#COVID19 Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
Habari wakuu

Dunia nzima imesimama na uchumi wa dunia unashuka kwa kasi sana kisa huu ugonjwa wa corona,maajabu yake sasa

Mtu anaweza kuwa haoneshi dalili zozote, hakohoi, hana homa kali, kifua hakibani, joto lake la kawaida lakini anakutwa positive, na anauwezekano wa kipona mwenyewe bila hata kutumia dawa,huu ni uhuni na itakuja kujulikana

Vipimo vinavyotumika kupima hawa wagonjwa mimi binafsi nina wasiwasi navyo sana, vinamkanganyiko kiufupi havieleweki,kama umeshatuliza kichwa vizur unaweza kugundua ,nadhani hadi jpm alishaanza kugundua ujanja ujanja wa hizi mambo ,hana wasiwasi kabisa

Mataifa ugonjwa ulipo anzia wameshaanza shughuli zao za kila siku, na saizi inaonekana ni ugonjwa wa kawida tu .

Kujifungua ndani ni upuuzi ambao utakuja kujulikana badae, kuchukua tahadhari kama yalivomagonjwa mengine ni muhimu zaidi

Mwisho kabisa, shule, vyuo na mambo mengine lazima yataendelea na corona itakuwepo ,watu wataiishi

JPM anaona mbali sana, Muda si mrefu hata shule, vyuo, na viwanjani shughuli zinaenda kuanza

Na huo ndio utakuwa mwisho wa corona Tz

Kablayaoctobarlazimamshindiwacoromaatakuwaamepatikana

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli ni Musa Anatupeleka Nchi ya ahadi

Waache wale chama cha kulalamika waendelee kujifungia
 
Kumeanza mabishano kuhusu jinsi CORONA miongoni mwa wanasiasa. Upimaji wa CORONA ni suala la kisayansi lakini kuweka sera jinsi CORONA inavyopimwa ni suala la kisiasa.

Ni vizuri sana wanasiasa wetu wakawauliza wanasayansi wetu ili wawe na uelewa na jinsi CORONA inavyofanya kazi na jinsi COVID - 19 ilivyo na inavyofanya kazi. Hapa chini nimeweka Video jinsi CORONA inavyopimwa.



Mjadala uwe wa kisayansi na si kwa manufaa ya kisiasa.
 
Test kits tunazotumia kupimia Corona ni zile tulizopewa na Jack Ma ambazo zimelalamikiwa nchi nyingi. Sisi kwa kuwa hatupo serious basi tunaenda nalo ilimradi tuu. Kila cha bure na cha bei rahisi kukabiliana na Covid 19 tunakipapatikia. Now tunaikimbilia dawa kutoka Madagascar, dawa ambayo haijawa approved na WHO. Huoni kama nchi tuna tatizo?

Ni lazima tuelewe kuwa Corona imeenea sana Tanzania kwa sasa. Hilo halina ubishi. Ushahidi mkubwa ni vifo vya holela holela vinavyotokea. Ingekuwa vinatangazwa tuu kwenye mitandao bila ushahidi basi Rais angekuwa na haki ya kulaumu ila vinaonekana na hata yeye vimemgusa kweli kwa watu wake wa karibu kuondoka.

Ushahidi mwingine ni raia wanaotoka nchini kuthibitishwa kuwa wana COVID 19 huko kwa wenzetu. Tena marafiki zetu.

Kosa kubwa tunalofanya kama nchi linaanzia kwa Rais mwenyewe. Kupuuza, kudharau huu ugonjwa na sasa kuja na excuses ambazo anataka kuzitumia kuficha udhaifu wake aliofanya na kuzembea kwa makusudi kulikabili janga hili. Hilo halikubaliki. Lazima Rais awajibike. Na mbaya zaidi anavyozidi kuongea anaionyesha dunia namna alivyozembea kukabiliana na gonjwa hili.

Tungewekeza vizuri kwenye kupambana na huu ugonjwa madhara yanayoonekana sasa yangepungua kwa kiasi kikubwa. Mambo hadi ya kutoa vitisho kwa vyombo vya habari vya BBC eti wanaitangaza sana Tanzania kuhusu Corona ni udhaifu mwingine. Kuwa umefanikiwa kudhibiti vyombo vya habari vya ndani ila bado huko nje unasumbuliwa.

Ni lazima vyombo vya kimataifa na hasa WHO wachukue jukumu la kuwaangalia watanzania maana kuna kila dalili Rais hataki kujisumbua kukabiliana na huu ugonjwa kwa njia ngumu zaidi. Vifo vipo, maambukizi yanakuwa kila uchwao. Tuache excuses zisizo na maana. Uhai una thamani kuliko kitu chochote kile. Eti posho! Jamani watu waende wakafe tuu kisa posho? Posho kweli? Ah ndugu Rais tafadhali bwana!
 
cha muhimu alichoona ni posho tu

nasikitika sana
bendera tuigeuze juu chini tu
 
Watanzania ni watu ambao wao kila jambo ni kulaumu tu hata kama hawajuin undani na ukweli wa jambo lenyewe.

Rais JPM aliwaita wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na kukutana nao akiwa huko mkoani Geita. Katika kikao hicho alizumgunza na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama na moja ya maagizo aliyoyatoa ni pamoja na kuangalia usalama wa vifaa vilivyoletwa kama msaada ili kuhakikisha kama vina ubora au madhara kwa wananchi.

Pia aliagiza kuchunguza nani aliruhusu kufanya fogging katika miji yetu kma vile watu wanaua mbu au viroboto. Na akatoa maagizo kuwa maabara ya taifa inayofanya vipimo ifanyiwe uchunguzi namna inavyofanya upimaji juu ya sampuli za watu wanaohisiwa kuwa na maabukizi ya Coronavirus.

Uchunguzi umefanyika na kwa mtego walioufanya wale waliotumwa kufanya kazi imeonyesha ni namna gani vyombo vya ulinzi na usalama vya taifa letu vipo makini. Mfano kama sampuli zilizochukuliwa kwenye papai lilipewa jina Elizabeth zilileta majibu positve hii kweli inatia mashaka.

Maana yake nini? Hivi vifaa vinavyotumika kupimia havina viwango au viko programmed kutoa majibu? Mask alizogawa Jack Ma na mwenzake hazina viwango?

Hivyo Watanzania tusiwe watu wa kulaumu tu eti kisa rais amekutana na wakuu wa vyombo vya usalama basi sio suluhu ya suala linalohusu afya. Tusiwe watu wa kulaumu tu kila wakati.
 
Hivi hizo sampuli za binadamu na papai zinafana?

Maana mimi nilijua sampuli zinazopelekwa kwenye vipimo ni damu!!!
 
Mkurungenzi mkuu wa maabara ya Taifa mara baada ya hutuba ya Rais hivi leo!
africansafaris_B_iSBULpOZZ.jpg
 
Hivi hizo sampuli za binadamu na papai zinafana?

Maana mimi nilijua sampuli zinazopelekwa kwenye vipimo ni damu!!!
Kuwa mfuatiliaji wa mambo. Kuna upimaji wa aina nyingi. Kunakuchukua sampuli kwa swab puani au kooni kwa ajili ya kipimo.
 
Rais Magufuli amesema viongozi wa makanisa na misikiti wanaofunga makanisa na misikiti kwa sababu ya corona wajitathimini kama wana imani au wababaishaji

Anasema anawashangaa viongozi hao kwani biblia inaonyesha watu mbalimbali walipitia mateso ya kurushwa motoni,kwenye Simba lakini walipona na anashangaa wanaogopa nini,?

Kwamba wanaweka ubidamu mbele kuliko mungu

Pia amesema masoko,minada iendelee,haiwezi kufungwa

My take:_Wachambuzi tutegemee nini kwa hili?

Je ile social distance kwa hotuba hii itakuwa na nguvu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa km anajiamini anashindwa nini kusema shule zifunguliwe?
Huyu mzee huyu........
 
Mnataka nyumba za ibada zifungwe tuanze kuabudu mashetani? Hovyo kweli
 
Back
Top Bottom