Mtu hatoki ndani asubuhi hadi jioni lakini analipa kodi na bills zote kwa wakati

Mtu hatoki ndani asubuhi hadi jioni lakini analipa kodi na bills zote kwa wakati

Anaweza akawa anafanya kazi online... ya kumuingizia kipato au anafanya kazi flani isiyo halal,anapata pesa,ukigundulika unamfuatilia,unaweza ukauawa.Achana nae.
 
atakua anayauza online
Sasa kama hatoki ndani hayo madawa anayauzaje?

Waswahili mnapenda sana mumjue mtu ndani nje ili baadae muweze kumkashifu kwa urahisi.

mtu anaweza kuwa na vitega uchumi kama hisa, majengo kapangisha hela zinatiririka kila baada ya kipindi fulan.i
 
Nimewahi panga Nyumba fulani hivi kuna jamaa alikuwa anashinda chumbani asubuhi hadi jioni na anakula vzuri anapendeza na analipa bills zote bila usumbufu hadi majirani na wapangaji wenzie hususani wanawake walikuwa wakihisi labda anajihusisha na uuzaji madawa au ndo wale wa ile pesa tuma kwa namba hii..
Hii imekaaje wadau
Mchomeshe Kwa askari
 
Anaweza akawa anafanya kazi online... ya kumuingizia kipato au anafanya kazi flani isiyo halal,anapata pesa,ukigundulika unamfuatilia,unaweza ukauawa.Achana nae.
Haha simfatiliii nimeshare hili baada ya kuskia majirani zake wakike wakimzungumzia
 
Dunia ya leo internet ndio kila kitu,

Kuna wengine wanacheza kamali online hakuna tena anaweza kupiga hela moja tu akalipa kodi ya miaka miwili.

Kuna jamaa yupo tiktok anakaa kenya yeye anashinda online hata masaa sita lkn kwa mwezi anaweka mpunga si chini ya 20million tzs.
 
Nilikuwa nakaa nyumba moja na Wanaigeria, akitoka ndani anaenda Chooni tu, kutoka kwao nje ni usiku tu... ilipobumbulila ni pale walidhulumiana na Mbongo akawaletea pila la Polisi.
 
Haha simfatiliii nimeshare hili baada ya kuskia majirani zake wakike wakimzungumzia
Kama ni wakike,unaweza ukakuta anafanya hata uhuni wa piga video call nakukojoza kwa 15000 akipata watano,kashapata hela au rum ipo usalama upo,njoo nipo sijui wapi... au ana biashara online ya halali
 
Huyo ana mtaji wa 50 000 tu na kila siku anabeti Odds mbili za uhakika! Kwa siku anaingiza 50,000 huku anakunywa juisi ya pasheni

Hakuna odds za uhakika wakuu! Tufanye kazi
Zipo ukipunguza tamaa. Mimi napiga 30% ya 200,000 kila siku. Jiongeze....siwezi leta formula hapa maana tukijua wengi makampuni ya kubet yatafungwa
 
Kawaida hiyo. Kuna jamaa namjua amepanga na huwezi kumuona akifanya kazi kutwa yupo na fortuner new model na bebz kama wote kumbe wazazi wake walivyofariki walimuachia ghorofa kariakoo kazi yake ni kupokea kodi na kufanyia marekebisho.
Cc : ephen_
 
Zipo ukipunguza tamaa. Mimi napiga 30% ya 200,000 kila siku. Jiongeze....siwezi leta formula hapa maana tukijua wengi makampuni ya kubet yatafungwa
Sasa kama hauwezi kuleta fomula mkuu si bora ungekaa kimya?
Kwamba wakifilisika ni dada zako?
 
Nimewahi panga Nyumba fulani hivi kuna jamaa alikuwa anashinda chumbani asubuhi hadi jioni na anakula vzuri anapendeza na analipa bills zote bila usumbufu hadi majirani na wapangaji wenzie hususani wanawake walikuwa wakihisi labda anajihusisha na uuzaji madawa au ndo wale wa ile pesa tuma kwa namba hii..
Hii imekaaje wadau
Mimi ninae jirani wa hivi..ndani hatoki yeye na mke wake ila anaishi vzr tu...ni simu tu zinasikika akiongea na wateja wake.
 
Kuna jamaa mmoja mtwara mjini yeye ilikuwa mchana ni kulala tu ikifika usiku ndipo anaondoka...na alikuwa na mkewe na hata mmoja aliewahi kuiona sura yake vizuri kwasababu kuna mama mmoja hiyo siku alienda kwao aliita sana ila hakuitikiwa ile wakati anaondoka akageuka ghafla akamuona mwanamke anarudishia pazia kwaharaka
 
Back
Top Bottom