kiranga ni kweli hapo ni sawa na kujifunga goli mwenyewe, nimetoa nafasi kushindwa hoja. By the way na stick kwenye hoja kwamba si vema kwenda ikulu huku umevaa hovyo hovyo, mivao ya ikulu inajulikana. Na pia haileti picha nzuri kuonesha udini kimavazi kama hao jamaa waliovaa kanzu za dini. Ingekuwa ni masheikh isingekuwa nongwa. Hebu fikiria inaeleweka vipi ofisi za umma sasa kila muislam aanze kuvaa kiislam kwa kuwa ni muislam na hakuna sheria ya kukataza mtindo huo wa mavazi ya kidini? Kuna wale mawaziri, wakuu wa mikoa huwa wanavalia kiislam kabisa, ni full ushungu, basi kwa wale akina mama wacha wavae hivyo maana wamefunika vichwa vyao. Sasa mwanaume unavaa kanzu na sio sheikh huoni kuwa inaleta ukakasi kuwa ni udini?