kutafiti kuna watu wanakubali na kuna wengine wanakataa.. lakini wengi wanaopinga ni wale wenye viwanda vya madawa.

Ila ukweli ni kwamba ukijifukizia kikohozi na mafua vinapona kabisa..

Kwa wale wanaopenda kujisomea naomba usome kuhusu

1. EUCALYPTUS OIL STEAM
2. EUCALYPTUS LEAVES STEAM

Huu mti ambao unapatikana kwa wingi Tanzania na ni bure , umefanyiwa tafiti nyingi za kisayansi na unatumika kama source ya madawa mengi sana.

Lakini baadhi ya nchi wamekua wakitumia kutibu baadhi ya homa kama za mafua.

Naamini pendekezo la mheshimiwa Rais likipata mwongozo wa watalaam linaweza leta matokeo mazuri.

Tungeomba waziri atangaze kila mtanzania kujifukizia asubuhi na jioni kila siku kwa kuchanganya na huu mti eucalyptus.

Wenye phamarcy mtatuwia radhi kidogo, tupo vitani.
FB_IMG_1587543742998.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wenye phamarcy mtatuwia radhi kidogo, tupo vitani.View attachment 1427392

Sent using Jamii Forums mobile app
Pia unaweza jifukizia kwa kuchanganya yaani unachemsha tangawizi, limao na Vitunguu saumu kimoja una kata nusu aisee kama una vimafua sijui kwisha habari yake
 
Mkuu, Mheshimiwa Ummy Mwalimu ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Kassim Majaliwa ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa John Magufuli ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kuna tofauti kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Tanzania Bara.
 
Rais kasema tuko vitani, na katuambia tuwe makini kupokea misaada, mingine ina Ma Corona humo humo, sisi tunapokea tu.

Jana niliona habari humu ikisema , Ghala vilimohifadhiwa vifaa vya kujikinga na Corona limeungua, leo tunaambiwa tusi pokee misaada hovyo, hasa hizi mask za kujikinga na maambukizi ya Corona virus.

Hii kauli na ule moto ni coincident tu au tulipanga kuunguza ghala?!

Ile misaada ilitoka China na ilitolewa na Bilionea Jack Ma, na ilipokelewa na waziri mkuu ,akiambatana na waziri wa Afya, na Balozi wang alituhakikishia misaada mingine inakuja. Je, hiyo inayokuja tutaipokea ua tumesha mwambia balozi Wang hatupokei misaada hovyo hovyo tena?

Au sasa misaada itapitia kule TFDA au kwa mkemia mkuu ikapimwe kwanza kabla haijapokelewa rasmi? Maana nasikia wanaweza kutuwekea Ka Corona humo, halafu sisi tuna vaa hayo ma mask hata hatuja yapima tukajiambukiza zaidi.

Kapokea taarifa ya vyombo vya ulinzi na usalama, na kuvishukuru. Kasisitiza tuko vitani, na kuwashauri wanasiasa wngine waache kutafuta cheap popularity kwa matamshi yao hasa wakati huu tukiwa vitani.

Tuondoe hofu, Corona itashindwa. Wamefunga shule na vyuo vyote kwa muda usiojulikana, je ni wao wanawasiwasi au ni sisi wananchi tunawasiwasi?!

Adui wetu nani hasa?! ni haka haka ka Corona au kuna mwingine?! Au ni ile ile vita ya kiuchumi inaendelea?!

Ka uzi Tayari.
 
Nilisema toka zamani kuwa kinachofanyika sasa hivi ni principals of natural selection by Darwinism kwamba the environment will create features which will tend to naturally select unfit organisms from the environment.

Carrying capacity ya nature imeelemewa kinachofanyika ss hivi ni kufagia uchafu wa mazingira na kubakia kilicho fit ndicho kinachoendeleza uhai

Wanasayansi hasa madaktari wamekosea sn kuwashauri wanasiasa Duniani kimsingi kufanya Lockdown ni kosa kubwa ambalo madaktari wa kipindi hiki watalaukia kizazi hadi kizazi

How could they suggest to lockdown 4.5billion people, ukifanya lockdown unaimmunocompromise watu yaani it is a highest level of stigmatization ever existed in the world

Watu wangetengenezewa utaratibu endelevu kwamba maisha yaende huku tukipambana pia na Corona
 
Utaratibu uendelee kwa kuchukua tahadhari ipi?

Wangefunga mipaka wangezuia muingiliano ya wageni kutoka mataifa ambayo yameathirika kulikua na uwezekano mkubwa kutopata hili janga

Tamaa ya pesa, ndio sababu mpaka sasa corona inatutesa
 
Upo
Utaratibu uendelee kwa kuchukua tahadhari ipi?

Wangefunga mipaka wangezuia muingiliano ya wageni kutoka mataifa ambayo yameathirika kulikua na uwezekano mkubwa kutopata hili janga

Tamaa ya pesa, ndio sababu mpaka sasa inatutesa
Upo sahihi, tamaa mbaya, hata hivyo utakuja kipindi watu hawataenda kufanya shopping,
 
Ka Corona haka tunaambiwa tusikaogope, lakini tunaambiwa tuchukue tahadhali. Tunaambiwa tuvae mask, lakini pia tutumie njia za asili. Tuliambiwa tuache ubishi tuwasikilize wataalam na viongozi wetu, lakini leo tumeambiwa takwimu zingine ni za uongo, yani alizo nazo yeye ndio za kweli waliokufa/kufariki ni 10 tu. Tumeambiwa tusikaogope lakini wamefunga vyuo na mashule yote kwa muda usiojulikana. Tunapambana na nani hasa viongozi wetu au Corona?
 
Tunapambana na Corona, kalipoanza ndio kalikuwa ka Corona sasa ni Corona, tuwasikilize viongozi wetu kwa kutekeleza kila maelekezo tunayopewa.
Tufuate maelekezo ya kitaalamu ya jinsi ya kujikinga lakini pia tuongezee na tiba asili na tiba mbadala.
P
 
Back
Top Bottom