Davido Amempoteza Mtoto Wake Wa Kiume #IfeanyiAdeleke Mwenye Umri Wa Miaka Mitatu 3 (Pichani).
View attachment 2403611
Kwa Mujibu Wa Ripoti Mbalimbali Ifeanyi Amefariki Kwa Kuzama Kwenye Swimming Pool Siku Chache Baada Ya Birthday Yake Oktoba 20. Amefariki Jumatatu Oktoba 31
Davido Na Chioma Walibarikiwa Kumpata Mtoto Wao Huyu oktoba 20, 2019.
View attachment 2403612
Wazazi na walezi kuna jambo la kujifunza hapo.
---
Mtoto wa mwanamuziki Davido Adeleke na mpenzi wake Chioma Rowland, Ifeanyi Adeleke (3) amefariki dunia baada ya kuzama kwenye bwawa la kuogelea ‘Swimming Pool’ nyumbani kwao.
Vyombo mbalimbali vya habari nchini Nigeria vinaripoti kuwa mtoto huyo alifariki jana Jumatatu Oktoba 31, 2022.
Taarifa zinasema Ifeanyi alizama kwenye maji kwa muda mrefu kabla ya wazazi wake hawajagundua kutoweka kwa mtoto wao na baadaye walikuta akielea kwenye maji.
Davido anakuwa msanii wapili nchini humo kumpoteza mtoto kwa kuzama kwenye maji, kwani mwaka 2018 moto wa msanii D’Banj naye alipoteza maisha katika tukio kama hilo.