#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Hivi mama samia suluhu yuko wapi? Tunajua boss wake yuko kuleee!!
Mkuu, Mheshimiwa Ummy Mwalimu ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Kassim Majaliwa ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa John Magufuli ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kuna tofauti kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Tanzania Bara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati huu wa Vita hii ngumu na Kirusi Covid ,Mambo yanakwenda Kasi kijamii,kisiasa,kiuchumi na kiusalama.Hakika hakuna anayejua ya kesho kws mtu mmoja mmoja Wala Taifa.
Jana niliuliza swali la kizushi,kuwa Kama sanitizer zinausanitize mwili ukiwa hai..zinashindwaje kusanitize maiti,then ifungiwe kwenye jeneza watu wamuage marehemu Kama kawaida huku eakizingatia kukaa mbalimbali!?
Magreater Thinker walichsngia wengine wakanikejeli...ila kwa kuwa sisi Darasa la Saba ...greti sinkers' tumevhinganya huku na Greater Thinkers wenyewe mtuvumilie tu!
Wakati mjadala mkali ukiendelea kuhusu Wataalamu wa Afya na Wakemia kuhusu Kirusi huyu mbaya leo Kuna swali limekuja kichwani...Hivi inakuwaje Waziri ea Afya Bara,Da Ummy anajumuisha takwimu za Zanzibar anapotoa Taarifa za Korona .Wakati upande wa pili nako Kuna Waziri anafanya kazi hiyohiyo!?
Nawasilisha.
Jibu la swali lako la mwisho utajibiwa ukiweza kuona jina la Zanzibar kwenye list ya dunia Coronavirus Update (Live): 2,638,852 Cases and 184,248 Deaths from COVID-19 Virus Pandemic - Worldometer

Kuhusu SANITIZER, tunatumia kufutia mikono ili kuua virusi vilivyopo kwenye mkono na siyo vilivyopo ndani ya mwili
 
Ummi Mwalimu ni wazir wa Afya wa Tanganyika ZANZIBAR ni Nchi huru iliyojitawala na kuwa na kiti UN
Suala la Afya SI suala la Muungano Tanganyika wana uchu wa kuitawala ZANZIBAR kimabavu kambo ambalo hamyafanikiwa
Watanganyika ni wavamuzi tuu kama Muengereza alivyotuvamia
ZANZIBAR ina Rais
ZANZIBAR ina katiba
ZANZIBAR ina Mahaka
ZANZIBAR ina Wimbo wa Taifa

Muungano huu ni Muungano wa KIHUNI
Watanganyika siku zote wanatutukana na kuikejeli ZANZIBAR na sisi tunapo jitetea au kuunyoshea kidole udhalimu wao basi tunaozea Magerezani
WATANGANYUKA NI WAKOLONI WEUSI ambao ni wabaya mara 1000000000000
Kiliko wakolon wa kireno kuliko wakoloni wa kijerumani kuliko wakoloni wa kiengereza


Sent using Jamii Forums mobile app
Na nyie si mmeng'ang'ania CCM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ummy Mwalimu anatoa takwimu za nchi nzima (Zanzibar inclusive).....pia United Nation organasition (WHO) wanataka takwimu za nchi, na mwenye mamlaka ya kutangaza na kuwatumia takwimu za nchi ni Mh. Ummy Mwalimu ova!
 
Umoja wa Mataifa hakuna inchi inayoitwa Zanzibar, hivyo Zanzibar ni sawa na Rukwa,Njombe ama mtwara.

Huyo Rais wenu mamlaka yake mwisho Kibanda Maiti, akivuka Bara anatambulika kama Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Taifa Philip Mangula tu...

Ndio maana hata kwenye Baraza la Mawaziri la Jamhuri hata asipohudhuria mwaka mzima hakuna shida, ila kwenye kikao Cha CCM Taifa asipohudhuria kimoja tu lazima awe na maelezo ya kutosheleza.
 
Naam wanajamvi, mmesikia? Kuwa zile machine ni upumbavu mtupu? Naam, siyo kuwa hazifai ila kuna mahali zimeingilia masilahi ya kisiasa.

Tunaenda kwenye uchaguzi halafu mtu awe maarufu kuliko Mimi? Haiwezekani! It is all about popularity. Nyakati hizi yafaa kuwa makini sana. Ukileta kitu chenye manufaa sana kwa jamii ni bora useme kwa hisani ya JIWE! Wewe umetumwa tu.

Hata Ummy ajipange upya! Anaonekana kwenye TV kila uchao halafu hamsifii aliye pumzika Chato. Popularity ya kumzidi.....haiwezekani.

Yangu macho! Sina nilicho jifunza Jana ila tumebugi meeeni !! 2020 for ...
 
Rais wetu Magufuli ni slow learner, uelewa wake uko taratibu mno na washauri wake ni waoga kupitiliza yaani hawawezi fungua midomo yao kumshauri rais kitu kuhusu corona, wao kila kitu anachosema rais wanashangilia na kupiga makofi ya pongezi

Mtakumbuka, hapo awali rais alibisha kwamba huu ugonjwa ni "kakoloona kagonjwa kadogo tu" hawezi kuzuia watu watoke nje

Watu wameendelea kupukutika, wanazikwa na serikali kimya kimya ndio rais ubongo wake umeshituka kidogo kwa kuanza kutoa njia za kutibu covid19 eti ni kujivukisha na mvuke... Hii imemuingia na kumstua kwamba corona ipo

Next time mpaka aje afikirie kwamba corona ni hatari na suluhisho ni lockdown watanzania tutakuwa tumekwisha! Corona inatutafuna kwa kasi
Rais ametoa mawazo yake.Jukumu la kujilinda ni lako.Hujapangiwa jinsi ya kijilinda nyumbani kwako.Wewe sikiliza na chuja.Kinachofaa kichukue kisichofaa kiache ila usivunje sharia na tararibu za afya na za nchi kwa ujumla.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wazanzibar wengi wanaouchukia muungano ni masalia ya waarabu coz muungano wa tanganyika na zanzibar ulikua na lengo la kudumisha udugu wetu wa kiasilia, coz 80% ya wazanzibar ni wabara walochukuliwa nyakati za utumwa.
mm siku zote husema bangi Tanzania bora iruhusiwe maana wavutaji ni wengi hivi wewe kwa bangi zako mbona hutetei Kenya wakati ni ndugu zetu hasa Kenya kuna wamasai na Tanzania kunawamasai msumbiji kuna wamakonde na Tanzania kuna wamakonde, Uganda kuna wahaya na Tanzania kuna wahaya sijuwi Malawi pia Tanzania wapo sasa huo ubwege wako umeona ni Zanzibar tu
 
Wakuu jana tumemsikia mheshimiwa Rais wakati akizungumza na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kule nyumbani kwake Chato kuwa, wizara ya afya itoe takwimu sahihi za idadi ya watu wanaopona ili kuwatolea watu taharuki. Kwa mjibu wa Mh Rais idadi ya waliopona ni zaidi ya watu 100 ilihali wizara ya afya bado inautangazia umma ya kuwa waliopona ni 11 tu.

Wakuu ikumbukwe kuwa mlipuko huu ulizikumba kwa wakati mmoja nchi za ukanda wa Africa mashariki lakini mpaka Jana idadi ya waliopona Kenya walikuwa watu 85, Uganda 51 na Rwanda zaidi ya 100 huku Tanzania waliopona wakiwa ni wachache zaidi miongoni mwa majirani zetu.

Sasa basi wizara itoe data sahihi kama alivyopendekeza Mh Rais, lakini pia wizara ihakikishe inazuia aina yoyote ya tarifa inayoweza kuzua Taharuki , miongoni mwa taarifa hizo kama ile ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam akisema Kuwa watu wanapukutika hii si Sawa.. .

Wakuu tuchapeni kazi huku tukifaata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wetu .
 
Back
Top Bottom