Mtoto wako unamleaje? Nimesikitishwa sana na watoto wa shule hii

Mtoto wako unamleaje? Nimesikitishwa sana na watoto wa shule hii

Inaumiza sana ila ukweli ndo huo....Lazima utofauti wa mtoto wa mwigulu na wangu watofautiane maisha
Mwigulu Nchemba ana hela za ofisini, siku akitoka nje ya ofisi hawezi hata kufanya biashara.

Kuna tofauti ya kuwa na hela na kuwa tajiri. Watoto tuwafundishe wawe matajiri, sio wawe na hela.

Utajiri unavuka kutoka kizazi kimoja hadi kingine, hela huja na kupita.

Kama akili yako imejengwa kwa msingi wa kuwa na mtoto tajiri, basi mfundishe kuheshimu kidogo alicho nacho.

Kama msingi wako wa akili ni kuwa tu na hela, basi mspoil mtoto wako kadiri uwezavyo. Mwisho wa siku hela zikikuishia mtoto wako atakuwa hajui kutunza wala kuzalisha mali.

Hawa watu tunawaona wana miaka 50 wanakaa kwa wazazi wao, hawawezi kujitegemea ni matokeo ya kudekezwa na wazazi wao
 
Leo nimetembelea shule anayosoma mwanangu, ni sekondari ya bweni. Nilichogundua ni kwamba wazazi wengi majumbani mwetu hatuwafundishi watoto kuthamini kidogo walicho nacho.

Nimekuta watoto wanatupa viatu vizuri kabisa. Wametupa mashuka na yako kwenye hali nzuri sana, wametupa nguo zao mbalimbali.

Wazazi, hata kama unadhani unaweza kumtimizia mtoto wako mahitaji yake yote, ni vyema ukamfundisha kutunza mali zake mwenyewe.

Kiatu kikichanika kishonwe na sio kutupwa, nguo zikichafuka zifuliwe, zisitupwe.

Kuna wengi wanavitamanani vitu tunavyowanunulia watoto wetu, lakini hawajabahatika kuvipata.
Hao watoto wazazi wao hizo hela hawazitolei jasho labda matarafiki
 
Hao watoto wazazi wao hizo hela hawazitolei jasho labda matarafiki
IMG-20230417-WA0002.jpg
 
Wafundishe busara ya kugawa kile ambacho kwao wanaona hakifai, kuwagawia wale wenge uhitaji nacho na sio kutupa.

Sio kuwaambia wakashone nguo iliyotoboka au kuchafuka au aliyoichoka.
Viatu vimebanduka, shona gawa.
 
Tatizo hadi kitu cha Mtz kiharibike ni kwamba kimechoooka
 
Kijana wa Secondari kufua nguo zake tu mtihani,nguo ikitatuka kidogo anatupa Baba atanunua nyingine!,changamoto sana malezi yetu ya kisasa.
 
Back
Top Bottom