mshamba_hachekwi
JF-Expert Member
- Mar 3, 2023
- 24,943
- 81,605
Beba dumu la maziwa mgando.
Unataka kuchota maji mtoni upeleke baharini?Habari zenu wakuu.
Tufanye una ndugu au jamaa yako aliyekupita mbali kifedha, unaweza kumbebea zawadi gani ili usiende mikono mitupu? Ile imetokea tu unataka kwenda kumtembelea sio kwamba ni mgonjwa au ana changamoto yoyote.
Hapo kwenye tuvitu ndio palikuwa patamu sema upishi meyo 😁😁Angalia chakula ambacho siyo common sana kwao, ndio ubebe.
Mimi mpishi wa cake huwa nabeba cakes na cookies, nk.
Yaani tuvituvitu tu tudogo.
Kwa ambao wapo mjini nawabebea hata unga, au viazi.
Mwenye Uzi hajakosea yupo mbele ya muda zawadi yoyote atakayopekeka itarudi kwake maradufu..
Hakuna Haja Ya Kujitutumua Kwa Aliyekuzidi,,Hakuna Kwenda Na Chochote..Lakini Hakikisha Wewe Ndio Unaondoka Na Chochote Kutoka Kwake...
Maharage yasiyo na Gas mazuri sanaNdio manini
Kwenda kwa watu mikono mitupu aibu mkuu, ukizingatia hujaitwa 😁😁Unataka kuchota maji mtoni upeleke baharini?
Wewe nenda kajibebee kila kitu mahindi,kuku,mboga,yani beba usiache kitu unataka kujifanya na wewe unazo wewe umejinunulia kuku lini😒