#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Wakati tukiwa katika vita Kali dhidi ya gonjwa hili la corona, ingekuwa busara Kubwa sana kwa serikali kuondoa gharama za malipo ya Maji kwa kila RAIA wa nchi hii,na gharama hizo zilipwe kupitia hela za misaada tunazopewa toka kwa watu mbali mbali wanaochngia kwaajili ya vita hii.

Nimelazimika kuishauri serikali kwasababu watu wengi wanashindwa kumudu kulipa bili za Maji na mwisho wake wnakatiwa Maji. Nimeona hili katika mji wa Iringa watu wanakatiwa Maji sababu hawajalipa bili.

Katika kipindi hiki ambacho watu wanasisitizwa kunawa Mara kwa Maria, watawezaje kunawa iwapo wakati mwingine wanakosa hata Maji ya kunywa? Serikali naomba ilitafakari hili kwa kina vinginevyo watu wetu wengi wataangamia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukishakufa hata ukidonolewa na mbuni hadi uishe haibadili kitu. Tatizo ni kuwa tulishazoea mfumo flani hivyo tunaona kama ni jambo la kuumiza ila ukweli ni kuwa ukisha kufa hakuna jambo lolote litakalofanywa na walio hai litakalokunufaisha wewe mfu.
 
Wakati tukiwa katika vita Kali dhidi ya gonjwa hili la corona, ingekuwa busara Kubwa sana kwa serikali kuondoa gharama za malipo ya Maji kwa kila RAIA wa nchi hii,na gharama hizo zilipwe kupitia hela za misaada tunazopewa toka kwa watu mbali mbali wanaochngia kwaajili ya vita hii.

Nimelazimika kuishauri serikali kwasababu watu wengi wanashindwa kumudu kulipa bili za Maji na mwisho wake wnakatiwa Maji. Nimeona hili katika mji wa Iringa watu wanakatiwa Maji sababu hawajalipa bili.

Katika kipindi hiki ambacho watu wanasisitizwa kunawa Mara kwa Maria, watawezaje kunawa iwapo wakati mwingine wanakosa hata Maji ya kunywa? Serikali naomba ilitafakari hili kwa kina vinginevyo watu wetu wengi wataangamia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nawakishindwa kufanya hivyo, Basi wasitishe operation kata maji na umeme pia hata Kama mtu ana Deni hivyo hivyo kwenye Mikopo Hadi hapo Hali itapotengemaa,,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania hii..kama Sukari tu 8000 pande hizi ije kuwa maji.Tena usiombe hali ikizidi kuwa tete tuyakose kabisa.Kuanzia maji mpaka umeme.
 
Hata bill za umeme ziko palepale itafikia kipindi watu watalala gizani, huku d'salaamu wenye nyumba ndo wamebanwa wasitoze kodi kwa wapangaji, ila concession za serikali na mashirika ya umma sijazisikia, labda hili la kupunguza ugumu wa maisha kwa wananchi kipindi hiki cha korona haliwahusu...
 
Wakati tukiwa katika vita Kali dhidi ya gonjwa hili la corona, ingekuwa busara Kubwa sana kwa serikali kuondoa gharama za malipo ya Maji kwa kila RAIA wa nchi hii,na gharama hizo zilipwe kupitia hela za misaada tunazopewa toka kwa watu mbali mbali wanaochngia kwaajili ya vita hii.

Nimelazimika kuishauri serikali kwasababu watu wengi wanashindwa kumudu kulipa bili za Maji na mwisho wake wnakatiwa Maji. Nimeona hili katika mji wa Iringa watu wanakatiwa Maji sababu hawajalipa bili.

Katika kipindi hiki ambacho watu wanasisitizwa kunawa Mara kwa Maria, watawezaje kunawa iwapo wakati mwingine wanakosa hata Maji ya kunywa? Serikali naomba ilitafakari hili kwa kina vinginevyo watu wetu wengi wataangamia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali gani hiyo? Labda uje na initiative ya kuchangisha pesa kwa ajiri ya SGR hapo hata Magu atatoka chato kuja kukupa support Ila anything about TZans is not a priority
 
Ndugu zangu nimeona nami nitoe mchango wangu wa mawazo nakushauri juu ya hili janga la dunia, kulingana na taarifa ya ongezeko la wagonjwa maeneo mbalimbali nchini nawashauri serikali iongeze wataalam yaani madaktari na wauguzi

Isambaze mashine zakusaidia kuvuta hewa Kila zahanati zisikosekane zakutosha, mashine zakupima Kila kata zisambazwe, na police wakishirikiana na jeshi la akiba (mgambo) kusimama kuzuia mikusanyiko isiyo yalazima ktk vyombo vya usafiri wa Umma na masokoni na vituo vya mabasi, kuamuru viwanda vyote vya nguo kutengeneza barakoa zakutosha na zisambazwe nchi nzima iwe bure serikali igharamie hili zoezi,

Pia kufuta Kodi na tozo zozote za vifaa Kama sabuni zakunawa mikono nakutoa Bei elekezi kwa ndoo za kunawia hata kwa 2000 ambayo haiwezi mshinda raia yeyote, kwani watu wanashindwa kuchukuwa tahadhari kwa sababu shughuli au upatikanaji wakipato kwa Sasa umepungua,

Sikwamba watu hawapendi kuvaa hizo barakoa Ila uwezo wakumudu ndio tatizo zio watu hawapendi kununua sabuni hizo majumbani Bali uwezo ndio tatizo, na mwisho Yale magari ya Police ya maji washa yatumike kubyunyiza madawa mitaani Kama inafaa,

Haya nimaoni yangu nakushauri,,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazo jema Kama wakilifanyia kazi inaweza saidia.. tunahimizwa kunawa mikono kila wakati kwa maji tililika wakati ndoo ya maji inauzwa 500 mnyonge gani atakaeweza kumdu gharama hizo... Kwasasa tunasaidiwa na maji ya mvua ila zikikata mambo yatakuwa magumu
 
Hii corona wewe acha tu, wengine wanafungua mfuniko wa ndoo wananawa wanawaachia mserebuke na maji tiririka.
 
Wakuu A. alleikhum,

Tuendelee kuchukua tahadhari ya gonjwa hili wakati tukiwa majumbani na hata kwenye mizunguko yetu ya kutafuta riziki, tunawe mikono kwa maji tiririka na sabuni/vitakasa mikono, tuvae barakoa kama ilivyoshauriwa na wataalam, tupunguze safari zisizo za lazima,tusikilize wataalam wa afya na kufuata maelekezo yao. Tusichukulie POA hata kidogo gonjwa lipo mtaani.

Nitoe rai kwa vyama vya siasa viache kutumia janga hili kama kivuli cha kupiga siasa,michango ya fedha na vifaa vitolewe kwa mamlaka husika ili kuvigawa/sambaza tena kwa maoni yangu visiwe na nembo/maandishi yoyote ya chama husika, tunapoteza focus na umoja katika kupambana na adui 'Covid-19' ambae hachagui wa kumdhuru. So sad.

Watanzania tunapaswa kujua kila jambo huwa na muda wake,kwa sasa tuzike itikadi zetu tupambane na janga lililo mbele yetu, Umoja ni Nguvu.

Niishie hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama vile alivyoondolewa Dr Possy Bungeni, Bulembo anaweza kuwekwa pembeni katika nyakati hizi za majeruhi na nafasi yake kuchukuliwa na Paul Makonda ili aongoze mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid 19.

Ni ushauri tu mapovu hayasaidii labda uoshee mikono yako.

Maendeleo hayana vyama!
 
MKUU NINGEPENDA KUJUA UMETUMIA VIGEZO GANI KATIKA HAYO UYASEMAYO
 
Ndugu zangu wapendwa,

Kwanza tupeane pole kwa janga hili linalotukabili kwa sasa.

Nimekuja kwenu naomba msaada wa ushauri. Mimi ni mtumishi wa umma. Tangu mwaka 2018 nilipanga nipambane kutafuta vijisenti ili mwaka huu mwezi wa tano nianze kujenga kabanda kangu kakuishi. Nimezichanga weee nina kama milioni 9, kiwanja ninacho na tofali ninazo sasa najiuliza weee majibu sipati.

Janga la corona linanichanganya, niko mkoa wa Njombe. Najiuliza kama corona ikaendelea kwa muda mrefu serikali ikayumba kiuchumi watumishi tukapata lidandasi (kuachishwa kazi) na hela hiyo nikawa nimeshapeleka kwenye ujenzi yote hii familia nitaiendesha vipi?

Nianze ujenzi au nisubiri corona ipite? Nimechanganyikiwa.

Ushauri wenu great thinkers.
Kodi kwa mwezi unalipa kiasi gani? Na hiyo 9M inayosha kumaliza kabisa ujenzi?
 
Jamii yoyote iliyostaarabika mi lazima iwalinde wazee au senior citizens wao. Kwa sababu kwenye wazee ndio tunapata uzoefu na busara (with age comes wisdom and experience) ingawa sometimes age comes alone.

Wazee ni watu wenye umri mkubwa na mara nyingi kibinadamu umri mkubwa unaambatana na magonjwa mengi. Ndio maana wizara ya afya na who wanasisitiza kua tuwalinde wazee wetu kwa sababu wako susceptible na magonjwa kwa sababu wengi hua wanasumbuliwa na magonjwa mengine (other underlying medical conditions).

Rais wetu ni mzee, ana umri wa zaidi ya miaka 55, hivyo yeye na wazee wengine ndio prime suspect wa corona. Lakini pia Rais yeye ndie raia namba moja na lazima ahakikishiwe usalama wa afya yake kwa gharama yoyote. Hii ni jukumu la kwanza la kitengo maalum cha ulinzi wa rais, kuhakikisha wanafanya threat analysis zote zikiwemo za kisiasa na za kiafya za rais na kuhakikisha mzee anakua salama, kumuondoa eneo ambalo sio salama na kumficha eneo lenye usalama.

Sasa, kuna watu wanataka rais aje au arudi Dar kutokea Chato, kiusalama Dar sio salama kwa afya ya rais kwa sasa kwa sababu zilizowazi kabisa.

Tumuache Rais apumzike Chato. Hoja ya kumtaka kurudi Dar haina mashiko.
 
Sasa, kama anaumwa visukari siaseme, tu hili watu tujuwe mbona kikwete alikatwa korodani hila watu, walifahamishwa.
 
Back
Top Bottom