Mtego Aliojitegea Rais Samia, nani atauvunjilia?

Unaonekana unaongea kishabiki ndugu.

1) Nani kakwambia Mama hawajui maadui zake na idadi yao?? Unamchkulia poa???

2) Yaani wewe hujui kwamba Rais ndio kila kitu ndani ya nchi hii. Kweli hujui hilo?? Unaikumbuka kesi ya uamsho??? Iliishaje???

3) Kwenye kamati kuu watu wa Mama ni wawili tu?? Like seriously? Huoni kama kuna Wazanzibari mpaka huko Njombe na Ilemela??

4) Ndugai ni wa kupuuzwa na hana nguvu yoyote mnayotaka kumpa. Walimtanguliza kikatuni chao slow slow akagonga mwamba chap kwa haraka, na hakuna yeye na genge lake walichoweza kufanya.

5) Nani aliekwambia wenyeviti mikoa sio watu wanaotakiwa kumpa imani Mheshimiwa rais?? Uliwaona Jana Ikulu?? Hivi wewe ulikuwa umekaa kwa upande gani pale??

6) Haya maneno ya watu hawako tayar kuongezwa na mwanamke ni ujinga tu. Huu ni mwaka sasa unamalizika na Mama ndie Rasi wetu

7) Mtu wenu hana namna zaidi ya kuachia ngazi tu. Sio suala la wewe kupenda au kutokupenda. Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Amir jeshi mkuu wa Majeshi ya ulinzi na Usalama na ni MWENYEKITI WA Chama Cha mapinduzi.
 
Mi nadhani mama kaona hana nafasi 2025 kwa sababu ya utamaduni wa chama chake kuwa mgombea urais anatoka bara na makamu zanzibar.kwahiyo kaamua kulipuka na ikiwezekana aaache legacy flani kwenye kipindi chake.Pia Ndugai ana damu ya kunguni.
 
Ukiisoma katiba vizuri kabisa utabaini kuwa hata huyo ndugai na wabunge wake hawana uwezo wa kumtoa rais madarakani
 
Now you are back.
We missed you bro.

Hoja hii makini sana.

Samia ameshatishwa na tetesi zinazoenea kwa kasi hivyo ameona wacha aoneshe makali kidogo..
Hivi umesikiliza hatua kwa hatua alichoongea Ndugai?! Yaani badala ya yeye kuilaumu serikali lakini ametupa makonde yake kwa Samia personally, na wala sio kama taasisi!!
 
Msamaha alitakiwa aseme kweli,sio kusema klipu iliundwaundwa,kwamba kakusema hayo na aombe msamaha,wa nini?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
My opinion anyway, there could be something fishy sported a far from presidentia advisory committee kumisslead Rais kwa manufaa yao, unajua hata mikopo inaweza kutumika kupata pesa za kupambania vita ya Urais 2025? Ni mtazamo wa kichokozi tu
 
Kwanini amebugi? Au kwasababu Rais ambae ni mwenyekiti wa chama ndie alipendekeza jina la job kugombea uspika? Hivi hatuoni haja ya kuwa na spika asiye na chama
 
Uko na point ila ina sononesha kwa mustakabali mpana muhimu wafunike Kombe shetani apite nchi ni kubwa kuliko sisi sote. Nimewaza kipumbavu kama mnyama Twiga.
 
Rais is everything in TZ tuczidanganye nafsi zetu
 
Anavimbaje wakati wenye mamlaka na kadi yako ya chama ndio wanaokupiga madongo hadharani kweupeee...kifupi Jobo hana pa kutokea....that is why KATIBA mpya ndio solution ya hizi mambo.
 
Kwa taarifa tu ni kwamba Ndugai alishaongea sana na mama private lakini hawaku-match interests,ivyo option ya Ndugai ilikuwa ni kupitia public lakini bahati mbaya uku kwenye public nako alishanyea kambi kitambo kwa matendo yake ya uongozi mbaya ivyo ana maadui wengi ndani na nje.

Ndugai angeinvest kwa wananchi na kupendwa na kuheshimika hii vita mama angeshindwa asubuhi tu
 
Kuna uwezekano wapo wengi nyuma ya Ndugai akitumika kama chambo tu, na Rais hupewa taarifa zote nyeti kwani vyombo vyote vipo chini yake.

Kaamua kumuanzishia ugomvi Ndugai ili aweze kufanya kazi kwa uhuru zaidi.

Kumbuka hii n nchi ya “mfumo dume” wapo baadhi hawaamini mpaka dakika hii kuwa nchi inaongozwa na rais mwanamke.
 
Mimi nina maoni tofauti, juu ya hili swala la hii mihimili miwili! Wakati wa JPM, ilisemekana bunge ni dhaifu na lawama zilikuwa zinaelekezwa kwa JPM. Sasa utawala wa Rais Samia, unataka kuonyesha bunge siyo dhaifu na Rais haingilii bunge (yaani kuna utawala wa sheria) - lakini tutaaminije? Ili kutuaminisha, basi zengwe hili la Spika likazaliwa. Players katika zengwe hili ni wao kwa wao, yaani CCM na mihimili husika.
Na nia kubwa, ni kuonyesha Muhimbili wa serikali haugandamizi wa bunge - Nafikiri zoezi limefanikiwa.
 
Wewe ile busara ya let us agree to disagree hauitambui kwahiyo ukipishana na kiongozi mwenzako ni unamuanika hadharani.
 
Paragraph ya mwisho umebashiri ukweli Ndugai akerwa na safari za Dodoma to Dar kila siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…