Kwanza walianza na imani kuwa sisi waafrika corona haiwezi kutudhuru.Waliposikia na hatimae kushuhudia vifo,wakaja na maelezo mengine.
Kwamba wazee na wenye kinga dhaifu hasa wenye pressure,kisukari na magonjwa ya moyo ndio watakufa.
Nahisi huenda wameona kuna watu hawa kuwa na magonjwa hayo wameugua na huenda kupoteza maisha.Wengi kama sio sote tumeshuhudia vijana hawakuachwa katika janga hili.Sasa wamekuja na jambo jingine.
Kwamba watu wanene tu ndio wanakufa na corona.Kwa hiyo nawaona watanzania wenye milli midogo wakijiachia kwenye party,vijiweni wakicheza pool table na kunywa kahawa,na kila aina ya shughuli.
Ila ikitokea mtu amekufa,kuna watu wanatoa kashfa na matusi sana kwa watu wanene kwamba hawasikii acha wafe!
Kwa kweli hakuna asiyependa kuishi,ila kumekuwa na tabia ya kujaribu kuingiza hofu kwa makundi ya watu na huku mkijitoa kuwa ninyi hamhusiki na ugonjwa huu na hivyo kuwa na sababu ya kujiachia.
Tumeona ugonjwa huu ambao hata kwa watu waliokuwa wakitumia muda wao mwingi kusali mfano Italia,wamekufa na ugonjwa huu.Tumeona misikiti Saudia imefungwa kwa hofu ya ugonjwa huu.Kwa nini sie watanzania kila siku kutafuta sababu ya kukwepa wajibu wetu?
Mimi nawaomba muwe makini,mchukue tahadhari zote,na hata suala la kujifukuza sio rahisi tu kama ambavyo wengine wanachukulia. Mvuke unaweza kuua.Iwapo utajifukiza maji yakiwa ya moto sana na mvuke mwingi,unaweza kuunguza mapafu.Mwili wa binadamu hauwezi kuhimili joto linalofikia jotoridi nyuzi 100.Niko tayari kukosolewa.
Tuwasikilize wataalamu na tuombe Mungu atunusuru na janga hili
Sent using
Jamii Forums mobile app