Relief Mirzska
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 13,992
- 22,396
Unaonekana unaongea kishabiki ndugu.Kosa kuu la kiufundi la Ndugai ni kuomba Msamaha.
Ila Kosa kuu zaidi la kiufundi ni alilofanya Samia kumsema Ndugai kiasi kile, au kwa maana nyingine ni kutangaza vita na adui asiyejua idadi yake.
Samia amedanganywa sana Kuwa Rais ndio Kila kitu, amesahau Bunge likiamua linaweza Kuifanya Serikali isifanikiwe kwa lolote kwa chochote.
Samia anasahau kwenye kamati kuu watu wake wa uhakika ni 2 tu labda na Wazanzibar wenzake, Bado Kwenye mkutano mkuu wa CCM hajui wapo wangapi.
Samia alidokeza Kuwa akina Ndugai walitaka hii serikali iitwe ya Mpito, Kama Ndugai aliamini anaweza kuipeleka hiyo hoja Bungeni basi, Sio wa kupuuzwa hata kidogo.
Hawa wenyeviti mikoa ni watu wasiotakiwa kumpa imani Rais.
Samia anatakiwa ajue Tanzania nzima 80% hawako tayari kuongoza na Rais Mwanamke..
Mwisho nisingependa Ndugai ajiuzulu, ila anoeshe makucha yake sasa
1) Nani kakwambia Mama hawajui maadui zake na idadi yao?? Unamchkulia poa???
2) Yaani wewe hujui kwamba Rais ndio kila kitu ndani ya nchi hii. Kweli hujui hilo?? Unaikumbuka kesi ya uamsho??? Iliishaje???
3) Kwenye kamati kuu watu wa Mama ni wawili tu?? Like seriously? Huoni kama kuna Wazanzibari mpaka huko Njombe na Ilemela??
4) Ndugai ni wa kupuuzwa na hana nguvu yoyote mnayotaka kumpa. Walimtanguliza kikatuni chao slow slow akagonga mwamba chap kwa haraka, na hakuna yeye na genge lake walichoweza kufanya.
5) Nani aliekwambia wenyeviti mikoa sio watu wanaotakiwa kumpa imani Mheshimiwa rais?? Uliwaona Jana Ikulu?? Hivi wewe ulikuwa umekaa kwa upande gani pale??
6) Haya maneno ya watu hawako tayar kuongezwa na mwanamke ni ujinga tu. Huu ni mwaka sasa unamalizika na Mama ndie Rasi wetu
7) Mtu wenu hana namna zaidi ya kuachia ngazi tu. Sio suala la wewe kupenda au kutokupenda. Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Amir jeshi mkuu wa Majeshi ya ulinzi na Usalama na ni MWENYEKITI WA Chama Cha mapinduzi.