Rais kasema tuko vitani, na katuambia tuwe makini kupokea misaada, mingine ina Ma Corona humo humo, sisi tunapokea tu.
Jana niliona habari humu ikisema , Ghala vilimohifadhiwa vifaa vya kujikinga na Corona limeungua, leo tunaambiwa tusi pokee misaada hovyo, hasa hizi mask za kujikinga na maambukizi ya Corona virus.
Hii kauli na ule moto ni coincident tu au tulipanga kuunguza ghala?!
Ile misaada ilitoka China na ilitolewa na Bilionea Jack Ma, na ilipokelewa na waziri mkuu ,akiambatana na waziri wa Afya, na Balozi wang alituhakikishia misaada mingine inakuja. Je, hiyo inayokuja tutaipokea ua tumesha mwambia balozi Wang hatupokei misaada hovyo hovyo tena?
Au sasa misaada itapitia kule TFDA au kwa mkemia mkuu ikapimwe kwanza kabla haijapokelewa rasmi? Maana nasikia wanaweza kutuwekea Ka Corona humo, halafu sisi tuna vaa hayo ma mask hata hatuja yapima tukajiambukiza zaidi.
Kapokea taarifa ya vyombo vya ulinzi na usalama, na kuvishukuru. Kasisitiza tuko vitani, na kuwashauri wanasiasa wngine waache kutafuta cheap popularity kwa matamshi yao hasa wakati huu tukiwa vitani.
Tuondoe hofu, Corona itashindwa. Wamefunga shule na vyuo vyote kwa muda usiojulikana, je ni wao wanawasiwasi au ni sisi wananchi tunawasiwasi?!
Adui wetu nani hasa?! ni haka haka ka Corona au kuna mwingine?! Au ni ile ile vita ya kiuchumi inaendelea?!
Ka uzi Tayari.