#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Sasa, kama anaumwa visukari siaseme , tu hili watu tujuwe mbona kikwete alikatwa korodani hila watu ,walifahamishwa.
Nje ya mada, naona matumizi ya herufi "i" na "h" yanawatatiza watu wengi sana siku za hivi karibuni. Ingawa wengine wanaweza kupuuzia lakini hilo sio jambo la kupuuzia kwa kuwa inaleta kosa la kimantiki, neno "ila" na neno "hila" yana maana tofauti kabisa.
 
Nje ya mada wewe untoka mataga party?
 
Kwahiyo unakiri kabisa kakimbia ikulu kukwepa Corona huku akituaminisha Korona ni kaugonjwa kadogo tupige kazi kama kawaida!
 
Jamii yoyote iliyostaarabika mi lazima iwalinde wazee au senior citizens wao. Kwa sababu kwenye wazee ndio tunapata uzoefu na busara (with age comes wisdom and experience) ingawa sometimes age comes alone.

Wazee ni watu wenye umri mkubwa na mara nyingi kibinadamu umri mkubwa unaambatana na magonjwa mengi. Ndio maana wizara ya afya na who wanasisitiza kua tuwalinde wazee wetu kwa sababu wako susceptible na magonjwa kwa sababu wengi hua wanasumbuliwa na magonjwa mengine (other underlying medical conditions).

Rais wetu ni mzee, ana umri wa zaidi ya miaka 55, hivyo yeye na wazee wengine ndio prime suspect wa corona. Lakini pia Rais yeye ndie raia namba moja na lazima ahakikishiwe usalama wa afya yake kwa gharama yoyote. Hii ni jukumu la kwanza la kitengo maalum cha ulinzi wa rais, kuhakikisha wanafanya threat analysis zote zikiwemo za kisiasa na za kiafya za rais na kuhakikisha mzee anakua salama, kumuondoa eneo ambalo sio salama na kumficha eneo lenye usalama.

Sasa, kuna watu wanataka rais aje au arudi Dar kutokea Chato, kiusalama Dar sio salama kwa afya ya rais kwa sasa kwa sababu zilizowazi kabisa.

Tumuache Rais apumzike Chato. Hoja ya kumtaka kurudi Dar haina mashiko.
Mkuu sasa kwa nini umebadilisha avatar Picha yako ya ffu?
 
Museven aliyeko mstari wa mbele na Trump nadhani wote ni under 18.By the way kwani ikulu hakuna maji tiririka na sabuni?
 
Yule aliyekantini jijini chattle hastahili ulinzi corona ifanye inaloweza asitumikie round ya pili
 
kwa Platoon inayomlinda Toyota corona haiwezi kupenya

kikosi chake cha ulinzi kimekamilika kama Barcelona ya Messi chini ya kocha katili Guardiola

..na alishasemaga tusitishane

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari ndugu wadau. Mimi naomba kuliongelea Gonjwa la CORONA kwa namna tofauti kidogo.

Katika hali ya kawaida dunia nzima ime kubari kuwa Civd2019 haina tiba, lakini pamoja na hayo kuna watu kadhaa wanalipotiwa kupona . Watu kadhaa walobahatika kupona wanaelezea baadhi ya vitu walivyotumia wanavyoamini ni chanzo na sababu ya kupona kwao ambavyo kwa kiasi kikubwa nathubutu kusema ni kama tiba asilia . Lakini chakushangaza ambacho ndo kimenifanya niandike Uzi huu ni kuwa watu wengi hasa wa Tanzania tumejikuta tukitumia nguvu kubwa kulumbana,kunyosheana vidole na kulaumiana sisi kwa sisi zaidi kuliko kutafuta suluhisho.

Binafsi nahisi tunakuwa wavivu wakufikilia mana sijasikia mtu alie umiza kichwa akafikilia juu ya tiba japo kwa hatua ya kwanza , mfano kwenye magonjwa kama Nguvu za kiume,Saratani,Homa ya Inni, Ukoma na hata UKIMWI ni magonjwa tunayoamini tiba yake ni ngumu lakini watu wamejaribu kutafuta suluhisho m'badala japo zingine hazijathibitishwa na mamlaka husika lakini nawapongeza japo kwa jitihada hizo.

Mimi nawaombeni watanzania wenzangu kuanzia sasa Nguvu tunazozitumia kwenye Tahadhali , kuilaumu selekali na kunyosheana vidole basi tuumize vichwa na kufanya tafiti mbambali za mimea asili na kwa uwezo wa MUNGU huenda wakapatikana hata watu wawili watatu wanaoweza gundua japo dawa yakupunguza makali .waswahili wanasema "penye nia pana njia" Natoa wito kwa wale ndugu zetu wa tiba asilia na tiba m'badala huwa mnajinadi kwa matangazo kuwa mna dawa zenu zinazotibu magonjwa karibuni yote yanayotibika na yasiyotibika hosptal ,hebu umizeni vichwa mtafute na dawa ya hii.

Kama kuna yeyote aliyewahi fanya tafiti namuomba atuhusishe angalau tuchangiane mawazo kwa pale alipoishia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiongozi ni mtu wa kwanza kuonyesha njia kwa wale anaowaongoza.Wakati huu ambapo taifa letu na dunia nzima kwa ujumla wake inakabiliwa na janga la COVID- 19 ni muhimu kwa viongozi wetu wa kitaifa, mikoa, wilaya, tarafa kata na vijiji na hata vitongoji kutoa uongozi kwa watu wanao waongoza.

Ndugu zangu Great thinkers wa Jukwaa hili, naomba nikumbushe jambo moja nalo ni kuwa " janga la "CORONA" ni collective accountability directly. CORONA siyo kama HIV/AIDS ambayo ni Individual accountability.

Nitafafanua kidogo Mtu mmoja asipowajibika vizuri kwenye jamii yetu au familia na akaambukizwa COVID-19.Madhara yake yataonekana moja kwa moja kwa kuwaambukiza watu wengine kwenye jamii au familia ndiyo maana nasema jamii yetu inawajibika kwa pamoja kujilinda na hili janga kwani mmoja akilipata lina nafasi sawa ya kuwapata watu wengine moja kwa moja.Tofauti na HIV /AIDS mtu asipo wajibika kujilinda mwenyewe na akaambukizwa HIV/AIDS basi wengine hawata ambukizwa na maambukizi ikiwa watajilinda isipokuwa madhara yatakuwepo lakini siyo ya moja kwa moja.

Hivyo ninatoa rai kwa viongozi wote kuonyesha uongozi kwa kutoa miongozo kulingana na wataalamu wa Afya kisha kutoa ulinzi wa hiyo miongozo, kwani miongozo bila kulindwa haiwezi kutekelezwa kwani binadamu daima ni mvivu na asiyependa kufuata sheria na taratibu.Refer theory X and Y.

"COVID- 19 is dangerous stay at home to safe guide yourself and those whom you love"
 
Serikali ya JMT na SMZ zote kwa ujumla wangeanza kutuangalia sisi wazee/katika janga hill la corona.

Maana sisi ndio tuko kwenye hatari zaidi, wengine tuna betri + kisukari+Bp .

Pia hata immunity zetu ziko chini ukicompare na vijana.

Sisi hili Taifa la Asali na maziwa, tumeshiliki kulijenga at the great extent

Serikali mtuhurumie wazee.
Nyie Wazee mmeshakula chumvi nyingi sana...wacha Corona naye afanye yake!! Hasa nyie wazee wa darisalama mnajifanyaga kimbelemble saana na miguo yenu ya kijani...haya moto huo....dadadeki
 
Wakati tukiwa katika vita Kali dhidi ya gonjwa hili la corona, ingekuwa busara Kubwa sana kwa serikali kuondoa gharama za malipo ya Maji kwa kila RAIA wa nchi hii,na gharama hizo zilipwe kupitia hela za misaada tunazopewa toka kwa watu mbali mbali wanaochngia kwaajili ya vita hii.
HILI NI OMBI LENYE KUTILIWA MSISITIZO NA KILA MZALENDO.

HASA HASA UKITILIA MAANANI MANENO MAZURI YA MUHESHIMIWA RAIS ALIYOYATOA LEO CHATO.

KWA KWELI AMEONGEA KIZALENDO SANA, TUNAMUOMBA AANGALIE NA MAOMBI KAMA HAYA KUHUSU GHARAMA ZA MAJI KTK KIPINDI HIKI CHA MARADHI YA COVID-19
 
Hiyo ni slogan iliyutumika miaka iliyopita kuwaasa watu kuhusu ukimwi,kipindi hichi inatakiwa itumike kiukweli.wakuu tuache masikhara tuweke team CCM na Chadema pembeni. Tufate maelekezo ya wataalam wa afya.

Iko HV mpotezee usiyempenda kisiasa,angalia afya yako na familia yako.we still need your support on this forum. Kikubwa epuka safari zisizo na tija.Thank me later.
 
mkuu umeongea bonge la point naamini siku yakiisha watakaofukua hii post wataona ni namna gani kulikuwa na watu wenye mawazo mazuri kwa jamii yao
 
Wakuu habari zenu ,dunia kwa sasa inaendelea kupambana na janga la corona -Covid19 kwa hapa tanzania ukizunguka mitaani kuna kundi la watu bado wana vuta sigara hadharani tena bila wasiwasi..sasa ikiwa ugonjwa una shambulia mapafu na ikatokea mtu ana corona akauacha moshi hewani badaa ya kuutoa kwenye mapafu unakaa hewani na mtu anaweza kuvuta tena hata ukiwa umbali wa mita nne (kwa mujibu wa utafiti wangu)
Tuwe ke utaratibu mzuri au itolewe kauli kuhusiana na hili
 
Back
Top Bottom