TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 11,999
- 24,328
Leo nimetembelea shule anayosoma mwanangu, ni sekondari ya bweni. Nilichogundua ni kwamba wazazi wengi majumbani mwetu hatuwafundishi watoto kuthamini kidogo walicho nacho.
Nimekuta watoto wanatupa viatu vizuri kabisa. Wametupa mashuka na yako kwenye hali nzuri sana, wametupa nguo zao mbalimbali.
Wazazi, hata kama unadhani unaweza kumtimizia mtoto wako mahitaji yake yote, ni vyema ukamfundisha kutunza mali zake mwenyewe.
Kiatu kikichanika kishonwe na sio kutupwa, nguo zikichafuka zifuliwe, zisitupwe.
Kuna wengi wanavitamanani vitu tunavyowanunulia watoto wetu, lakini hawajabahatika kuvipata.