Mtoto wa Rais Samia, Wanu Hafidh Ashinda Tuzo ya Mwanamke Mahiri Zanzibar

Mtoto wa Rais Samia, Wanu Hafidh Ashinda Tuzo ya Mwanamke Mahiri Zanzibar

Ushindi wake unatokana na mzazi wake kwa sababu huko nyuma hakusikika. Hata kaka yake ana jina kubwa serikalini ingawa hana cheo kinachofahamika
Wanawatumia watoto wao kuanzisha NGOs kama uchochoro wa kupitishia mali wanazoibia nchi wakiwa madarakani!! Kikwete nae alimuanzishia Mkwewe NGO ikiitwa WAMA ambayo aliitumia kwenda kuomba misaada kwa matajiri kama wakina Bill Gates wakati mumewe akiwa Rais!! Toka amestaafu mumewe umeisikia WAMA tena?
 

MTOTO WA RAIS SAMIA, WANU HAFIDH ASHINDA TUZO YA MWANAMKE MAHIRI ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke Initiative ambae pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mheshimiwa Wanu Hafidh Ameir amenyakua tuzo ya mwanamke mahiri katika kipengele cha mtendaji bora wa taasisi kwa mwaka katika kuchochea shughuli za maendeleo kwa jamii.

Mhe. Wanu ambaye ni mtoto wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amekuwa miongoni mwa wanawake washindi 17 waliopatiwa tuzo hizo ambazo hutambua mchangao wa mwanamke katika kuleta matokeo chanya.

Mhe. Wanu anasema kufanyika kwa tunzo hizo kunaibua ari na ujasiri kwa wanawake wote nchini kufanya juhudi katika kufanikisha mipango mbalimbali kwa maslahi ya Jamii zao.

View attachment 2840418
View attachment 2840420
Hunter Biden
 
Back
Top Bottom