Mtu ukiwa na pesa, somesha mwanao international schools, achana na hizi exam based schools or education

Nimesema mamako kwa vile nina uhakika mamako unamfahamu. Mimi haunifahamu. Kwa hiyo kusema mimi ni ngwini ni usanii tu.
Mama yangu kaingiaje hapa, huwezi ukawa umesoma PCM kwa design hii ya uandishi..
 
Which you can still get at the University level...
Never.
University zetu hawana tofauti na sekondari, mentality yao ni ile ile, ufaulu. Ndio maana wanafunzi wanasoma wawe na GPA kubwa basi.

Yaani usome elimu ya msingi, sekondari jumla miaka 13 halafu uje kupata exposure university kwa miaka 3? Kua serious mkuu.

Lakini kuna mahala nimeona umeseam ulisoma shule za "sirikali", nimekuelewa.
 
Hapo ume-exaggerate sana, sijajua kama ulikua unanogesha ngano yako au lah. Ni kweli hizo shule ni nzuri hasa hasa kumpa mtoto exposure na kujifunza lugha zingine kwa ufasaha kama kiingereza au kifaransa.

Ila ukija ktk uwezo wa utendaji na ufanisi sio kweli hao wanatuzidi ila wao kwa asilimia kubwa wanaonekana wako smart ni kwa sababu wanakuwa wanajifunza kwa lugha za kigeni tangu awali. Kama ukichanganya mtoto aliyesoma shule msingi Bunge na shule ya kimataifa ya Tanganyika uwapime uwezo wao kwa lugha ya kiswahili utahamaki ukweli wa mambo, ni ngumu sana mtoto anayesoma lugha ya kigeni kwa kugusa gusa awe sawa kwa kujiamini na mtu aliyesoma shule ya kimataifa kwa lugha ya kigeni.

Binafsi nimesoma shule za umma kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo kikuu, nimebahatika kufanya kazi na watu waliosoma shule za kimataifa kama Tanganyika na Moshi pia vyuo vikuu wamesoma Ivy league (Harvard, Princeton, Brown) ila sijawahi kuona utofauti mkubwa baina yao na sisi. Jaribu kwenda ofisi kama World bank country office (Mirambo 50) au auditing firms (Kpmg, delloitte, EY, PwC) au oil & gas companies huwezi kuona utofauti baina yao na sisi.

Changamoto kubwa sana niliyoigundua asilimia kubwa ya watu ambao waliosoma shule za umma kuanzia chini mpaka vyuo vikuu ni kupata shida kuimudu lugha ya kigeni kwa ufasaha hii hupunguza hali ya kujiamini kwa kiasi kikubwa sana. Labda serikali wajaribu kuboresha mitaala ya elimu lugha ya kiingereza ianze kutumia kuanzia chini yaani shule ya msingi na sio kuanzia sekondari. Watumie mfumo unaotumika kwa shule za msingi kama Bunge, Mlimani na Olimpio.
 
Kwa sababu wao ni international level.

Huwezi waona au wasikia bongo
International ni wapi mzee
Ninavyojua unavyoongelea international ni kama wasafi wale ni international na wengine maarufu Sana yani ndani na nje hata Kama mtu yuko nje tutamjua kwa umaarufu wake kupitia huko alipo
 
Talent zipi nazani unazungumzia za Ku rap, Hahaaa tupe talent tofauti na za kuimba.

International watoto wanapata Exposure kubwa sana
Talent ni nini
Na wewe ndiyo utupe mifano ya hao ma international scholars waliokuzwa vipaji vyao mashuleni kwao tuwaone kitaifa na wawe wakubwa kimataifa sio kusifia tu hizo shule nadhani wengi wao wanaishia ama kusimamia biashara za familia zao au kupewa nyazifa kwenye serikali ambao labda wazazi wao ni viongozi na wengine kuajiriwa nje huko ambayo inawakuta hata waliosoma shule za kata na ku scholarship

Lakini katika mpira, mziki, uigizaji, ngumi,dancerz na vipaji vingine vingi ni akina sisisi tu na Kama ukimkuta huko
Aliyesoma international kwenye familia huwenda wanamuona Kama kapotea vile
 
Ni sawa lakini inasemwa katika huu uzi kwamba international school inakuza vipaji tofauti na shule zetu hizi
hatuzumguzii kufundisha vipaji vipaji havifundishwi wote tunajua hilo ndiyo tukaomba mfano wa watu ambao kusoma international kumewasaidia kukuza talent zao na wao wakaenda kimataifa
 
Teh teh teh we jamaa umenichekesha sana
 
Umeongea ukweli,ila ni wachache sana wataelewa unachomaanisha...
 
Hivi inamaana hatuwezi kubadilisha mitaala ya hizi shule zetu ziwe kama za kimataifa. Najiuliza tu. Kwani hatuwezi au ni nini shida
Inawezekana ingawa litachukua miaka mingi sana,elimu hiyo ilikuwepo tena kwenye shule za kawaida sana,ikafa miaka ya 80 mwishoni,ikabakia ile ya mwenye uwezo mkubwa wa kukariri au kuweza kupitia mitihani mingi ya miaka ya nyuma ndio mwenye akili...
 
Wazazi tusake hela jamani watoto wetu wakasome kwenye shule bora, mwezi wa 7 nilikutana na binti mmoja hapa Johannesburg akiwa anajiandaa kurudi Tanzania kwa sababu ya restrictions za covid-19. Huyu bunti amesoma primary na secondary Aga Khan international school ambapo wanatumia mtaala wa Cambridge. Baada ya hapo akaja kujiunga Stellenbosch University iko cape town (1 ya top 3 universities hapa SA).

Anakotoka hela ipo sio kidogo na hapo chuo ada kwa mwaka ni around 20m za kitanzania plus accommodation na extras nyingine. Binti anajiamini huku akijua anachokifanya,anachukua degree ya Mambo kilimo na economics na akimaliza mwakani ana job offer Canada.

Naendelea kuzisaka hela mwanangu at least apite njia kama ile, makapuku tunanyongwa kielimu ndiyo maana wanasiasa hawapeleki watoto zao shule za kawaida za serikali. Pesa tu ya kugharamia elimu bora ndiyo ticket ya kumfanya mwanao aje akae kwenye high table ya maisha.
 
Ungeanza walau kuzilist Shule chache kwa manufaa ya wadau ili wajipange
 
Shida ingine ni ada ya hizi Shule
 
Hivi inamaana hatuwezi kubadilisha mitaala ya hizi shule zetu ziwe kama za kimataifa. Najiuliza tu. Kwani hatuwezi au ni nini shida
Mtaala kuubadilisha inawezekana ila changamoto ni:
1.Wanaopaswa kuubadilisha wanajua wabadilishe nini? Wako na hiyo elimu?
2. Gharama za kuuendesha huo mtaala kama: vifaa vya kufundishia, ziara za ndani na nje ya nchi za kimasomo wazazi watazimudu?
3. Serikali inaouwezo wa kuweka miundo mbinu n.k?
4. Wazazi wana uwezo wa kugharamia ada na michango mingine? Iwapo sasa hakuna ada ila uniforms zinawashinda wazazi mfano viatu n.k?
 
Hili linahitaji mchakato mzito haswaaaa
 
Hivi inamaana hatuwezi kubadilisha mitaala ya hizi shule zetu ziwe kama za kimataifa. Najiuliza tu. Kwani hatuwezi au ni nini shida
Mitaala ya kimataifa iendane na miundombinu ya kitaifa
 
Sisi tabaka la kati tukijivuta saaana basi angalau watoto wetu wanasoma hizi saint saint nani sijui, tunaona angalau kuliko ile elimu bure.... hizo za kimataifa ni chache na gharama sana.

Mchawi pesa.
 
Mkuu kuna world scholars kibao ambao hawajakanyaga hizo international schools na wanaheshimika kwenye field zao. Nafikiri hizo shule zimeanzishwa purposely kwa ajili ya watoto wa mabalozi kwenye nchi husika, hakuna jipya...
Hao ni outliers tu na huwezi kutoa conclusion based on them. Asilimia kubwa humu tumesoma shule hizi duni ila ukweli ni watoto wa huko shule zenye mitaala ya mabeberu wapo vizuri. Huku kwetu ni karama ya Mungu tu unakuta mtu yupo very articulated
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…