#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Kasema kuna uwezekano wa hizo barakoa kuwa zinapandikizwa corona mbona baada ya matumizi idadi imepanda?
Ana mashaka hata na upulizaji wa madawa (fumigations) kunaweza kuwa kumetumika kupandikiza virusi na ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama vichunguze, kuna haja tena ya kupuliza madawa?
Huyo ndio Rais wetu maarufu kama Jiwe! hajaribiwi hata kidogo.
Sasa lile agizo la kutaka kuvaliwa barakoa katika ofisi za umma, mabenki na daladala halina maana kwani barakoa haziaminiki tena na kwa nini watu wavae vitu wasivyo na uhakika kama ni salama?
Hayo ya kujipulizia madawa ya kuua mende, Rostam naye akachukue mamashine yake aliyofunga. Kwanza nani kamruhusu kufunga (hata kama ni Majaliwa) mbona yeye hana taarifa huko Chato mapumzikoni?
Haya sasa kwa wale mlio sema kakaa kimya sana! Kasema sasa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kasema kuna uwezekano wa hizo barakoa kuwa zinapandikizwa corona mbona baada ya matumizi idadi imepanda?
Ana mashaka hata na upulizaji wa madawa (fumigations) kunaweza kuwa kumetumika kupandikiza virusi na ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama vichunguze, kuna haja tena ya kupuliza madawa?
Huyo ndio Rais wetu maarufu kama Jiwe! hajaribiwi hata kidogo.
Sasa lile agizo la kutaka kuvaliwa barakoa katika ofisi za umma, mabenki na daladala halina maana kwani barakoa haziaminiki tena na kwa nini watu wavae vitu wasivyo na uhakika kama ni salama?
Hayo ya kujipulizia madawa ya kuua mende, Rostam naye akachukue mamashine yake aliyofunga. Kwanza nani kamruhusu kufunga (hata kama ni Majaliwa) mbona yeye hana taarifa huko Chato mapumzikoni?
Haya sasa kwa wale mlio sema kakaa kimya sana! Kasema sasa!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mie nauliza tu,Mkurugenzi wa TBS na TFDA wametumbuliwa? Hizo mask tunazinunua kwenye maduka yaliyo ndani ya Tanzania
 
Ni ukweli usio fichika kuwa utalii unachangia kiasi kikubwa sana kwenye pato la Taifa nafikiri zaidi ya 25% hivyo ni kati ya Nguzo muhimu ya ukuaji wa Uchumi wa Nchi yetu
Kwa uelewa wangu, baada ya Janga kubwa, Nchi Tajiri huanza kutadhmini kila Nchi na Hatua iliyochukua wakati wa Janga kulinda watu wake lakini pia jinsi hatua zilizochukuliwa zilisaidia Kulinda Maslahi ya Kimataifa .

Kwa suala la Ugonjwa, tutapimwa jinsi tulivyo linda watu wetu/wananchi lakini pia jinsi tulivyo linda usalama wa Raia wote wa maduniani waliopo kwetu.
Hapa na maanisha, kwa Nchi Tajiri maisha ya Mtu ni kitu ambacho hakiwezi kulinganishwa na chochote hivyo ni muhimu kuwa na matamko yenye Nguvu yakuonesha msisitizo na pengine Amri za mazuio yenye muelekeo wa Kulinda na Kujali maisha ya watu wasiambukizwe; BAADAE hawa wakubwa watakuwa na imani na sisi kuwa hata watu wao wakiwa kwetu na hata kama litatokea janga tutakuwa tupo tayari kuchukua hatua ngumu za kuwanusuru
Huu ni wakati wa kuandaa na Kutoa kauli zenye Nguvu ambazo hapo baadae zitasaidia kujitetea na kulinda/Kuinua utalii wetu kwa kasi .
kwa mtazamo wangu, ni bora kunyamaza Kimya kuliko kutoa kauli za Kejeli kwenye Janga kama hili kwani huko mwishoni ztakuwa ngumu sana kuzitolea ufafanuzi hadi tueleweke na kuaminika
 
Rais Magufuli amefanya maamuzi sahihi Mungu anatupesha na corona

Ondoa shaka
 
Wakati huu wa Vita hii ngumu na Kirusi Covid ,Mambo yanakwenda Kasi kijamii,kisiasa,kiuchumi na kiusalama.Hakika hakuna anayejua ya kesho kws mtu mmoja mmoja Wala Taifa.

Jana niliuliza swali la kizushi,kuwa Kama sanitizer zinausanitize mwili ukiwa hai..zinashindwaje kusanitize maiti,then ifungiwe kwenye jeneza watu wamuage marehemu Kama kawaida huku eakizingatia kukaa mbalimbali!?

Magreater Thinker walichsngia wengine wakanikejeli...ila kwa kuwa sisi Darasa la Saba ...greti sinkers' tumevhinganya huku na Greater Thinkers wenyewe mtuvumilie tu!

Wakati mjadala mkali ukiendelea kuhusu Wataalamu wa Afya na Wakemia kuhusu Kirusi huyu mbaya leo Kuna swali limekuja kichwani

Hivi inakuwaje Waziri ea Afya Bara,Da Ummy anajumuisha takwimu za Zanzibar anapotoa Taarifa za Korona .Wakati upande wa pili nako Kuna Waziri anafanya kazi hiyohiyo!?

Nawasilisha.
 
Dunia nzima, kupitia WHO, inasisitiza kuzingatia ushauri wa kitaalamu wa kujikinga dhidi ya maambukizi. Je, pale ambapo mtu anapojihisi amekwisha ambukizwa achukue hatua gani kabla ya kusombwa kupelekwa karantini?

Kuna waliopona, je, wametumia tiba gani kUpona? Je, ni siri?

Tunaomba hao hao wataalamu watushauri jinsi ya kukabiliana ba COVID-19 ukihisi umeambukizwa au una dalili za awali, ili kupunguza msongamano kwenye vituo vilivyotengwa kwa ajili ya wagonjqa wa COVID-19.
 
Wana jukwaa salaam!

Wakati nchi ikiwa katika tahadhari kubwa ya kupambana na vita ya CORONA kunawananchi mnaleta masihara tu unakuta mtu kavaa barakoa mdomoni pua kaiachia wazi kabisa tuache utani.
Jambo lingine mtu unanawa vizuri unapaka sanitizer unaenda kwenye usafiri wa uma umevaa shati, t-shirt, ay gauni ya mikono mifupi au kwa lugha.
nyingine kata mikono, bila hata wasiwasi mtu unakaa kwenye daladala au bajaji una kutana na mwenzio nae yupo hivo hivo sidhani kama kuna usalama tena hapo kwa msuguano wa mtu na mtu kwasababu hakuna daladala au bajaji au hata basi lenye seats zilizo wekwa kwa distance ya 1meter hiyo tunayo ambiwa na WHO
Jambo lingine simu za mikononi nazo kwa kiasi kikubwa zinabeba bakteria kwa hiyo hata huyu virus unaweza shangaa kakaa kwenye simu ni muhimu kuzisafisha.
Lastly, mavazi yetu hata kama una nguo moja ni bora ukirudi uivue uifue kesho nyoosha vaa kwa sababu tunakaa sehemu mbalimbali huwezi jua huyo virus labda kaachwa hapo tabia ya kuingia majumbani unakaa na nguo ulio zurula nayo kitandani au kwenye makochi si nzuri huwezi jua unaleta nini home, tusiwe wa bahili wa kutumia sanitizer tusafishe mpaka komeo za milango.
Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Africa, amen
Ni ushauri tu sio lazima ahsanteni nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mixa ya mchaichai mwarobaini majani ya mwembe mlonge tangawizi na limao kwa mbaaaali.
EWOpbQsWoAIs9TN.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Turuhusiwe kuvaa ma coverall/ overall makazini, tukifika nyumbani unalivua getini na kulidumbukiza kwenye maji Moto, unaji sanitize mwilini Kisha unaingia ndani, mmoja kwa moja bafuni
 
Back
Top Bottom