Mtoto wa kaka yangu wa kwanza (First born) amebamiza 'A' za kutosha za darasa la nne mpaka nimeogopa sana, tutafute pesa Elimu nzuri ni gharama

Elimu ya Tanzania ni changamoto mimi namlaani sana aliyeandaa mitaala ya elimu wakati ule tunasoma, walikuwa watuandaa kuwa watumwa wa CCM.
Zile nyimbo za kuisifu tanu na mwenyekiti wake matunda yake tunayaona leo
Kweli mkuu Tanzania Hamna Elimu shule za serikali sio shule.
 
Mtu alimpie mtoto mil 5 Kwa mwaka then aje awe omba omba ?

Sahau kabisa kuhusu hilo
Huyo anaongea maneno ya mkosaji ni heri mtoto awe na matokeo mazuri kuliko mtoto awe na matokeo mabovu. Haijalishi ataajiriwa au atajiajiri. Logically tu kama mtoto amefaulu vizuri hii ni kumaanisha hata muda wake anajua kuutumia vizuri na yuko focused. Ndani ya muda huo huo wa kupata elimu wakati kuna mtoto anapata A ndani ya muda huohuo kuna mtoto anapata D au C hii ni kusema huyu wa D, C hawezi kuwa na maarifa sawa na huyu wa A na ina maana huyo wa D au C hakutumia muda wake vizuri.
 
Nachojua we jamaa Una akili Sana na umeshafanikiwa hata Kama sio kuwa tajiri.


So uwezekano wa kumfanya kijana kusoma dumu fagio na kubutua A unao .
True,
Mimi sio tajiri Ila na uwezo wa kumpa maji mshikaji yeyote alie na kiu..

Kuhusu huyu dogo kuanzia Leo nataka awe DACTARI wa binadamu.

Tukiwa hai hii comment miaka ijayo ntakuja kuithibitisha...

Japo anasoma kayumba Ila nafanya mazingira afanye vyema kwenye safari za ELIMU yake..

NB.
Much appreciation Kwako tupo pamojaa
 
Huyo mtoto hizo elimu za A mnaenda kuua kipaji chake. Mfundisheni vipaji. Mimi mtoto wangu kama hawezi kutumia viungo vyake vya mwili (mikono, miguu, au mdomo) kufanya jambo fulani bado siwezi kumsifia kwamba anaakili.
 
Much 👍 appreciation 😁 Kwako... wewe ni mtu mzuri.
Thank you Mr.... nipo kawaida lakini ni matokeo ya malezi na jamii na mtu mwenyewe...

Naona watu wanabeza elimu Haina maana mbona hamna ajira na mambo mengine kama hayo....

Nikamuuliza swali kwahiyo tuache kusomesha ama wazazi wenye watoto waache kusomesha ili wote tuende kkoo ? ama tufungue mangi shop au tukalime ?

Akasema tunataka pesa.... nikamwambia ni sahihi lakini ni lazima tupate wataalamu sahihi ili hizo pesa zije ! kwenye kila fani kukiwa na ujinga tutaangamia kama nchi

Good luck 👍
 
Mtoto akipata matokeo mazuri hata mzazi/mlezi/ndugu unajisikia vizuri. Endelea kumuombea huyo mtoto kwa Mungu ili apate maarifa mazuri na aje atekeleze ule wito ambao Mungu amemuitia.
 
Sasa A za darasa la nne zitasaidia niniz?👀😒😒😒😏😏
 

Mbona kuna wamesoma St. Kayumba na A wamebamiza kuanzia la nne Mpaka kidato cha sita.

Hao unawazungumzia vipi
 
Wewe mbona ni mjinga kiasi hiki?
Kwahiyo kama ajira hamna niambie atajiajiri kwenye nini!!?

Na kama hiyo elimu inafundisha kujiajiri kwanini graduates wengi wameshindwa kujiajiri ndani ya professional zao walizosomea!!?

Au ndio Yale unasomea engineering halafu unakuja uza Duka la taka taka sawa na std 7 leaver!!?au boda Boda kama graduates wengi!!?

Sijakurupuka mkuu!!

Hao wenye vipato vya kulipa mil.5 ada wapo wangapi kwenye population!!?

Njoo na facts sio majibu mepesi!
 
Mtoto akipata matokeo mazuri hata mzazi/mlezi/ndugu unajisikia vizuri. Endelea kumuombea huyo mtoto kwa Mungu ili apate maarifa mazuri na aje atekeleze ule wito ambao Mungu amemuitia.
Atajisikia vizuri baada ya kupata KAZI au kujiajiri na kula matunda ya mtoto baada ya kumaliza elimu yake!!
 

A darasa la 4 nazo za kujivunia? Hakuna mtoto wangu ambaye mpaka la 7 ni mtindo wa A zote ; matokeo ya Primary huwa Mama yao ndo anafuatiliya zaidi!
 
Ulienda hapo kuushtua umaskini sio?
 
Mtoa mada inaonekana ukoo wenu shule ni ya kuunga, A za std 4 na 7 hata sio issue
Ingekuwa form 4&6 hapo kweli
Kuna dogo mtoto wa shemeji yangu nimemtoa St kayumba mwaka juzi akiwa la 3 nikampeleka medium ya ada isiyozidi 2mil lakini now kapata A zote
 
Benjamin Fernandez pamoja na kuwa hakufanya vizuri shule aliyosoma hapa Bongo ambaye ilikuwa ni shule ya private tena ya gharama lakini alipata msingi mzuri sana na ilimpa kujiamini na leo hii yupo na NALA yake.
Kitu ambacho nimejifunza ni kuwa uwekezaji ukiwa mzuri kwa mtoto, hii huweka msingi mzuri sana, na humpa mtoto vitu vingi sana ambavyo kwenye shule nyingi ambazo uwekezaji ni mdogo hamna.

Hapa tuelewe kuwa elimu ni uwekezaji ndiyo maana hata shule kama Weruweru miaka hiyo zilitoa watu wenye maarifa mazuri maana wakoloni waliwekeza.
Mshua wangu wakati anasoma sekondari miaka hiyo kafundishwa na waalimu toka ujerumani, UK, Japan na shule ilikuwa na nyenzo zote za kupatia elimu. Ina maana kwa leo hii shule ingawa ilikuwa ni ya serikali ingekuwa ni kama private fulani hivi. Na mshua hata akiongea tu unaona Yes huyu alipata maarifa mazuri.

Ninachotaka kusema shule iwe ya private/serikali kama hakuna uwekezaji lazima itoe product za kiwango cha chini. Sasa hapa kuna jambo moja kuna ile mtoto kusoma shule mbovu halafu still unakuta kapata ufaulu wa juu. Hii bado haiwezi kujutfy kuwa uwekezaji usifanyike maana hata huyu mtoto utakuta kuna vitu/maarifa hana pamoja na ufaulu wake wa juu.
Kwa wale ambao hawana uwezo wa kuwasomesha mtoto shule nzuri pia wasiwe wanyonge/wala kukata tamaa hapohapo anaposoma mtoto still bado mpambanie apate maarifa ya kumsaidia siyo ndo tena umuache tu mtoto iwe bora liende.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…