Mtoto wa miaka sita anagoma kwenda shule. Nini kifanyike?

We uliona wapi wazungu wakifanya hivyo??
Kwahiyo bongo zozo alimuweka mwanae ndani akamkuta anakimbia kimbia ndio akaona huyu atakua mwanariadha au sio?

Na vipi wacheza porn wa kizungu ilikuaje kuaje??
Ngoja nikupe shule kuhusu wazungu kaka ahahah
 
Tatizo linaanzia kwenye hiyo ya kudhani kupiga ndio jawabu ya kila kitu. Kaeni nae, muongee nae. Kama inaruhusiwa, mzazi akae nae shuleni siku za kwanza. Akitoka shule mpe kizawadi ( kidogo sio kikubwa) kumuonyesha kuwa mmefurahi yeye kwenda shule. Ongeeni nae kuhusu yanayoendelea shule. Kuweni karibu na mwalimu wake.

Amandla...
 
Toa viburudisho na comforts zote nyumbani. Akibaki asione katuni, hakuna kula kula, hakuna toys za kuchezea. Yaani apaone nyumbani kama Jehanamu.
 
Ukiona hivyo huyo anataka awe kama wakina dulla makabila
Kila mtoto sahv anataka kuwa msanii mkata kiuno

Ova
 
Kwanza usimpe chakula mpaka aje akitafute. Pika cha kwake hifadhi. Utagundua kitu fulani. Hata ipite siku na zaidi. T
 
Toa viburudisho na comforts zote nyumbani. Akibaki asione katuni, hakuna kula kula, hakuna toys za kuchezea. Yaani apaone nyumbani kama Jehanamu.
kwangu hakuna tv wala sabufa na wanangu gawana kawaida ya kuangalga tv wala katun
 
Mzazi unajivunia ujinga na malezi mabovu

Yaani mtoto wa miaka sita unamtuma anakataa na wewe unakenua tu wazazi siku hizi tumekuaje kwani ? Mbona tumeingiwa na upumbavu mwingi sana ( sio wewe tu wazazi wengi siku hizi hopeless kabisa ) hakuna future bila elimu/maarifa na hasa maarifa formal

Hebu usiwe mjinga ndugu kuwa baba kuanzia saizi toa kauli yenye mamlaka mwongoze mwanao


Miaka 6 anakataaje kwenda shule ?

Anyway wewe kama baba umechukua hatua Gani baada ya mwanao kukataa kwenda shule ?
 
Tunda halianguki mbali na mti
 
tafuta mwalimu wa nyumbani mfundisheni akiwa mazingira nyumbani.

kupata elimu sio mpaka mtoto avae sare abebe begi kidumu na ufagio akae kwenye kidawati aangalie ubaoni.
Mkuu; wewe ulienda shuleni halafu eti sasa unatoa ushauri wa namna hiyo. Hiyo ya nyumbani mbona ni tuition? Atapata cheti gani kama uthibitisho wa yeye kapata mafunzo stahiki? Shuleni yapo mambo mengi sio kusoma tuu bali ni pamoja na kujizoesha kuishi katika jumuia (Socialisation).
 
Hii ni muhimu sana. Pia aangaliwe na wataalam wa saikolojia ya watoto kama yupo kwenye autism spectrum.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…